Uchomaji wa Nguvu wa Maiti za Waathiriwa wa Kiislamu wa Covid-19 Nchini Sri Lanka Chini ya Utawala Ulio na Chuki na Waislamu Ambao Unalitumia Janga Hili la Maambukizi Kuzidisha Ajenda Yake Dhidi ya Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Manmo Jumanne tarehe 1 Disemba, Mahakama ya Upeo ya Sri Lanka ilikataa ombi la mashirika ya kiraia na kesi za kimahakama zilizoletwa na familia za Waislamu na Wakristo nchini, wakipinga sera ya serikali inayoamuru kuteketezwa kwa vifo vyote vinavyohusiana na Covid-19 au maiti yoyote inayoshukiwa kuambukizwa na virusi hivi, bila kujali imani za kidini. Serikali ya Mabudha wenye nia ya pamoja ya kitaifa ya Sri Lanka ilipuuza miongozo kutoka kwa wataalam mashuhuri wa matibabu na wanasayansi pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni ambao walisema kuwa wahasiriwa wa Covid wanaweza kuzikwa salama bila hatari yoyote kwa afya ya umma. Badala yake, ilijaribu kutumia janga hilo kuendeleza ajenda yake dhidi ya Waislamu, dhidi ya Uislamu kwa kutoa kanuni mnamo Aprili ikisema kwamba “wahasiriwa wote wa COVID-19 watachomwa ndani ya masaa 24 ya kifo”, wakijua fika kuwa hatua hii inakiuka imani za kimsingi za Waislamu kwani Uislamu huliona hili kama ukiukaji wa utukufu wa mwili wa marehemu. Tangu kutolewa kwa sera hiyo, zaidi ya Waislamu 50 wamechomwa. Kwa kweli, ripoti zimeibuka kuwa Waislamu kadhaa ambao miili yao ilichomwa na mamlaka hawakuwa wamepimwa Covid wala hata kutokuwa na virusi hivyo. Mtu mmoja Muislamu ambaye aligundua kuwa mamake alikuwa amechomwa kimakosa alisema: “Siku ambayo mamangu alikufa hospitalini, walichukua mwili wake na kisha wakanipa sufuria ya majivu yake. Lakini siku iliyofuata waliniambia kuwa vipimo vya mamangu vilikuwa hasi na ilikuwa kosa kumteketeza. Kila usiku ninaamka na kufikiria hatima ya mama. Sisi ni masikini na hatuna uwezo wa kudai haki wala kupigana na mamlaka. (imenukuliwa katika gazeti la Guardian la Uingereza). Mamlaka za Sri Lanka hata zinawaomba Waislamu walipe ada ya 48,000 (£192) inayodaiwa na serikali kulipia gharama ya kuteketeza mwili. Kwa kuwa familia nyingi za Kiislamu zinakataa kufanya hivyo kwa kuhofia kwamba watahusika katika unajisi wa wapendwa wao. Waathiriwa wa Kiislamu wa Covid-19 wameanza kurundikana katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya hospitali. Waislamu kwa hivyo wanalazimishwa kuachana na maiti zao.

Maoni:

Waislamu nchini Sri Lanka hawaishi tu kwa hofu ya kuambukizwa na virusi vya Korona, lakini pia kwa hofu ya virusi vya chuki dhidi ya Waislamu vinaenezwa katika jamii na serikali ya kijamii ya kitaifa, inayoungwa mkono na wafadhili wao wa Kibudha wenye msimamo mkali. Familia za Kiislamu, huku zikiomboleza wafu wao, pia zinateseka uchungu wa ziada wa kunyimwa haki ya kutekeleza ibada za mwisho za kidini za wapendwa wao za kuzika kwa amani. Waislamu wengi hata wanaogopa kutafuta matibabu hospitalini kwa hali zingine mbaya, wanaogofya na fikra ya kuwa lau watakufa wakiwa hospitalini kwani mamlaka itachukua miili yao kwa ajili ya kuichoma hata bila kuipima virusi.

Sera hii ya kuteketeza miili isiyo na msingi imetekelezwa bila chochote isipokuwa chuki dhidi ya Waislamu ya serikali hii. Mwandishi mmoja wa Sri Lanka aliiweka ipasavyo kwa maneno yafuatayo: “Serikali inatoka nje ya mipaka yake ili kuumiza hisia msingi kabisa za jamii ya Waislamu”. Lakini, hii haishangazi. Uadui dhidi ya idadi ya Waislamu nchini Sri Lanka umekuwa ukiongezeka kwa miaka mingi, ukisimamishwa kwa kimsingi na vikundi vya kitaifa vya Mabudha walio na chuki na Waislamu, kama vile Bodu Bala Sena (BBS) na watawa wachochezi wa Kibudha ambao wanapata msukumo kutoka kwa wenzao nchini Myanmar. Wanaruhusiwa kufanya kazi kwa uhuru na wanaeneza hadithi ya kipuuzi ya uchochezi kwamba Mabudha wa Sinhala katika nchi hii yenye Mabudha wengi wako chini ya tishio la idadi kubwa ya Waislamu (inayojumuisha chini ya asilimia 10 ya idadi ya watu). Katika miaka ya hivi karibuni, maneno kama haya yenye sumu dhidi ya Waislamu na Uislamu yamekuwa ya kawaida, yameonyeshwa wazi na wanasiasa, waandishi wa habari na kwenye mitandao ya kijamii. Jamii ya Waislamu imekuwa ikikabiliana na hofu ya kinidhamu ya Uislamu kwa miaka mingi, na imeishi chini ya wingu la kushukiwa na unyanyasaji, haswa kufuatia mashambulizi la bomu ya Pasaka ya 2019, inayokabiliwa na vurugu na uchafuzi wa majina. Wanawake wa Kiislamu waliovaa hijab wamekuwa wakiteswa na kuambiwa wavue kitambaa chao wakati wa kuingia kwenye maduka au majengo anuwai, au wakati wanaongozana na binti zao kwenye mahojiano ya kuingia shuleni; marufuku ya niqab ilitekelezwa; kulikuwa na kampeni dhidi ya uandikishaji ‘Halal’ wa chakula; Waislamu wamekabiliwa na kukamatwa kiholela na upekuzi wa polisi katika nyumba zao wa nyenzo za Kiislamu; uongo wa moja kwa moja umeenezwa juu ya Waislamu na Dini; na kumekuwa na mashambulizi mengi ya umati kwenye misikiti na nyumba za Waislamu na biashara. Kwa kweli, chama kinachotawala cha kitaifa, kinachoongozwa na ndugu wa Rajapaksa, ambao wana uhusiano wa karibu na BBS, walichaguliwa kwa ushindi mkubwa, juu ya wimbi la maoni ya Mabudha wenye msimamo mkali wenye chuki na Waislamu. Waislamu wengi nchini sasa wanaogopa kwamba wanaweza kukumbana na hatma sawa na ndugu na dada zao Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar.

Ukweli huu unaoumiza moyo unaowakabili Waislamu nchini Sri Lanka ni ukumbusho mkali wa jinsi gani mfumo wa utawala wa kisekula uliotungwa na mwanadamu ulivyo hatari na usivyo tabirika, ambapo haki za kidini na zingine za watu, haswa wachache, zinaweza kubadilika kama upepo kulingana na mapendeleo na chuki za wale wanaotawala, na ambapo wale wanaodhulumiwa wameachwa bila nguvu chini ya mfumo wa kupindua dhulma dhidi yao. Kwa hivyo inapaswa pia kuwa ukumbusho wenye nguvu kwa Waislamu kwamba hawapaswi kamwe kuweka tumaini na uaminifu wao kwa mfumo wowote sheria wa kidemokrasia uliotungwa na wanadamu ili kupata maslahi na haki zao. Mtume (saw) amesema,

«لا يلدغ المؤمن من جحر واحد مرتين»

“Muumini hang’atwi kutoka tundu moja mara mbili.” Fauka ya hayo, inapaswa kuwa wazi kama usiku na mchana kuwa hakuna serikali ya kidemokrasia au serikali nyingine yoyote, mtawala, dola au chombo cha kimataifa leo – katika ulimwengu wa Kiislamu au usio wa Kiislamu – ambaye ana nia ya dhati ya kisiasa kuwasaidia Waislamu wa Sri Lanka, au kwa hakika Waislamu wanaodhulumiwa popote duniani leo.

Kwa hivyo tunawalingania Waislamu wa Sri Lanka kugeuza umakinifu wao na juhudi zao kwa suluhisho la kweli la shida yao, ambalo ni kusimamisha tena kwa haraka Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt): Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo ndio dola pekee ambayo itasimama kama mlinzi wa kweli juu ya ustawi wao na Dini, ikitumia zana zote za kisiasa, kiuchumi na hata za kijeshi katika hazina yake ya silaha kulinda haki zao kama ilivyo fanya kwa Waislamu zamani, kwani Mtume (saw) asema:

 «الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Imam (Khalifah) ni mchungaji, na ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake.” Kwa hakika, pasi na dola hii, Waislamu hawawezi hata kufa kwa heshima.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir