Hizb ut-Tahrir Kenya yatuma ujumbe wake kwa ubalozi wa Pakistan ukibeba mwito wa Kusitisha utowekaji wa Naveed Butt.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Katika moja wapo ya sehemu ya kampeni ya Kiulimwengu kushinikiza serikali ya Pakistan na majenerali wa Kijeshi kumwachia huru Naveed Butt aweze kujumuika na Familia yake. Siku ya Jumane tarehe 29 Juni 2021 Hizb ut-Tahrir Kenya ilituma ujumbe wake katika ofisi za ubalozi wa Pakistani Jijini Nairobi.

Ujumbe huo uliongozwa na Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir/ Kenya Shabani Mwalimu aliesuhubiana na:

Yasin Kiwayo -Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano wa Hizb ut-Tahrir/ Kenya.

Yusuf Gasana  Mwanachama wa Hizb ut-Tahrir/ Kenya.

Ujumbe huo ulifika ubalozini majira ya saa nne na dakika thelathini na mbili (10:32 AM)  kwa majira ya Afrika Mashariki  ukakutana na kuzungumza na mmoja ya wafinyakazi kwa Jina la Charles ambae aliahidi kumpa balozi nakala tatu za taarifa kwa vyombo vya Habari kwa lugha tatu; Kiurdu, Kiarabu na Kingereza.

Taarifa hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir ilio na anwani: “Mwito wa kusitisha upoteaji wa mhandisi  Naveed Butt katika Wilaya ya Pakistan”, aliekuwa mzungumzaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir huko Pakistan alietekwa nyara miaka na majasusi wa Pakistan ambaye hadi leo hajulikani alipo. Tokea mwa wa 2012, tawala zilichokua hatamu nchini Pakistan zimekataa kubaini alipo na hali imefikia kiasi  kuwa majasusi wa Pakistan kuwatishia Familia yake kumwangamiza endapo hatositisha amali zake za Kisiasa za Hizb ut-Tahrir

Taarifa hiyo ya ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir pia ilikuwa na mwito kwa maofisaa wa ngazi ya juu wa Kijeshi ukisema: Someni aya tukufu zinaambatana na nembo zenu kwenye mabega yenu. Kumbukeni asili ya itikadi ya Jeshi lenu…

Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir, aidha ilielekeza mwito wake kwa wanadiplomasia wa Pakistan ukiwaambia:

“Nyinyi munawakilisha twaswira, maadili historia na hali halisi ya Pakistani kwa ulimwengu. Kupotezwa kwa Naveed kunachafua maadili ya haki ya nchi yenu. Tunatoa mwito kwenu kushiriki katika kusitisha fedheha hii ambayo serikali imejitia yenyewe ndani yake”.  Barua hiyo pia ikaeleza mwito kwa kila Muislamu na kila mwanahabari kushiriki kwenye kampeni hii ya kutia shindikizo kwa serikali ya Pakistan. “Tuna wapa mwito nyote:  “Njooni mshiriki katika kampeni hii to kutia shindikizo kwa utawala wa Pakistan na majenerali wa jeshi lake kumtoa Naveed Butt, aweze kuungana na familia yake”. MwenyeziMungu SWT:

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba kwenu msaada katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia .

[Al-Anfal: 72].

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir in Kenya

 Kumb: 14/1442AH

Jumanne, 18 Dhulqaada 1442AH

29/06/2021 CE