Mikopo ya mfumo wa Riba wa Kibepari huleta  maafa zaidi ya Kiuchumi

Habari na Maoni

Habari:

Kenya imepata mkopo wa shilingi bilioni 40 kutoka taifa la Uchina kwa lengo la kuendeleza miradi iliokwama katika majimbo 15. Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti bungeni Ndindi Nyoro amesema makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu mkopo huo itawafanya wanakandarasi waweze kurudi kwenye maeneo ya miradi mara tu uingiapo  mwezi wa Septemba.

Maoni:

Ni harakati za mabadiliko ya kimuundo ya uchumi wao zinazoifanya nchi kama Kenya kuingia ndani ya shindikizo la kuomba hatua inayozidisha viwango vya madeni. Kwa madhumuni ya kuanzisha mabadiliko ya kiuchumi, mataifa mengi ya Afrika hulazimika kuekeza pakubwa kwenye miundo mbinu ambayo ufadhili wake ni kupitia kukopa ndani na nje ya nchi. Kwa muktadha huu, serikali ya Kenya ndio imeamua kuchukua tena mkopo kutoka china. Izangitiwe kwamba katika mwaka wa fedha uliotamataika hivi punde   tayari Kenya shilinigi bilioni 152.69 kulipia deni lake la china hali inayomlimbikizia mlipa ushuru mzigo wa kulipa mkopo uliochukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Utawala wa Ruto ulipoingia madarakani August 2022 deni la nje la nchi lilikuwa kima cha takriban$62 bilioni,hii ikimaanisha asilimia 67 ya pato jumla lake. Uongozi uliopita ambapo Wiliam Ruto alihudumu kama naib rais ulikopa mikopo mingi kutoka kwa nchi kama vile China kufadhili miradi mbalimbalii ya miundo mbinu ikiwemo barabara ya reli inayounganisha Nairobi na Mji wa bandari wa Mombasa. Mingi ya mikopo hiyo ilikuwa ya kibiashara, ikimaanisha kuwa ilikuwa na viwango vya juu vya riba. Wakati huo huo, miundombinu haikuweza kuleta mapato yaliyotarajiwa. Kibaya zaidi, viongozi wengi wa Kiafrika wanaokopa fedha kutoka nje ya nchi, hupora fedha hizo kwa matumizi binafsi, na kuwaachia madeni raia wanaowatawala.

Kwenye maandamano ya miezi miwili iliopita ambayo yaliyopelekea watu kuuwawa, mabango ya waandamanaji yalishtumu shirika kuu la fedha duniani (IMF)na benki kuu ya dunia kwa kuwa taasisi hizo mbili ndio zilizochangia maafa haya. Moja katika ya mabango hayo yalibeba ujumbe: “ IMF na Benki ya Dunia sitisheni utumwa wa kileo” . Kwa hakika ni wazi kuwa maandamano hayo ni natija ya sera mbovu za Kibepari kama vile kuongeza kodi na kutafuta mikopo ambayo imesababisha maumivu na matatizo makubwa sio tu nchini Kenya bali dunia nzima. Ni dhahiri kwamba kutafuta mikopo ilikuwa chombo cha kubuni kilichotumiwa na nchi za magharibi ambao walikuza kikundi kidogo cha watu wa ndani (viongozi) ambao wangeunganisha nguvu za kisiasa na kibiashara ili kudhibiti uchumi wa nchi za dunia ya tatu kama Kenya.

Kuondokona na jinamizi la kukopa, Kenya na ulimwengu kwa ujumla inahitaji mfumo mpya wa kiuchumi ambao si mwingine ispokua mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu unaozingatia zaidi usambazaji wa mali badala ya uzalishaji na ulimbikizaji wa mali ndani ya tabaka maalumu. Zaidi ya hayo, kwa kutumia mfumo wa fehda  inayotokana na dhahabu na fedha pekee, mikopo inayotokana na riba haina nafasi itafanya mikopa ya riba isichukuliwe kabisa katika mfumo wa Kiislamu wa Kiuchumi. Kwa hakika mfumo huu wa kipekee utatekelezwa chini ya Dola ya Khilafah (Ukhalifa) ambayo itarejeshwa kwa njia ya Mtume Muhammad (saw).

 

Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut -Tahrir Na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut-Tahrir Kenya