MSIMAMO WA KIISLAMU JUU YA KUWATWII VIONGOZI WAOVU!

Katika Uislamu, uongozi ni amana kubwa inayotakiwa kujengwa juu ya Aqidah sahihi ya Kiislam,na kutekelezwa juu ya msingi wa Qur’an na Sunnah.

Japo Kwa masikitiko makubwa,kwa kuondolewa makusudi fiqhi ya ya siasa,au muamalat na wakoloni wakishirikiana pamoja na watawala waovu vibaraka,Ummah umepoteza dira sahihi juu ya suala la amana hii.

Amana inayojulikana sana,ni Ile ya upande wa muamala wa kifedha na uaminifu pekee!

Huku suala la amana ktk utawala na uongozi,likipuzishwa kwa kufichwa makusudi na tawala chafu.

Japo,Ar Rasul Saw alitufafanulia vyema,dhahiri shahiri suala la amana ktk uongozi،ili Ummah wake,uishi kwa salama bila hofu wala wasi wasi wakunyanyaswa pale alipoamrisha Ummah wake kuichunga amana ya uongozi, utawala na madaraka:

عن ابي هريرة رضي الله عنه قال:

قال النبي صلى الله عليه وسلم:

*”إذا وُسِّدَ الأمرُ إلى غيرِ أهله، فانتظرِ الساعةَ.”*

) رواه البخاري(

UFAFANUZI WA WANAVYUONI JUU YA MAUDHUI HAYA:

1)AL IMAAM Ibn HAJAR AL-‘ASQALANI  Alisema kuwa: “al-amr” ni uongozi,mamlaka au madaraka.

“Ghairu ahlihi” ni wale wasiokuwa na sifa ya kielimu, kiakhlaqi na kitaasisi.

Anasema hii ni alama ya ujinga, dhulma na kuporomoka kwa jamii ambayo huleta fitna, migogoro na kuondoka kwa baraka.

2)AL IMAAMU NAWAWI:

Alifafanua kuwa hii ni ishara ya mwisho wa zama, na siyo tu mwisho wa dunia, bali pia mwisho wa uadilifu katika jamii.

3)AL-QURTUBI:

Alieleza kuwa mtu anapopewa jukumu kubwa bila elimu au uadilifu,basi hukumu,sheria,na maadili ya watu huanguka jamii huingia katika uharibifu wa kiroho na kimaadili.

 

Mpaka hapa,yabainika wazi kuwa,ni suala lenye mizizi ndani ya Aqida.Hivyo basi, Ummah lazima ujue kuwa:

1.Uongozi si nafasi ya heshima tu,ni dhimma, majukumu na amana,ambayo wataulizwa walivyo itekeleza siku ya Qiyama.

2.Kukabidhi uongozi au madaraka kwa wasiostahiki, ni kuitendelea Dini  khiyana.Kando na kuwa,sababu ya kuporomoka kwa Ummah.

3.Ni wajibu kwa Ummah kuhakikisha kuwa uongozi unakabidhiwa kwa wenye sifa za Kiislamu juu ya kiongozi.

4.Ni alama ya maangamizi pale watu wanapopuuza misingi ya mafunzo haya.Kwani watakuwa wachangia kuivunja Dini.

MITAZAMO WA KISIASA WA KIISLAMU

1.Utawala kwa Uislamu ni Wajibu

Uislamu umeweka masharti madhubuti kwa wanaostahiki kuongoza,kwa sababu,uongozi na utawala,si wadhifa tu,bali njia ya kuhifadhi,kusabaza na kutabikisha Dini.

Hivyo,wanaokabidhiwa au kutwaa wadhifa hio,lazima wawe na sifa zilowekwa na Sharia wacha Mungu,zitakazo kuwapa uwezo wa kisiasa kuongoza kwa Qur’an na Sunnah bila hofu au kuzembea.

2.Viongozi wa leo ni mfano halisi wa Hadith hii.

Leo,badala ya kuwa na kiongozi mmoja,kama Uislam unayotuamrisha,tunaona watawala wengi ulimwengu wa Kiislamu wote,

wamekabidhiwa mamlaka bila sifa halali: hawahukumu kwa Uislamu, wanatumikia wakoloni, wanapendelea familia zao, na wanawanyima Ummah haki zake. Hawa ndio “ghairu ahlihi” walioashiriwa na Ar Rasul Saw

Hadith “إذا وُسِّدَ الأمر إلى غير أهله فانتظر الساعة ni onyo la Ar Rasul Saw,kwa Ummah wake:ikiwa mtaacha misingi ya Uislamu katika kugawa uongozi, basi mtaingia kwenye maangamizi.

Ni wajibu wetu kurudisha uongozi kwa watu wenye sifa kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume (SAW)

Kiongozi wa Kiislamu (Khalifah/Imaam au Amir) lazima atekeleze Uislamu kikamilifu katika maisha ya watu, ndani ya dola ya Kiislamu (Khilafah),na pia kubeba jukumu la kuisambaza njee,kwa Daawah na jihad

Kwa msingi huu, utiifu kwa kiongozi unakuwa na masharti madhubuti.

1.Utiifu Unalazimika tu kwa Kiongozi anayetawala kwa mfumo sahihi wa Kiislamu.

ALlah Swt Asema ktk kitabu Chake kitukufu:

*يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

 

Enyi mlioamini! Mtwiini Mwenyezi Mungu, na mtwiini Mtume, na wenye mamlaka(viongozi) miongoni mwenu.Ikiwa mutakhitalifiana katika jambo lolote, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa nyinyi munamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.Hayo ndiyo bora zaidi na yana mwisho ulio mzuri zaidi.

(Surat An-Nisaa, 4:59)

Mtume (SAW) amesema:

“Yeyote miongoni mwenu atakayemtii kiongozi,basi amemtii mimi.Na anayeniasi mimi, basi amemuasi kiongozi wake.Na kiongozi wenu akiamrisha kwa yale ya ucha Mungu,basi msikilizeni na mtiini.”

(Bukhari na Muslim)

Hii inaonyesha kuwa utiifu unalazimika tu ikiwa kiongozi anawaongoza kwa Uislamu,si kwa mfumo wa kikafiri kama demokrasia, ukoloni au ujamaa.

2.Haram Kuwatii Viongozi wanaotawala kwa mfumo wa kikafiri

Allah Swt Asema:

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allah, basi hao ndio makafiri.”

(Surat al-Ma’idah: 44)

Hii inaonyesha wazi kuwa kiongozi anayehukumu kwa mfumo usiotokana na Uislamu ni kafiri, fasiki au dhwalim,na haifai kutwiiwa.

Kuwatwii ni kuridhia ukafiri,ufisadi na dhulma zao.Jambo ambalo Sharia,hairuhusu

3.Kukataa Dhulma ni Wajibu,Sio Hiari

Ar Rasul Saw amesema:

“Bora ya jihadi ni kusema neno la haki mbele ya mtawala dhalimu.”

(Abu Dawud,Tirmidhi)

Hii inaonesha kuwa si tu haifai kuwatii viongozi waovu,bali pia ni lazima kupinga dhulma yao kwa njia ya kisiasa, kifikra na ujuzi,lakini kwa msimamo mkali.

4.Sulhu ni Kusimamisha Dola ya Khilafah Rashidah.

Suluhisho la kudumu,siyo kubambanya marekebisho ndani ya mfumo wa kisekula,au kufuata kipofu viongozi waovu kwa kisingizio cha umoja,kuepuka fitna,bali ni kuung’oa mfumo mzima wa kisekula na kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Ar Rasul Saw.

Kwa kujitolea kihali na mali,kyk ulinganizi wa kisiasa na kielimu kwa watu na majeshi.

Enyi Waislam!

Kwa mujibu wa mafunzo sahihi ya Dini yenu juu ya suala la fiqhi ya  siasa,uongozi,madaraka na utwala ktk Uislam,haitakiwi kuwatii viongozi waovu wanaotawala kwa sharia za kikafiri,au kutekeleza mambo  yenye kukhalifu Sharia: Qur:an na Sunnah.

Bali ni wajibu wa Waislamu kufanya kazi ya kisiasa ya kuwang’oa na kusimamisha utawala wa Kiislamu wa Khilafah kwa njia ya Mtume (SAW)

Na hapa  kuna mfano mzuri wa tukio la kutomtwii Wala kumsikiza, kiongozi atakae kuamrisha jambo lenye kutofautiana na mafunzo ya Qur’an na Sunnah.

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Bukhari: Ametusimulia Sadqa bin al-Fadl, akasema: Ametusimulia Hajjaj bin Muhammad al-A‘war, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ya‘la bin Muslim, kutoka kwa Sa‘id bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ‘Abbas akisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mtwiini Mwenyezi Mungu, mtwiini Mtume, na wenye mamlaka miongoni mwenu”.

Aya hii iliteremka kuhusu ‘Abdullah bin Hudhafa bin Qays bin ‘Adi, wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu Saw alipomtuma akiwa kiongozi wa jeshi (sariyya).

Walipotoka pamoja naye, aliwachukia kwa jambo fulani. Akawaambia: “Je,si Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaamuru kunitwii(kiongozi)?”

Wakasema: *”Ndiyo.”

Akasema: “Nikusanieni kuni.”

Walifanya hivyo, kisha akawasha moto na kusema:

“Nawaamuru kwa jina la utiifu kwangu,muingie motoni.”

Watu wakaanza kujiandaa kuingia.

Lakini kijana mmoja miongoni mwao akasema: *”Hakika nyinyi mumemkimbilia Mtume wa Mwenyezi Mungu Saw,ili kuokoka na moto huu.Basi msifanye lolote mpaka mumfikie Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akiwaamuru muingie humo, basi ingieni.”*

Walipomfikisha habari Mtume, akawaambia:

“Lau mngeliingia humo, musingetoka kamwe.Hakika utiifu ni katika mambo ya mema (ma’ruf tu).”

(Bukhari na Muslim kupitia kwa al-A‘mash).

Abu Dawud amesema: Ametusimulia Musaddad, kutoka kwa Yahya, kutoka kwa ‘Ubaydullah, kutoka kwa Nafi‘, kutoka kwa ‘Abdullah bin ‘Umar, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) alisema:

“Kusikia na kutii ni juu ya Muislamu, katika anachokipenda na anachokichukia, maadamu hajaamrishwa kufanya maasi. Ikiwa ataamrishwa kwa maasi, basi hakuna kusikia wala kutii.”

Hadithi hii pia imesimuliwa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Yahya al-Qattan.

Na kutoka kwa ‘Ubadah bin as-Samit amesema: Tulimpa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) kiapo cha utii katika hali ya kupenda na kuchukia, katika hali ya wepesi na ugumu,na hata tunapotengwa (na haki zetu), na kwamba tusipingane na wale waliokabidhiwa uongozi.

Akasema:

Ila mutakapoona ukafiri wa waziwazi, ambao muna ushahidi wa wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yake.”

Imepokelewa na Bukhari na Muslim.

Mtazamo wa haraka haraka juu ya haki ya Ummah,waonyesha machungu juu ya hali ya watawala waovu wenye kutawala kimabavu juu ya Ummah,na wanaodhihirisha maovu hadharani,bila kujali mafunzo ya Dini.

Na huku,kukipatikana wasomi matata wa watawala,waliovaa vazi la Dini,wenye kuwaunga mkono kwa kupotosha dalil za Kisharia,ili kuwahadaa Ummah kuwafuata na kuwatwii waovu hawa

Tofauti kabisa na alivyotufunza Ar Rasul Saw,na walivyofanya maswahaba ra

Kuhusiana na kusikiliza na kuwatii watawala, hasa pale wanapodhihirisha uovu na uchafu.

Enyi Waislam wapendwa!

Ni kweli kabisa,kuwa katika Uislamu, ipo amri ya kuwasikiliza na kuwatii viongozi wa Kiislamu.Kisha hata ktk mambo Muislam anayochukia binafs.Lakini utiifu huo,ili upate kutekelezwa,umebanwa na masharti ya Kisharia:

1.Iwapo wanaamrisha mema (ma’ruf). Mtume (saw) alisema:

“Utiifu uko katika mambo yaliyo mema (ma’ruf).”

(Bukhari na Muslim)

Ikiwa, maswahaba watukufu Ra, walokataa kumtwii kiongozi mwema Umar bn Khattab Ra,mpaka awaeleze,ilikuwaje akawa na vitambara viwili alivyoshona kanzu,ilihali Waislam amewapa kitambaa kimoja kimoja

Kefu hawa vibaraka waovu wenye kudhihirisha uchafu na ufusqa wazi bila hofu!

Enyi Waislam wapendwa!

2.Si halali kumtwii kiongozi katika maasi. Mtume (saw) alisema:

“Hapana utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

(Ahmad, Bukhari)

Hivyo,ikiwa mtawala anadhihirisha uchafu,dhulma,au anaendesha hukmu kinyume na Shari’ah ya Kiislamu,kama walivyo watawala bandia ambao ni vibaraka  wa makafiri wakoloni wamagharibi,ktk biladi za Kiislam zote,haifai kuwatwii katika hilo,wala kumkalia kimya.

Kwa muktadha huu,ndipo Ar Rasul Saw alipotufundisha misimamo na hatua ya kutwaa atakapo kutokea viongozi waovu:

“Watakuwa baada yangu viongozi mtaona kwao mambo mnayoyakataa… Mtu anayeona uchafu (munkar) basi si lazima amtii.”

(Sahih Muslim )

Kwa hivyo, si kosa kusema “Fala sam’a wala ṭa’ah” kwa watawala wanaoasi waziwazi, kwani utwiifu wao sio wa lazima wala wa kiwajibu katika maasi au utawala usio wa Kiislamu.

Katika Dini ya Kiislamu, hatutakiwi kuwasikiliza au kuwatii watawala wanaodharau Uislamu, wanaoendesha hukmu kwa kanuni za kikafiri, au wanaodhihirisha maovu.

Wajibu ni kuamrisha mema na kukataza maovu,na kutofanya hivyo ni kuvunja  na kupoteza majukumu ya Dini.

Enyi Waislam wapendwa!

Amana hii ya uongozi, madaraka na utwala,itatimia na kukaa mahali kufikishwa mahali pake salama penye kustahiki,pale tutakapo,kuwang’oa vibaraka waovu ktk biladi zetu,wenye kuikhini amaa hii,na kumkabidhi amana hii,Khalifah Rashid anaestahili pekee kusimamia amana hii.

Enyi Waislam wapendwa!

Tusimameni pamoja na harakati ya kiulimwengu: Hizb-ut-Tahrir,ktk kutimiza miadi ya Allah Swt Alipotwambia:

*وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ*

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini  miongoni mwenu na wakatenda mema kuwa atawafanya kuwa makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya walio kabla yao, na atawaimarishia Dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia kutoka kwenye hofu yao hadi kuwa na amani. Wataniabudu bila kunishirikisha na chochote.Na atakayekufuru baada ya hayo, basi hao ndio waasi.”

(Surat An-Nur, 24:55)

Na kufanikisha bishara njema ya Ar Rasul Saw alipotwambia:

 

حديث أبي هريرة قال: قال رسول الله ﷺ: كانت بنو إسرائيل تسوسهم الأنبياء،كلما هلك نبي خلفه نبي، وإنه لا نبي بعدي، وسيكون خلفاء فيكثرون قالوا: يا رسول الله، فما تأمرنا؟ قال: أوفوا ببيعة الأول فالأول، أعطوهم حقهم، واسألوا الله الذي لكم، فإن الله سائلهم عما استرعاهم  (متفق عليه)

 

Hadith ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) alisema: Mtume wa Allah (ﷺ) alisema:

“Wana wa Israil walikuwa wakiongozwa na manabii; kila mara nabii alipofariki, alifuatiwa na nabii mwingine.Lakini hakika hapana nabii baada yangu, bali kutakuwepo makhalifa wengi.”

Wakasema: “Ewe Mtume wa Allah, unaamuru tufanye nini?”

Akasema: “Timizeni utiifu kwa yule wa kwanza mliyempa bay’ah (kiapo cha uchaguzi na utwiifu), wapeni haki yao, na muombe kwa Allah haki yenu, kwani hakika Allah atawauliza kuhusu uongozi aliowapa.”*

(Bukhari na Muslim)

Enyi Waislam wapendwa!

Nakariri tena mara nyingine,kwa saabu,ulumbusho huwanufaisha Waumini.

Ili tuzingatie na kutekeleza,basi lazima tujue marekebisho ya kweli ya haki ni kupitia kusimamisha Khilafah Rashidah:

Wala si kuwafuata watawala waovu kwa kisingizio cha “umoja” au “kuepuka machafuko.”

Suluhisho la kweli ni kung’oa mzizi mzima wa mfumo wa kisekula na kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Ar Rasul Saw kupitia mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa.

Ewe Muislam mpendwa!

Jee wewe uko wapi?

Ni mmoja wa wale wanaojitolea kihali na mali kufanikisha Ahdi ya ALlah Swt na kutimiza bishara njema ya Ar Rasul Saw?

Au wewe ni shabiki tu,ukiwaangalia nduguzo wakisomba khairati?

 

Imeandikwa na Hussein Muhammad

Mwanachama wa Hizb-ut-Tahrir Kenya.