Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Mnamo tarehe 18 Februari.2025, kikosi cha Rapid Support cha Sudan kilifanya mkutano katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta jijini Nairobi kuzungumza uundaji wa serikali ya umoja ya majimbo yanayodhibitiwa na kikosi hicho nchini Sudan. Utawala nchini Kenya unashikilia kudai kwamba kujihusisha kwake kwenye mazungumzo hayo ni kuimarisha “juhudi za amani nchini Sudan”. Nairobi imetetea uamuzi wake wa kuwa mwenyejji wa kufanya mazungumzo na kikosi cha kipiganaji yanayolenga kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa. Maofisaa wa Kiutawala wa Sudna wameiona hatua hii kama jaribio la kuanzisha utawala mwengine sambamba na ule wa Khartuom, hatua hii ya Kenya imepelekea kulaumiwa kwake kwa kukiuka mamlaka ya Sudan na kujihusiha kwa matendo ya kiuhasama.
Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kuangazia yafuatwayo:
Huku ikiwa maudhui ya mkataba huo wa Kisiasa haujatolewa kwa umma, lakini kinachotarajiwa ni kueleza mfumo wa kiutawala wa RSF,malengo yake ya kisiasa na mikakati yake ya kuunganisha udhibiti wake kwa majimbo yake. Mkataba huo unalenga kuja na muundo wa kiutawala kwenye maeneo ambayo RSF inayadhibiti. Kiuhakika ni jambo la kuhuzinisha kuiona Nairobi kwa kisingizio cha kutafuta suluhu ya mizozo,inaendelea kucheza dori ya kiuwakala ya kuendeleza mizozo inayopelekea kupotea maisha ya wanadamu!
Uhalisia wa hali ya sasa ya kisiasa nchini Sudan na nchi zingine zinazoendelea kama vile Somalia na DRC ziko hatarini kwa nguvu za nje ambazo, kwa kufuata masilahi ya mataifa makubwa ya Magharibi (Marekani na Uingereza). Inasikitisha leo kushuhudia nchi za Kiafrika na taasisi zake zote kama vile AU na IGAD zikishiriki katika kuunga mkono maslahi na ushawishi wa wakoloni wa Magharibi. Tangu mzozo huo ulipozuka miaka miwili iliyopita, tamko lote la mapatano, kuanza tena kwa mapigano, mazungumzo na mawasiliano ni kati ya pande mbili zilizo na uhusiano na Amerika: uongozi wa Jeshi na uongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka.
Nia ya Marekani ni kupunguza mzozo kati ya mawakala wake na kudhibiti matokeo kwa kugawanya majukumu kati yao.Hatua yake ni kusambaratisha vikosi pinzani vinavyoegemea upande wa Uingereza na Ulaya ambavyo tangu michafuko ianze vimekuwa vimelemazwa. Kwa hakika, mawakala wa Uingereza katika ni kikosi cha Freedom and Change na vyengine.
Mizozo na ‘miito ya kutafuta amani’ kote barani Afrika inachangiwa pakubwa na mvutano wa kiubabe wa Kikoloni. Sudan imekua ni jeraha jengine baya la umma wa Kiislamu baada ya kuushuhudiwa miongo mitatu ya Waislamu kupigana wao kwa wao nchini Somalia.
Tunahitimisha kwamba kwa vile migogoro yote barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla inapangwa na mataifa yenye uchu wa kikoloni na washirika wao, suluhu za kikweli kamwe haitoafikiwa na mfumo wa Kibepari unaendeleza ukoloni. Kwa hiyo, Afrika inahitaji mfumo mpya wa dunia yaani Uislamu ili kumkomboa kutoka kwa mnyororo wa kikoloni unaoliona bara tajiri la Afrika kama chanzo cha malighafi na soko la bidhaa zao. Uislamu unamkomboa Mwanaadamu kutoka kuwa mtumwa wa mtu mwingine badala yake kumfanya mja wa Muumba wake MwenyeziMungu (swt) Kwa maana haya, mfumo wake wa utawala (Al-Khilafah/Khalifa) utafanya kazi kuelekea kuukomboa walimwengu wote katika nyanja zote za maisha. Hapo ndipo Afrika itakapokombolewa na kuishi kwa heshima na mafanikio.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Kenya