Chaguzi za Kidemokrasia: Njia ya kumakinisha Ukoloni Mamboleo

Habari na Maoni

Habari:

Baada ya IEBC kumtangaza naibu rais Dkt William Ruto  kuwa ndiye rais –mteule, ujumbe wa maseneta wa Amerika ukiongozwa na Seneta Chris Coons uliizuru Kenya. Ikumbukwe kwamba seneta Chris alikua mchangiaji mkubwa sana wa mazungumzo ya ‘handshake’ kati ya rais Uhuru Kenyatta na aliekuwa waziri mkuu wa Raila Omolo Odinga.

Maoni:

Ujumbe huu uliokutana na viongozi muhimu serikalini kiuhakika unahitaji kumulikwa kwa kina na kuangaliwa kwa umakini mkubwa. Kwa upande mwengine, balozi wa Uingereza nchini Kenya, Jane Marriot kwenye mtandao wake wa Twita akaandika kwamba: ‘Uingereza haiungi mkono au kupendekeza mgombea au chama chochote katika uchaguzi huu.

Marekani na Uingereza kuingilia mchakato wa kisiasa wa Kenya unaonesha wazi mapambano na kinyang’an’ganyiro kwa mataifa ya ulimwengu wa tatu ili ziendelee kuwekwa chini ya ushawishi na mduara uleule wa mabeberu wa kikoloni.Na hili ndilo linaloangaliwa zaidi na mataifa haya.

Ukoloni kama sera ya kigeni ya mataifa ya kimagharibi hujaalia chaguzi za Kidemokrasia zinabakia kuwa ni zana na uwanja kwa mapambano na kinyang’ang’anyiro kwa rasilimali za ulimwengu wa tatu.

Mataifa ya kimagharibi ya Kibepari yameweza kutunga urongo wa madaraka na uhuru ambao hata huwahadaa wasomi miongoni mwa wananchi. Hakika Demokrasia inabaki na itaendelea kuwa njia ya kikoloni kudumisha ukoloni mamboleo.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir twapenda kueleza kinagaubaga kwamba walimwengu hawatoweza kujikomboa kutoka pingu za ukoloni ispokuwa kupitia kusimamisha Uislamu kimfumo na kiserikali.

Imeandikwa kwa ajili ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na

Ali Omari

Mwanachama wa Ofisi ya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya.