Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Mnamo siku ya Alhamisi tarehe 4 Oktoba 2018, harakati ya Kiislamu ya Hizb ut Tahri /Kenya ilifanya ziara maalumu ya kumfariji Professa Mohamed Manyora (zamani Hermon Manyora). Profesa Manyora alilazwa katika hospitali ya Mater jijini Nairobi anakoendelea kupata matibabu kufuatia ajali ya gari iliyompelekea kupata jeraha kichwani.
Ziara hiyo iliongozwa na Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano wa Hizb ut Tahrir /Kenya Arkanuddinn Yassin, akifuatana na Shabani Mwalimu -Mwakilishi kwa Vyombo ya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya na Yusuf Ghasana -Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Kenya.
Prof. Manyora ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi pia ni mdadisi maarufu wa kisiasa kwenye runinga za Kenya. Siku chache tu kabla kupata ajali Prof. Manyora alikuwa ameingia katika nuru ya Uislamu -Alhamdulillah. Kwa hakika hatua yake hiyo ni ya kupongezwa sana kwani imedhihirisha usafi wa fikra za mfumo wa Uislamu licha ya kampeni kubwa ya wamagharibi ya kuupaka matope na kukejeli sheria zake. Ni wazi kwamba licha ya njama za wamagharibi dhidi ya Uislamu lakini bado kuna mabongo kama ya Prof. Manyora yanayochanganua baina ya ukweli na urongo haki na batili na hatimaye kuifuata haki.
Ujumbe wa Hizb umehitimisha ziara hiyo kwa kumpa zawadi ya vitabu kadhaa vya Kiislamu vikiwemo vya harakati ya Hizb ut Tahrir. Pia ikamuombea Mwenyezi Mungu ampe shifaa ya haraka Ndugu Manyora ili aweze kuendelea na shughuli zake za kimaisha na apate fursa ya kuusoma Uislamu ili apate kudumu kwenye uongofu nayo ndio njia bora ya kuifuata.
فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا
Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu. [Al-Jinn: 14]
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya
KUMB: 1440 / 01
Ijumaa 25, Muharram 1440H /
05/10/2018M
Simu: +254 707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke