Na Wakikutana na nyinyi wanakuwa maadui zenu; na wanakukunjulieni mikono yao (kukudhuruni) na ndimi zao kwa uovu.
Habari:
Katika hatua za kuzuia msambao wa maradhi ya Covid 19, jeshi la polisi huko Afrika Kusini siku ya Jumamosi tarehe 26 Aprili, ilivamia chumba ambacho ndani yake kulikuwa na Waislamu 20 wakiswali na kuwaamuru kulala chini. Picha za video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na wakuu serakalini nchini humo, huku zilionesha udhalilishaji huo dhidi ya Waislamu huku ofisaa mmoja wa polisi akisikika kuwatukana Waislamu “Je nyinyi ni wakubwa zaidi kuliko raisi? Je Muhammad ni mkubwa kuliko raisi?” Kulingana na Aljazeera, ni kuwa mkuu wa polisi nchini humo Bheki Cele aliomba radhi kwa matamshi hayo ya kukufuru ya ofisaa huyo wa polisi dhidi ya waislamu hao waliokuwa wakiswali. Cele alisema ‘ uchunguzi wa haraka’ umeanzishwa “kumtambua polisi alifanya kisa hicho”
Maoni:
Ni wazi kwamba mataifa yote ulimwenguni yameshindwa kudhibiti maambukizi ya janga la Covid 19. Kama jaribio la kuficha fedheha hiyo, sasa yameamua kutoa makucha yake kwa kuamuru vikosi vyake vya usalama kutekeleza vitendo vya kikatili dhidi ya raia chini ya madai ya mikakati ya kuzuia msambao wa Corona’. Ukatili huo ulioshuhudiwa Afrika Kusini pia umeshuhudiwa nchini Kenya mwanzoni mwa utekelezwaji wa marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja. Shirika la Human Watch linasema askari Kenya walihusika kuwauwa wakenya takriban sita kwenye mchakato wa kutekeleza agizo hilo la serikali ambalo kwa sasa linaingia mwezi wa pili. Taswira inayojitokeza ni kuwa ndani ya serikali za Kirasilimali,vikosi vya usalama viko tu kulinda watawala na wala sio raia.Aidha ni wazi kuwa ukatili na mateso ndio zana pekee ya serikali kibepari.
Kitendo cha kuwadhalilisha Waumini pamoja na kutukaniwa Mtume wao kunakuja sambamba na amri ya kuifunga majumba ya- MwenyeziMungu ambazo ndani yake hutajwa jina Lake. Haya yote yanaabiri pupa kubwa ya warasilimali na mawakala wao ya kudhuru Waislamu. Amesema MwenyeziMungu SWT:
إِنْ يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُمْ بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ
Wakikutana na nyinyi wanakuwa maadui zenu; na wanakukunjulieni mikono yao (kukudhuruni) na ndimi zao kwa uovu.Na wanapenda muwe makafiri
Cha kusikitisha ni kwamba pamoja na uadui huu wa wazi dhidi Uislamu na Waislamu, bado kuna Waislamu hadi sasa hulingania siasa ya Kidemokrasia na kuwafanya wasiri wanasiasa na watawala ambao kupitia Demokrasia na mwito wake wa uhuru wa maoni wanavunja heshima za Waislamu na kutukuna matukufu yao ya kiislamu..
Asema MwenyeziMungu Swt:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِنْ دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ
Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika nyinyi: hao hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yale yanayokudhuruni. Bughudha (yao juu yenu) inadhihirika katika midomo yao. Na yanayofichwa na vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekubainishieni dalili (zote) ikiwa nyinyi ni watu wa kufahamu.
Hatua ya kuomba radhi Waislamu na kuwa eti uchunguzi wa haraka unafanywa, hii ni kuonyesha daraja kubwa ya kejeli za viongozi wa kisecular ambao baada kumkanusha MwenyeziMungu na sheria zake huwafanyia istihizai waja wa MwenyeziMungu wanaojifunga na sheria Zake. Je kweli yaingia akilini serikali hiyohiyo ilioamuru kuwadhalilisha Waislamu imtie mbaroni mtu alietekeleza agizo hilo? Uchunguzi upi wa kufanywa ikiwa kikosi hicho kinajulikana na serikali? Yatosha kuwa ni matusi makubwa kule kumlinganisha Mtume SAAW na viongozi waovu wa kirasilimali wanaolaaniwa na raia wao nao wanawalaani.
Kwa hakika kitendo cha uovu cha kuwavamia Waislamu wa Afrika kusini hakitovunja kattu ari ya Waislamu kushikamana na Dini yao kote duniani. Kitendo hiki kimetanguliwa kabla na vitendo vyengine vya kikatili dhidi ya umma wa Kiislamu ikiwemo kukaliwa ardhi yao tukufu ya Filastin, kumwagwa damu za Waislamu huko mashariki ya kati, kunajisiwa kwa Quran na mengine mengi. Yote haya, ni kukosa Waislamu ngao yao –Khalifah ambaye mmoja katika jukumu lake ni kuhami matukufu ya Uislamu. Khalifah ambaye humuadhibu adhabu ya kifo kila anayethubutu kutusi bwana Mtume SAAW. Kwa haya basi Waislamu wakiwa katika kipindi muhimu cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wafanye bidii kuisimamisha tena Khilafah serikali pekee itakayoweza kuhami heshima na matukufu yote yaKiislamu.
Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya