Uamuzi wa Mahkama juu ya LGBT ni uthibitisho wa Itikadi ya Kisekular (Utenganishaji wa Dini na Maisha) na siasa ya Kidemokrasia
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Mahakama ya upeo nchini Kenya imeamua kuwa jumuiya ya Wasagaji, Mashoga, Wapenda jinsia mbili, Wanaobadili jinsia (LGBTQ) wana haki ya kujumuika. Uamuzi huo sasa unamaanisha hatua ya kukataa kwa Bodi ya Uratibu ya mashirika yasokua ya kiserikali (NGOs) kusajili kikundi hiki ni ukiukaji wa haki za binadamu zinazolinda watu wenye msimamo huu wa kingono. Katika uamuzi uliotofautiana, mahakama kuu, ilisema kuwa sheria ya nchi – Kifungu cha 162 cha Kanuni ya Adhabu – inayokataza "makosa yasiyo ya asili" (yaliyofafanuliwa kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanamume, mwanamke au mnyama yeyote kinyume na utaratibu wa kimaumbile ) ni yenye kufuata.
Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kutaja yafuatayo:
Kwa kuwa Kenya ni taifa la kisekula,sio jambo la kushangaza hata kidogo kwa Mahakama kuja na maamuzi haya, hii ni kwa sababu itikadi ya kisekula huamini fikra ya kutenganisha Dini na Maisha hivyo kumpa mwanadamu uhuru wa kujitungia kanuni zinazotokamana na mawazo na mataminio ya nafsi. Kwa mantiki hii suala la kutukuza matamanio ya kimwili hutangulizwa mbele huku maadili mema yakidharauliwa,hii ni kwa kuwa vipimo maishani havisimami juu ya halali ama haramu bali ni kwa msingi wa kufikia upeo mkubwa wa kujistarehesha kimwili.
Kupigia debe na kulindwa kwa "jamii" ya LGBTQ+ ni sehemu tu ya kampeni pana inayoendeshwa na mataifa makubwa ya Magharibi ambayo tayari yamehalalisha ushoga na inaonekana kuwa yamejumuishwa katika malengo yao ya sera zao za kigeni. Hii inajidhihirisha katika dhima ya kulinda haki za LGBTIQ+ na usaidizi wa kifedha kwa nchi za ulimwengu wa tatu. Mbali na haya, uhakikisho wa kisheria na propaganda unafanywa katika tabaka zote za jamii ili kuhalalisha LGBTQ+ miongoni mwa jamii ya Kenya. Uamuzi huu unakuja miezi miwili tu baada ya mauaji ya mwanaharakati wa LGBTQ+ yaliyoibua hisia kali kwenye safu ya wanasiasa wa humu nchini na wenzao katika mataifa ya Kimagharibi ambao walichukua hatua kubwa za kuwasaka wauaji chini ya bendera ya kutetea " haki za watu wa ngono." Kinachoshangaza maisha ya Wakenya wengi yanapotea kila siku na wala hilo haliwatii wasiwasi wowote maofisaa wa vyombo vya usalama vya serikali wala mabepari wa kimagharibi!
Huku ulimwengu ukishuhudia mmomonyoko huu wa kimaadili unaopaliliwa na utamaduni wa kimagharibi, hili liwe dalili tosha kwa wote wenye akili kuona kwamba machafu zaidi yataruhusiwa kikanuni katika siku za usoni. Twasema wakati umefika wa kutupilia mbali itikadi ya kimagharibi pamoja na maovu yake yote. Walimwengu lazima waelekee kwenye mfumo wa (Uislamu) ambao umemtukuza na kunyanyua heshima ya mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi, kulinda familia, kukuza maadili na kudhamini mafanikio makubwa sio hapa duniani tu bali kesho Akhera.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir
Kenya