Sera Fisidifu za Kiuchumi za Kirasilimali Zinaendelea Kuwaumiza Zaidi Wakenya

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watu wa Kenya wanalipa ushuru wa VAT wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta katika hatua iliyokiuka kura ya bunge ya kuakhirisha ushuru huo kwa miaka miwili. Utekelezaji wa ushuru wa VAT kwa asilimia 16 juu ya mafuta uliomo ndani ya Mswada wa Fedha wa 2018, unaanza kutekelezwa baada ya kumalizika muda wa kusubiri wa miaka mitano ulioanza mnamo 2013. Kupandishwa kwa ushuru huo inadaiwa kupangwa ili kufadhili malengo kadhaa ya kimaendeleo ya serikali ikiwemo matibabu kwa wote na makao nafuu.

Sisi Hizb ut Tahrir / Kenya tungependa kufafanua yafuatayo:

Ushuru huu mpya pasi na shaka ni pendekezo kutoka kwa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IMF) ambayo imekuwa ikitia shinikizo kwa Kenya kuondoa misamaha ya kiushuru kama sehemu ya mpango mpana wa kukuza mapato, kupunguza mapungufu katika bajeti na hatimaye kupunguza mrundiko wa deni.

Ukweli ni kuwa dola za kigeni za kikoloni pamoja na taasisi zao za kifedha ndizo zinazoendesha uchumi wa Kenya nyuma ya pazia huku machoni kukiwa na vikaragosi wanaobeba lawama kwa niaba yao. Hivyo basi, kupitia mkusanyiko wa sera zote za kirasilimali, wakoloni wa Kimagharibi pamoja na ushirikiano wa wazi wa serikali zinawatumbukiza raia katika mateso zaidi ya kiuchumi. Wakenya daima wamekuwa waking’ang’ana kujimudu lakini sasa idadi kubwa zaidi wamejipata wakiwa na changamoto ya kununua hata bidhaa msingi kama ugali na mchele.

Mvutano kati ya baraza la mawaziri na bunge unaonyesha migongano na dosari za nidhamu ya kidemokrasia. Zaidi ya hayo, urasilimali unajitia katika mzozo wa kimaslahi kupitia kuweka bei huku wakati huo huo ukilingania sera za soko huru zinazojumuisha maamuzi ya bei yawe kwa mujibu wa kupanda na kushuka kwa miondoko ya usambazaji na matakwa ya bidhaa.

Imedhihirika wazi wazi kuwa serikali haijali kuhusu maslahi ya raia ambao inadai kuwaongoza. Badala yake, inacho maanisha katika uboreshaji maisha ya watu wake ni kuongeza bei, kuwawekea ugumu juu yao na kupanua viwango vya ufukara. Kuchukua mikopo mingi mno huku kodi za raia zikiwa kama dhamana ili kufadhili miradi ‘hewa’ halafu fedha hizo zinaishia kuporwa na serikali hiyo hiyo. Mnamo 2008 wakati ambapo serikali ya muungano wa kitaifa ilipoundwa kupitia shinikizo kutoka nje, maisha yalikuwa magumu sana. Leo miaka 10 baadaye tuna ule unaoitwa ‘mchakato wa Kujenga Maelewano’ uliojengwa juu ya mtazamo ule ule lakini kwa muundo tofauti, ambao utasababisha ugumu zaidi juu ya maisha ya raia wengi ambao tayari wanateseka na lindi la umasikini.

Hatimaye tunasema suluhisho msingi la hili haliko katika maandamano, badala yake, ni kupigania nidhamu inayowatizama na kuwajali watu wake kwa ukarimu. Nidhamu inayomridhisha Mwenyezi Mungu na inayohukumu watu kwa haki ya kupitia hukmu za Uislamu. Nidhamu ambayo watu wake wakilala njaa basi viongozi wao wamewatangulia katika njaa hiyo; na watu wake wakiwa na shibe basi viongozi wao wanashiba baada yao. Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Mtume (saw) itadhamini kiukweli maisha ya raia na haitowatoza ushuru isipokuwa kukitokea dharura ambayo iko nje ya uwezo wa Khilafah. Zaidi ya hayo, watakaotozwa ushuru ni matajiri walio na mali ya ziada.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 15/ 1439 AH

Jumanne, 24 Dhul Hijjah 1439 H /

04/09/2018 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke