Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Ni miaka tisa sasa tangu Huduma za Ujasusi za Pakistan (ISI) kumteka nyara Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, Mhandisi Naveed Butt, mnamo Mei 11, 2012. Kuhusiana na tukio hili, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan imetoa taarifa mbili kwa vyombo vya habari:
Ya kwanza mnamo 03/01/2021 kwa anwani: “Agizo la Kumtoa Naveed Butt Lilitolewa Mnamo 4 Januari 2018, lakini Angali Hajaonekana wala Kuskika Tangu Kutoweka Kwake kwa Kulazimishwa mnamo 11 Mei 2012.”
Ya pili mnamo 02/05/2021: “Katika Kipindi cha Mwezi Uliobarikiwa wa Ramadhan, Wito wa Kuachiliwa Huru Naveed Butt, Mtetezi Halisi wa Khilafah, Aliyetekwa Nyara Tangu Mnamo 11 Mei 2012.”
Naveed alikuwa mtu wa kisawasawa kutoka Lahore, mlezi wa familia, mhandisi wa umeme, Muislamu mwenye ikhlasi, mtu wa tabaka nadra miongoni mwa wanafikra wa kisiasa na kimkakati, na msemaji rasmi wa chama cha kale cha kisiasa Hizb ut Tahrir / Pakistan. Hii ni orodha fupi tu ya sifa zake, lakini hakuna hata moja ya haya lililokuwa umuhimu kwa ISI wakati Naveed aliposukumwa kuingia kwenye moja ya “gari maarufu za Suzuki zenye sifa mbaya”, na kundi la karibu wanaume kumi wakiwa wamevalia sare, na mbele ya watoto wake walioandamana naye kutoka shule.
Naveed ni mtu wa tabaka maalum la wanafikra wa kisiasa wa Kiislamu ambao wana uwezo wa kipekee wa kutoboa joho la udanganyifu ambalo limetupwa kwenye mazingira ya kisiasa yanayooza. Hii ndio sababu Naveed aliweza kufikiria “ramani halisi ya utendakazi” ambayo nchi yake, Pakistan, ambayo anaipenda, inaweza kutambua ukuu wake. Ruwaza ambayo kwayo Pakistan inaweza kutumia vizuri faida zake za kijiografia, idadi ya watu, asili na za kiufundi na hivyo kuwa kituo cha mvuto katika Asia ya Kusini na Kati. Ruwaza ambayo kwayo Pakistan itaweza kuwa kituo cha nguvu kubwa katika Asia, na kufikia mwamko wa pili wa Umma wa Kiislamu, na kuzindua tena urithi wake ambao umeanza miaka 1,400.
Sababu ya ukosefu wa haki ambao Naveed alifanyiwa ni kukosoa kwake barabara maamuzi na matendo ya wanasiasa wakuu na maafisa, iwe serikalini au katika jeshi. Maamuzi na hatua ambazo, kwa upande mmoja, zilivuruga uwezo wa Pakistan, na kwa upande mwengine, zikivunja mshikamano wa karne nyingi kati ya jamii za Waislamu ambao walikuwa wameishi na kufanikiwa kwa muda mrefu katika sehemu hii ya Asia.
Moja ya msimamo wa ukosoaji wa Naveed ulikuwa ni juu ya vita jumla ambayo Pervez Musharraf aliendelea kupigana dhidi ya watu wa Magharibi mwa Pakistan. Jeshi la Pakistan lililazimika kupigana na kuua kaka na dada zake katika makabila ya eneo la FATA. Hii yote ilikuwa kwa ajili ya kupunguza shinikizo kwa jeshi la Amerika lililokuwa likiwakamata upande wa pili wa mpaka nchini Afghanistan. Vita vikali ambavyo vilidumu kwa miaka 17, ambavyo viliharibu miji, shule na nyumba, viliua makumi ya maelfu ya Waislamu, vilihamisha mamia ya maelfu yao, na kusababisha mpasuko mkubwa katika kitambaa cha jamii za Waislamu ndani ya Pakistan, ambacho bado kingali hakijatengenezwa.
Naveed aliwakosoa waziwazi majenerali mafisadi na maafisa vibaraka ambao wameruhusu kuenea hatari kwa ushawishi wa Amerika katika vituo nyeti zaidi vya taasisi za jeshi na serikali. Kila aina ya maafisa kutoka Shirika la Upelelezi la Amerika (FBI) na Shirika la Ujasusi la Amerika (CIA) walikuwa wamewekwa ndani ya idara ya “Makao Makuu ya Jeshi”, “Kitengo cha Operesheni za Kijeshi” na “Ujasusi wa Ndani” za jeshi la Pakistan kwa ajili ya usimamizi na kudumisha udhibiti. Na hivi sasa, kwa msaada wa majenerali na wanasiasa mafisadi, Amerika inafanya maamuzi juu ya silaha za kinyuklia na za kawaida, na maamuzi ya vita na amani nchini Pakistan. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِن تُطِيعُواْ الَّذِينَ كَفَرُواْ يَرُدُّوكُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُواْ خَاسِرِينَ]
“Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat’ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.” [Surah Aali-Imran 3:149].
Tangu walipomteka nyara Naveed, serikali zote mtawalia nchini Pakistan zimekataa bila aibu kujulisha mahali alipo; Hawaja punguza hata kwa uchache mateso kwa wapendwa wake, kupitia kumleta hata kwa muda mchange ili akutane na familia yake. Kwa muongo mmoja, wameziba masikio yao kwa wito wa familia yake na ndugu zake katika Umma wa Kiislamu na kila mtu aliyehurumia mateso yake. Kinyume chake, wakala za ujasusi zilitoa vitisho kwa familia yake kwamba ikiwa Naveed hakuacha kazi yake ya kisiasa, atauawa na mwili wake kutupwa mahali pengine.
Tuko hapa leo, na baada ya kuingia katika mwaka wa kumi wa utekaji nyara wake, bado tunaendelea kutaka kuachiliwa huru kwake, na tunamtaka kila Muislamu, mkubwa au mdogo, wa karibu au wa mbali, kushiriki katika juhudi hii iliyobarikiwa. Utekaji nyara wa Naveed unawakilisha nukta ya mgongano kati ya mapenzi ya mwenye haki na mapenzi ya msaliti.
Kwa Maafisa Wenye Ikhlasi na Watiifu katika Vyeo Vyote vya Jeshi la Pakistan:
Someni ayah zinazoambatana na miito yenye kuyapamba mabega yenu. Kumbukeni mafundisho ya itikadi asili ya kivita ya jeshi lenu. Angalieni usaliti unaofanywa kwa kaka na dada zenu katika maeneo ya FATA, Jammu na Kashmir. Angalia kutokuchukua hatua kwa wanaodhulumiwa nchini Myanmar, Msikiti wa Al-Aqsa na Ukanda wa Gaza.
Tunakuulizeni… Tangu lini jeshi la Pakistan limekuwa jeshi la maneno matupu, sio jeshi la vitendo?! Je! Tangu lini walinzi wa Uislamu wamekuwa ni watazamaji tu wa matukio?! Je! Silaha mnazozibeba zinafaida gani ikiwa sio za kuzuia na kulipiza kisasi?! Kwa nini simba katika vikosi vya jeshi la Pakistan wanatanua nguvu zao juu ya ulimwengu badala ya juu ya uonevu wa sasa wa Amerika?!
Hakika Ndugu Naveed ni mmoja wa mashababu wanaojulikana kwa kujitolea kwao kwa hukmu za Uislamu na tabia njema, mwanafikra mwaminifu, na mwanasiasa mashuhuri … Aliwasilisha ramani ya ukweli ya utendakazi ambayo ingeleta kheri na wokovu kwa Pakistan na nchi zote za Waislamu ulimwenguni … Ramani ya Utendakazi ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume Muhammad, (saw)… Lakini badala ya kumheshimu na kumthamini, watu mafisadi kati yenu walimteka nyara mahali kusikojulikana, La Hawla wala Quwatta illa Billah… Kwa hivyo, tunamtaka kila mmoja wenu mwenye ikhlasi kushinikiza mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru haraka kwa Ndugu Naveed kurudi kwa familia yake, ili apande minbar na kusema ukweli pamoja na ndugu zake wengine katika Hizb ut Tahrir.
Kwa Wanachama wa Ujumbe wa Kidiplomasia wa Pakistan:
Nyinyi mnawakilisha sura, sifa, historia na hivi sasa watu wa Pakistan ulimwenguni. Kupotezwa kwa nguvu kwa Naveed kunachafua sifa ya haki katika nchi yenu. Kwa hivyo tunakulinganieni mufanye sehemu yenu katika kumaliza aibu hii ambayo serikali imejiletea.
Kwa kila Muislamu anayetamani kuchomoza tena kwa siku za tukufu za Umma,
Kwa kila mwandishi wa habari ambaye amechukua jukumu lake kufichua uonevu na dhuluma,
Tunakulinganieni nyote: njooni mjiunge na kampeni hii kuishinikiza serikali ya Pakistan na majenerali wa jeshi lake kumwachilia huru Naveed Butt na kumunganisha tena na familia yake.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].
#FreeNaveedButt
Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir