Utawala wa Marekani: Sura Mpya lakini zenye Njama Zilezile

Habari:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika Antony Blinken ataizuru Kenya, Nigeria na Senegal kuanzia Novemba
15-20, akisisitiza umuhimu wa mahusiano yao na washirika wa barani Afrika. (The Star, 12/11/2021).

Maoni:
Kwa mara nyingine tena utawala wa Marekani umemtuma mwanadiplomasia wake mkuu barani Afrika
kibinafsi baada ya kuzuru Kenya na Nigeria kimtandao mnamo Aprili 2021. Hata hivyo, mara hii Senegal
imejumuishwa katika ziara. Ni muhimu kuweza kuzishughulisha akili zetu kwa kujiuliza maswali yafuatayo: 1 –nini
kilichonyuma ya ziara hii? 2 – kwa nini kuyazuru mataifa hayo matatu maalumu? 3 – nani anatarajiwa kunufaika
zaidi katika ziara hii? 4 – mataifa hayo matatu na Amerika ni washirika katika nini? Maswali hayo manne yatajibika
kimakosa lau tutazizingatia taarifa zilizotumwa kwa ummah kupitia vyombo vikuu vya habari ambavyo hupokea
malipo ili kupigia debe propaganda za serikali.
Kwa hakika, ziara hii sio chochote bali ni kampeni ya kidiplomasia ya ukoloni mamboleo inayolenga
kukazanisha vitanzi katika shingo za watawala vibaraka barani Afrika, ili waendelee kujifunga na mchoro
unaoongozwa na mkaazi mpya wa Ikulu ya White House. Mchoro ambao unajumuisha kuyatia pingu mataifa ili
kushikamana na mungu aliyefeli wa demokrasia, nidhamu huria ya kijamii, nidhamu ya kiuchumi iliyojikita katika
riba na ukandamizaji miongoni mwa maovu mengine yanayo endelea kusababisha majanga yasiyohesabika kwa
wanadamu duniani kote. Kwa kuongezea, utawala wa Marekani unakwenda mbio kuzipiku hatua zilizopigwa na
utawala wa Uchina barani Afrika.
Mataifa hayo matatu yanacheza dori muhimu katika maeneo yao na barani Afrika kwa ujumla. Kenya ndio
kituo cha uchumi wa eneo la Afrika Mashariki na Kati ikiwa haina mshindani. Nigeria ndio yenye uchumi mkubwa
na idadi kubwa ya watu barani Afrika. Rais wa Senegal anatarajiwa kuingia katika cheo cha juu katika uongozi wa
Muungano wa Afrika (AU). Fauka ya hayo, mataifa hayo matatu yamebakia kuwa watiifu kwa mabwana zao
wakoloni ambao ni Uingereza na Ufaransa. Kwa hiyo, Amerika inatambua umuhimu wa mataifa haya na
imewekeza juhudi zake ili kuzitoa kutoka kwa washindani wenza wa kikoloni.
Utawala wa Marekani kwa kuwa ndio wenye usemi duniani inatarajiwa kunufaika zaidi kutokana na ziara hiyo.
Hata hivyo, mataifa watumwa yatanufaika kutokamana na makombo machache watakayopewa na bwana mkoloni.
Amerika itanufaika kupitia utekelezaji wa mikataba mingi itakayotiwa saini nyuma ya pazia na ambayo
itayafadhilisha makampuni ya Marekani pasina kuzingatia viwanda vya nchini. Na wakati huo yakitoa mwanya zaidi
kwa taasisi za kifedha za Marekani mfano Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuendelea kufanya
uharibifu kwa uchumi wa mataifa yaliyosalimu amri.
Amerika na mataifa hayo matatu ni washirika katika kusababisha ufisadi duniani. Kilele cha kiwango cha
ufisadi ni wao kuupiga vita Uislamu na Waislamu. Kwa pamoja wameubandikiza Uislamu kuwa ni itikadi kali na
Waislamu ni wenye misimamo mikali na magaidi. Hivyo basi, wameamua kuwakandamiza na kuwaua Waislamu
kupitia kutunga na kutekeleza sheria na sera dhidi ya ugaidi na misimamo mikali! Kwa pamoja wanaukashifu
Uislamu na kuuona kuwa ni wa kikatili na wa kizamani usioweza kutatua changamoto za karne hizi! Alas!
Changamoto zilezile ambazo zimetokamana na kutekeleza mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na mataifa
yayo hayo!
Kwa kutamatisha, ziara hii haileti matumaini wala ustawi kwa Afrika. Badala yake ni ziara nyingine inayotekelezwa
na sura mpya lakini zenye njama zilezile ambayo ni ziara ya kikoloni kuja kutathmini mashamba ya kikoloni
yanayomilikiwa na washindani wa Marekani. Lau kutapatikana fursa, basi wajaribu kuwavutia wasimamizi wa shamba la
kikoloni kwa vijipesa kwa jina la msaada wa kifedha miongoni mwa vivutio vingine ili kuuhamisha utiifu wao wa kikoloni.
Lau hakuna fursa, basi angalau kutafuta japo uungwaji mkono katika kutekeleza ajenda ya Amerika iliyo na sumu ndani
ya mataifa yao husika na ng’ambo. Sehemu ya ajenda ikijumuisha kupigana vita vya kiwakala vya Amerika.
Afrika itaendelea kutaabika chini ya mikono ya wakoloni Wamagharibi ambao wanatawala mataifa ya Afrika kupitia
watawala vibaraka wa kikoloni. Watawala waovu ambao wanaiba mali za watu binafsi na za ummah na kisha kuzituma
ng’ambo ilhali raia wamebakia wanateseka kwa umasikini wa kudumu. Kwa kuongezea, wanakula njama na yale
yanayojiita ni mashirika ya Magharibi ambayo hudai kuwasaidia raia; lakini yapo kwa ajili ya kulinda hali iliyoko na
kuwahadaa watu. Afrika imezama ndani ya dhiki. Kuchipuza kwa nidhamu mbadala ya uongozi ndio pekee itakayo
dhamini kuondoka shidani. Nidhamu mbadala inayochipuza kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ni Khilafah kwa njia
Utume. Khilafah italeta matumaini na ustawi wa kikweli sio tu kwa Afrika bali kwa dunia jumla. Itakuwa na uwezo wa
kuyafanya hayo kupitia utekelezaji wake wa nidhamu tofauti za Kiislamu.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir