Taarifa kwa Vyombo Vya habari
Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kutuma salamu za dhati za siku kuu ya Iddul- Adh-ha kwa Waislamu wa humu nchini na ulimwengu kwa ujumla. Idd hii inawadia wakati ambapo raia wa kawaida wanakumbana na hali ngumu ya kiuchumi kwa kutokamana na kupanda maradufu kwa bidhaa msingi. Kwa sasa Kenya inashikilia nafasi ya nane duniani na ya sita barani kama taifa lenye watu wengi wanaoishi kwenye lindi la umasikini. Nao msururu wa kashfa za ufujaji wa fedha, unyakuzi wa ardhi na ufisadi umekuwa ni jambo la kawaida ambapo wanasiasa wakitupiana lawama ilhali kashfa hizi ni ukumbusho kwamba serikali za Kibepari kattu hazijali maslahi ya raia wake na pia ni kawaida kukumbwa na kashfa.
Huku tukisherehekea Idd na familia zetu kama jamii ya Kiislamu, tusisahau kuwaombea ndugu zetu katika mataifa ya Syria na Yemen wanaoshambuliwa na mabomu ya majeshi ya mataifa makubwa ya Kimagharibi na mawakala wao. La kusikitisha mauaji haya ya halaiki yafanywa peupe na Marekani na Urusi na vibaraka wao hayajachangamsha damu na mioyo ya majeshi ya Kiislamu yaliyopo katika nchi za Kiislamu!
Tunafahamu kwa yakini kuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu ushindi uko karibu mno. Tuna imani kubwa tutafaulu katika kazi ya kulingania Uislamu kama suluhisho mbadala la kimfumo juu ya mfumo uliofeli wa Kibepari na kuwa kazi hiyo italeta mafanikio makubwa. Ukweli huu ni wenye kufahamika vyema na wamagharibi na vibaraka wao katika mataifa ya Kiislamu kama vile Pakistan ambayo inatumia mbinu za kuwateka nyara wanawake wa kweli waumini Waislamu kama kina dada Romana Hussain, Dkt.Roshan na wengineo wengi kwa ajili tu ya kulingania kwao Uislamu! Imani yetu ni kwamba Uislamu ndani ya serikali yake Khilafah itakayosimama hivi karibuni itasitisha na kumaliza unyanyasaji wote unaofanyiwa Waislamu pembe zote za dunia.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubaliye matendo yetu mema, atuongoze kwa kutufikisha katika Idd ya mwakani tukiwa nchini ya Khilafah Rashidah kwa njia ya bwana Mtume Muhammad (saw). Serikali ambayo itaunganisha Waislamu wote duniani chini ya bendera ya ‘Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah.’
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya
KUMB: 12 / 1439 H
Jumatatu, 09 Dhul- Hijja 1439 H/
20/08/2018 M
Simu: +254 707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke