Khilafah

Sasa ni karine moja, tangu ivundwe khilafah,

Umepotea umoja, umma hauna sharafa

Tunadhalilishwa waja, uchao kwetu maafa,

Turudisheni khilafah, ijekutupa faraja,

 

Amiri wetu mmoja, ndiye huyuno khalifa,

Atatuleta pamoja, pasi kujali masafa,

Kwa chombo hiki kimoja, kilo kwetu maarufa,

Turudisheni khilafa, kwa hima bila kungoja,

 

Kwa dalili na kwa huja, kusimamisha khilafa,

Ni faradhi kishataja, tumwa wetu mustwafa,

Iisimamie hija, na sharia za raufa,

Kuirudisha khilafah, na iwe ni yetu haja,

 

Kattu kwetu si kiroja, suala la ukhalifa,

Ni wadhifa ulokuja, baada ya tumwa kufa,

Kiidadi mikorija, walokuwa makhalifa,

Natum’bai’ khalifa, vyereje twajikongoja?

 

Sineni kwa kubwabwaja, ngao yetu ni khilafah,

Itatukinga na luja, nakuziba penye ufa,

Izza yetu letu  koja, itarudi na kafafa,

Turudisheni khilafah, isilamu kwa pamoja,

 

 

MTUNZI – MOHAMMED BAKARI

 

ALMUFTI

 

MOMBASA – KISAUNI