Tanzia ya Mbebaji Daawa nchini Kenya

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

”Hakika Sisi Ni Wa MwenyeziMungu Na Hakiki Sisi Kwake Yeye ni Wenye Kurejea” 

Kwa imani thabiti na kujisalimisha kikamilifu kwa Qadhaa ya Allah (swt), Hizb ut Tahrir/Kenya
inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla, na haswa watu wa Kenya;

Seif Omari Mwaruwa

(MwenyeziMungu Amrehemu) aliefariki dunia siku ya Ijumaa Juni 28, 2024. 

Licha ya kuwa mzee, mzee Seif alijiunga na Hizb ut Tahrir – harakati ya Kiislamu ya kiulimwengu ya Kimfumo
inayobeba wito adhimu wa kufufua maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume
(saw). Pamoja na hali yake ya maradhi mzee alikuwa bado anatimiza ahadi yake na kutangamana na watu wa
umri wake juu ya suala muhimu la Khilafah na wala hatumsifii yoyote mbele ya MwenyeziMungu (swt). Hakika nyoyo zetu zinahuzunika, macho yetu yanatokwa na machozi kwa msiba huu mkubwa wa baba na
ndugu yetu.Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu na umsamehe. Ewe Mwenyezi Mungu, kirimu mashukio yake
yafanyie ukunjue makaazi yake. Mwisho tungependa kutuma rambirambi zetu za dhati kwa familia yake huku tukimuomba
MwenyeziMungu swt awalipe ujira awape subra, ujasiri na faraja.Twamuomba MwenyeziMungu aidha, ambadilishie nyumba yake kwa makaazi bora, na familia yake kwa familia bora zaidi na akatukutanishe pamoja naye chini ya bendera ya Mtume SAAW siku ya Qiyamah.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya