Msikiti Al-Aqsa Ni Qiblah Chetu cha Kwanza na Mji Mkuu wa Khilafah lakini Umbile la Kiyahudi ni Mvamizi wa Ardhi Yetu na Adui wetu Milele!
Mnamo Jumatatu, 21 Septemba 2020 The EastAfrican iliripoti kwamba Amerika imeiambia Kenya kuwa iunge mkono umbile la Kiyahudi ‘Israel’ au isahau makubaliano ya biashara huru. Hii inakuja wiki moja tu baada ya kutiwa saini ule unaoitwa mkataba wa kutambua baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ikiwakilishwa na Waziri wa Kigeni, Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan na Bahrain ikiwakilishwa na Waziri wa Kigeni, Abdullatif bin Rashid Al Zayani pamoja na umbile la Kiyahudi likiwakilishwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu mjini Washington D.C, Amerika wakishuhudiwa na Rais wa Amerika Trump na wageni wengine waalikwa mnamo Jumanne, 15 Septemba 2020 (Al Arabiya, 15/09/2020).
Makubaliano hayo ya ukhaini yanafuata nyayo za usaliti za waliowatangulia kama ifuatavyo:
Kwanza: Mnamo Jumatatu, 26 Machi 1979 – Rais wa Misri, Anwar Sadat na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Menachem Begin walisaini makubaliano ya amani mjini Washington D.C wakishuhudiwa na Rais wa Amerika Jimmy Carter.
Pili: Mnamo Jumatatu, 13 Septemba 1993 – Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) likiwakilishwa na Mahmoud Abbas (Rais wa sasa wa Mamlaka ya Palestina) na umbile la Kiyahudi likiwakilishwa na Waziri wa Kigeni, Shimon Peres walisaini makubaliano ya amani mjini Washington D.C wakishuhudiwa na Rais wa Amerika Bill Clinton, Mwenyekiti wa PLO, Yasser Arafat na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Yitzhak Rabin.
Tatu: Mnamo Jumatano, 26 Oktoba 1994 – Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Yitzhak Rabin na Waziri Mkuu wa Jordan, Abdelsalam al-Majali walisaini makubaliano ya amani huko Araba wakishuhudiwa na Rais wa Amerika Bill Clinton, Rais wa umbile la Kiyahudi, Ezer Weizman na Mfalme wa Jordan, Hussein bin Talal.
Makubaliano ya hivi majuzi ni kudungwa kwa uchungu moyo wa Uislamu na Waislamu kwani Ardhi Tukufu ya Palestina ni sehemu ya Isra’ na Mi’raj ya kipenzi chetu Mtume (saw). Al-Quds kwanza ilikombolewa na Umar al-Faruq (ra) kama Khalifah wa pili chini ya kamanda Abu Ubaidah mnamo mwaka 638 Miladi na ikakombolewa tena mara ya pili chini ya kamanda Muislamu Salahuddin al-Ayyubi mnamo 4 Julai 1187 katika Vita vya Hattin. Tangu kukombolewa kwake na Khilafah ya Umar (ra) inabakia kuwa ardhi ya Waislamu na hakuna anayeweza kuiondosha haki hiyo tuliyopewa na Mwenyezi Mungu (swt) kupitia ushindi Wake wa kukata dhidi ya Ukafiri na Makafiri.
Kenya ni dola ya kisekula ya kidemokrasia ambayo maamuzi yake yanatagemea ushawishi kutoka nje wa Wamagharibi wakoloni hususan Uingereza na Amerika. Hivyo basi, Kenya inabakia kuwa ni dola nyenyekevu ambayo inatekeleza ajenda za kikoloni juu ya watu wake kama vile vinavyoitwa Vita dhidi ya Ugaidi na Misimamo Mikali ambavyo vinadhaminiwa na kuungwa mkono na mabwana zeke Wamagharibi. Katika mchakato huo Uislamu na Waislamu wanabaguliwa, wanafedheheshwa na mali zao zinachukuliwa na kuporwa na damu zao kumwagwa pasina kuhesabiwa! Haijapotea katika akili za Waislamu kwamba Kenya inakwenda mbio kuungana na mabwana zake kila inapoamrishwa kufanya hivyo. Na ndio maana mnamo Jumatatu, 14 Mei 2018 Kenya ilijiunga na nchi nyingine kuhudhuria sherehe za kuadhimisha kuhamishwa kwa ubalozi wa Amerika kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem kufuatia tangazo la Rais Trump kwamba Jerusalem ilikuwa ni mji mkuu wa umbile la Kiyahudi mnamo mwanzoni mwa Disemba 2017 (The Star, 16/05/2018)! Msimamo wa Kenya ni ule wa Uingereza nao ni suluhisho la dola mbili na Umbile la Kiyahudi litambuliwe ndani ya Palestina. Hivyo basi, umbile la Kiyahudi liliweka jiwe msingi la Ubalozi wake mjini Nairobi mnamo Disemba 1963 pale ambapo Waziri Mkuu wa Kenyatta, Jomo Kenyatta alipokutana na Waziri wa Kigeni wa wakati huo wa umbile la Kiyahudi, Golda Meir.
