Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alikamilisha ziara yake ya Afrika kwa ziara ya Kenya mnamo Alhamisi, 30 Agosti 2018. Kabla ya ziara yake nchini Kenya, alikuwa amezuru Afrika Kusini mnamo Jumanne na Nigeria mnamo Jumatano. Ziara yake ni ya kwanza katika muda wa miaka mitano katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara na ya pili kwa Kenya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Uingereza katika muda wa miaka 30 tangu mwaka wa 1988 alipozuru Margaret Thatcher. Ziara hii inajiri wakati ambapo Uingereza iko karibu kuuacha rasmi uanachama wa Muungano wa Ulaya kufikia 29 Machi 2019. Ujumbe wake Afrika kote umekuwa upanuzi wa mipaka ya kibiashara na kuimarisha ile iliyopo kwa sasa.
Kuhusiana na ziara hii, sisi, katika Hizb ut Tahrir / Kenya, tunasema yafuatayo:
Mikataba yao ya kibiashara ambayo May na Kenyatta walijadili na kukubaliana si chochote isipokuwa upanuzi wa njia za kikoloni ili kuzipora rasilimali za Kenya na kumakinisha nidhamu ya kiuchumi ya kisekula ya kirasilimali iliyouangusha uchumi wa Kenya na kuwasukuma raia katika lindi ovu la umasikini na hali mbaya za kimaisha. Wenye kufaidika pekee na mikataba hii ya kibiashara daima wanabakia kuwa wachache miongoni mwa mabwenyenye na kikundi chao kidogo cha wapatilizaji fursa kinacho wazunguka wao kutoka katika sekta za kibinafsi na umma. Huku Kenya ikiwa kama soko la watumizi wenye papatiko na jaa la kumwaga bidhaa na huduma za Kiingereza na wakati huo huo kutoa ajira duni na yenye kutapatapa kwa makampuni ya kimataifa ya Uingereza.
Ushirika wao wa kiusalama ili kupambana na ugaidi si chochote isipokuwa ni muendelezo wa chuki kuu ya Uingereza dhidi ya Uislamu kwani Uingereza ndiyo iliyokuwa muhusika mkuu katika kuivunja Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 H / 3 Machi 1924 M. Fauka ya hayo, mtazamo muovu wa Waziri Mkuu May dhidi ya Uislamu ulithibitika kwa ukakamavu wake alipokuwa kama Waziri wa Ndani na ambao utaongezea kasi kwa serikali ya Kenya kuendelea katika vita vyake vya ndani dhidi ya misimamo mikali (kushikamana imara na Uislamu) na kijeshi nchini Somalia dhidi ya Al Shabaab kwa kutumia vikosi vya KDF na AMISOM.
Makubaliano yao juu ya ufisadi ni usanii tu na kutemea mate nyuso za Wakenya. Uingereza ndiyo mporaji mkuu wa rasilimali za Kenya na inaendelea kufanya hivyo kupitia watawala vibaraka wake wa kikoloni ambao wanatekeleza mfumo wake batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zitokanazo nao ikiwemo sera zake za kisiasa, kijamii na kiuchumi zilizoiacha Kenya kukwama kimaendeleo tangu 1963!
Kuhusiana na yale yanayoitwa maelewano ya pamoja juu ya mchakato wa Ujenzi wa Makubaliano ni thibitisho kuwa kwa hakika Uingereza imetambua kwa ujanja maridhiano kati yake na Amerika kupitia vibaraka wao wa kisiasa wa kieneo. Hivyo basi, Uingereza imepata nafasi ya kupumua ili kupanga njama yao nyengine dhidi ya Amerika kwa lengo ya kuidhibiti Kenya kikamilifu.
Kwa kutamatisha: Sisi katika Hizb ut Tahrir / Kenya tunaiona ziara hii kama tu mkakati makini wa Uingereza wa kurudisha haiba yake ya kiulimwengu iliyozorota hususan barani Afrika ambapo China inatumia ‘nguvu yake laini’, Amerika inatumia ‘mipango yake ya kupambana na ugaidi’ na mbeleni Muungano wa Ulaya kwa kutumia ‘mikataba yake ya awali ya kibiashara’ kuzitongoza zilizokuwa koloni zake. Hakuna chochote kilichopatikana isipokuwa Uingereza kudumisha uhusiano wake wa bwana na mtumwa wake kati yake na Kenya.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
KUMB: 14/ 1439 AH
Jumamosi, 21 Dhul Hijjah 1439 H /
01/09/2018 M
Simu: +254 707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke