Habari na Maoni
Habari:
Mnamo Mei 2025, mamlaka ya Tanzania iliwaweka kizuizini mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi na wakili wa Uganda Agather Atuhaire walipokuwa wakijaribu kuhudhuria kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu jijini Dar es Salaam. Amnesty International ilitoa wito kwa serikali ya Tanzania kuchunguza kukamatwa kiholela, kuteswa, kuzuiliwa bila ya mawasiliano na kufukuzwa kwa nguvu kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
Maoni
Tukio hilo liliibua hasira kubwa nchini Kenya na Uganda, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu ndani ya kanda hiyo na nje ya nchi yakitaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya kudhulumiwa kwa wanaharakati hao. Ofisi ya Masuala ya Afrika ya Marekani ilisema kwenye mtandao wa X “imesikitishwa sana na ripoti za unyanyasaji” wa Atuhaire na Mwangi wakiwa Tanzania. “Tunatoa wito wa uchunguzi wa haraka na kamili kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu,” ilisema, na kuzitaka “nchi zote za kanda hiyo kuwawajibisha wale waliohusika kukiuka haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mateso. Mitandao ya kijamii imekuwa uwanja wa majibizano makali kati ya raia wa Kenya na Tanzania, huku baadhi ya wabunge wa Tanzania wakiwashutumu Wakenya kwa unyanyasaji mtandaoni na kuingilia masuala ya ndani.
Ni dhahiri shahiri kuwa ukoloni mamboleo ni moja wapo ya mikakati ya kisasa ambayo ipo na inaendelea kupitia mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uingiliaji kati wa kibinadamu, masharti ya misaada, shughuli zisizo za kiserikali, na diplomasia ya nguvu laini. Nchi za Magharibi kwa kisingizio cha kutetea haki za binadamu zimeimarisha uundaji upya wa jamii za Kiafrika ili kuakisi miundo mbovu ya Kimagharibi ya kiliberali kama vile LGBTQ. Hasa, Kenya ina idadi kubwa ya mashirika ya kutetea haki za binadamu ambayo yanakuza mifano ya nchi za magharibi. Kisiasa, mataifa ya kigeni yanaendelea kuwa na ushawishi au Afrika chini ya kivuli cha haki za binadamu. Zaidi ya hayo matamshi ya kimagharibi ya kutetea haki za binadamu yanaonyesha viwango vyake viwili vya tawala za kimagharibi ikiwemo ‘mtetezi wa haki za binadamu’ wa Marekani. Huko Gaza, nchi za magharibi sio tu zimekaa kimya lakini zinaunga mkono kundi la Kiyahudi la mauaji ya halaiki ambalo linatekeleza mauaji ya kutisha.
Kuhusu vita vya mtandaoni kati ya Kenya na Tanzania huku kila mmoja akijigamba kuwa ni mstaarabu na ameendelea kuliko mwenzake, hii ni moja ya magonjwa hatari ya Utaifa. Kuna aina mbili za Utaifa ambazo ni vifungo vya kifisadi: Utaifa wa Kitaifa ambao unamaanisha hisia ya kiburi na ubora unaohusishwa na hisia ya kuwa wa eneo fulani kwa kuzaliwa au uraia. Kuna nyingine ni Cultural Nationalism; ushirikiano wa kipengele cha ziada yaani utamaduni maalum kwa eneo na hisia ya kujivunia inayotokana na muungano huu. Ukweli tu kwamba dhana ya juu juu ya utaifa imepata mvuto mkubwa inazungumza juu ya udhaifu wa kiitikadi wa ubepari na kutokuwa na uwezo wa kusimamia na kutatua shida za kibinadamu na kijamii.
Mkakati wa kikoloni “Gawanya utawale” (au divide et impera) umetumiwa sana na mabepari kudumisha udhibiti wa maeneo ya Afrika-na athari zake bado zinaonekana leo. Kanuni ni rahisi: kukuza migawanyiko kati ya vikundi vya wenyeji ili kuzuia upinzani wa umoja, na hivyo kupata utawala wa kigeni. Wanasiasa wenye mawazo ya kibepari wa ndani katika nchi zote mbili hutumika kama mawakala wa nchi za Magharibi katika kupora rasilimali nyingi na hivyo kuwafanya raia wao kuwa katika umaskini uliokithiri. Katika nchi za Kiislamu ni mpango wa Sykes-picot ambao umesababisha kudorora kwa kisiasa na kiuchumi kwa umma wa Kiislamu.
Kazi iliyo mbele ya watu wa Afrika mashariki ni kuzikomboa fikra zao kutoka kwenye minyororo na surua ya fikra ya utaifa na ufilisi wa wanasiasa (watawala na wa upinzani) kwani wote hao ni wamoja wakiamini mfumo fisidifu wa kibepari. Kinyume chake Umma unatikiwa kuamini mfumo na fungamano sahihi unazotokana na Uislamu kwa fungamano hili kiasili huvuka vizuizi vya mipaka ya Kitaifa. Hili ndio fungamano ambalo ndio dhamana inayoweza kuwaunganisha watu katika jamii iliyo imara na yenye umoja.
Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
na Shabani Mwalimu
Mwakilishi wa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir nchini Kenya