Hivyo basi, huu msukumo mpya wa Amerika kuitaka Kenya kuiunga mkono umbile la Kiyahudi waziwazi sio jambo la kushangaza kwa kuwa ni njama tu ya kuipa fursa Kenya kuokoa sura na kuhalalisha maamuzi yake. Inatambulikana wazi kuwa Amerika huamiliana na mataifa mengine kwa msingi wa utumiaji kifua na vitisho ikilinganishwa na dola nyingine za kikoloni kama vile Uingereza na Ufaransa ambazo kwamba hutumia diplomasia nyuma ya pazia kimya kimya ili kutekeleza ajenda yake na kuamua kutumia kifua na vitisho ikiwa hakuna budi. Lakini Kenya tayari ni mshirika katika uhalifu kwa kuwa sera yake ya kigeni inashawishiwa kwa njia ya moja kwa moja na isiyokuwa ya moja kwa moja kutegemea maslahi na manufaa ya mabwana zake Wamagharibi wakoloni. Ama kuhusiana na Makubaliano ya Biashara Huru (FTA) ambayo Amerika imeyawekea masharti hayo, anayetarajiwa kupoteza ni Kenya kwa kufanya biashara na Amerika ni sawa na tone baharini.
Kwa kutamatisha, hali ya Uislamu na Waislamu duniani ni kama yatima anayeshambuliwa kutoka kila kona ya dunia. Au ni kama mbuzi aliyepotea njia na kuokotwa na mbwa mwitu na fisi walio na njaa! Vilio vimeshamiri kuanzia Somalia, Uzbekistan, Xinjiang, Urusi, Syria, Libya, Kashmir, al-Quds, Tajikistan, Afghanistan n.k. vinalilia ukombozi wa kweli. Ukombozi kutoka katika utumwa wa kimfumo na mateso yanayotekelezwa na maadui wa Uislamu na Waislamu wakiongozwa na Amerika duniani kote. Kujitoa katika minyororo ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake ovu kunahitaji mfumo mbadala ulio na uwezo wa kuufutilia mbali mfumo wa kisekula wa kirasilimali uliofariki na unaosubiri kuzikwa rasmi. Mfumo wa Kiislamu unaotoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) Muumba na Mpangiliaji wa ulimwengu, mwanadamu na uhai. Dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamima kwa njia ya Utume ndio mbadala pekee uliowahi kujaribiwa na kufaulu kwa zaidi ya karne 13 kuweza kuwa ngao na mlinzi wa Uislamu na Waislamu damu zao, mali na matukufu yao kama vile Ardhi Tukufu ya Palestina, sehemu ya Isra’ na Mi’raj ya kipenzi chetu Nabii (saw). Khilafah itayaunganisha majeshi ya vijana mukhlisina wa Ummah wa Kiislamu ambao wako tayari kufa kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Khilafah itaandaa wanajeshi wawe na utambulisho wa Kiilslamu kama vile walivyokuwa Sa’d ibn Muadh, Abu Ubaidah, Khalid ibn Walid, Salahuddin al-Ayyubi n.k. ambao ni watiifu kwa Dini yao na sio mabwana Wamagharibi wakoloni na ajenda zao ovu. Kwa kuongezea nidhamu ya elimu ndani ya Khilafah itazalisha watawala mukhlisina na wanachuoni ambao ni warithi wa kweli wa mitume na sio wale tulionao katika watawala na wasomi vibaraka ambao wameuza akhera yao kwa thamani ndogo ya dunia hii ya muda mchache. Hapo ndipo itakapokuwa hakuna atakayejaribu kuwaotesha kidole au kupiga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu kattu!
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir