Uchaguzi wa Urais Nchini Kenya

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Jibu la Swali

(Imetafsiriwa)

Swali:

(Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Odinga, mnamo Jumatatu: “22/08/2022,” aliwasilisha rufaa rasmi katika Mahakama ya Upeo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais alioshinda mpinzani wake, William Ruto, Naibu Rais anayemaliza muda wake. Shirika la Associated Press liliripoti kwamba Odinga aliwasilisha nyaraka za kupinga leo asubuhi kwa Mahakama ya Upeo ambayo yalazimika kujibu ndani ya kipindi cha siku 14 kulingana na sheria… 22/08/2022, Shirika la Anadolu). Mnamo Agosti 15, 2022, alitangazwa kwamba William Ruto alimshinda mpinzani wake Odinga kwa tofauti ndogo katika uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Kenya mnamo Agosti 9, 2022… Katika kampeni hizi za uchaguzi, Rais Kenyatta alionekana kumpinga naibu wake, William Ruto, na kumuunga mkono hasimu wake, kiongozi wa Upinzani Odinga baada ya maridhiano kufanyika kati yao. Je, huu ulikuwa ni mchezo wa Kenyatta kuonyesha kwamba anamuunga mkono mpinzani wake Odinga na kumpinga naibu wake, Ruto, ili kumhakikishia ushindi naibu wake dhidi ya mpinzani wake? Nini siri ya hatua za Amerika kwa Kenya? Je, kuna mgogoro kati yake na Uingereza?

Jibu:

Ili kufafanua jibu la maswali ya hapo juu, tunawasilisha mambo yafuatayo:

1- Angazo letu kwa Kenya ni kuwa ni sehemu ya eneo la Pembe ya Afrika, ambayo inachukuliwa kuwa eneo la Kiislamu lenye umuhimu wa kimkakati na kiuchumi.Watu wengi wa eneo hilo ni Waislamu na walitawaliwa na Uislamu. Nchi hizi zina mafungamano ya wao kwa wao na wengi wao walikuwa chini ya mabavu ya ukoloni wa Waingereza. Kenya ilikuwa imefungamanishwa na Sultan Muislamu wa Zanzibar hadi ilipoangukia chini ya utawala wa kikoloni wa Muingereza mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Licha ya kuwa Kenya ilipata uhuru wake tangu mwisho wa 1963, lakini huo ulikuwa ni uhuru bandia, kwani uhusiano wake na Uingereza ulionekana kupitia mawakala, Utawala wake ulifuatiwa na mawakala wa Uingereza tangu Jomo Kenyatta kutoka uhuru wakati wa uhuru bandia hadi 1978 kwenda kwa Daniel arap Moi hadi 2002, kwenda kwa Mwai Kibaki hadi 2013, hadi alipokuja Uhuru Kenyatta, mtoto wa rais wa kwanza Jomo Kenyatta. Na akashinda tena katika uchaguzi wa 2017. Uingereza inaunda mawakala kwa macho pevu kutoka kwa baba hadi watoto na mikononi mwa watawala mawakala ambao hawampi mamlaka yeyote isipokuwa akiwa ni kibaraka wa aina yao, na wa jinsia ya wasaidizi wao na uaminifu wao kwa mkoloni mwenyewe…

2- Amerika iliweza kujimakinisha katika kuchuma mawakala kutoka kwa upinzani, haswa Odinga, ambaye kabila lake linachukuliwa kuwa kabila la tatu nchini, na kwa sababu hii nchi ilianza kushuhudia mapambano ya kikoloni ya kisiasa ambayo yanachukua muondoko wa kikabila. Vyama vyake vinachukuliwa kuwa vya kikabila, na vinapata uungwaji mkono wa wafuasi wa makabila yake kwa jumla. Uhusiano wa kikabila ndio kiungo kati ya wanachama wa chama kimoja. Kila ulipofanyika uchaguzi, damu ilimwagika kupinga matokeo yao, kwa kasumba ya mtoto wa kabila letu. Naye William Ruto, rais mpya aliyetangazwa ushindi katika uchaguzi wa hivi majuzi, anatoka makabila ya Wakalenjin anayotoka Rais wa zamani Daniel arap Moi. Na Ruto anajivunia kuwa mwanafunzi wa rais huyu wa zamani, baada ya kujiunga na chama chake tangu mwaka wa 1992.

3- Matokeo rasmi yalitangazwa, huku Ruto akishinda kwa tofauti ndogo, kwani alipata 50.5%, huku Odinga akipata 48.8% ya kura. Itambuliwe kuwa kuna mgawanyiko ndani ya Tume ya Huru ya Uchaguzi, na mkuu wa tume ya uchaguzi, Wafula Chebukati, alisema: “Tumefunga safari ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanapata uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika, na safari hii haikuwa rahisi,” huku naibu wake, Juliana Cherera, akisema, “Hatuwezi kupitisha matokeo yatakayotangazwa kutokana na hali ya kutoeleweka ya awamu hii ya mwisho ya uchaguzi mkuu” (BBC 15/8/2022). Makamishna wanne kati ya saba wa tume ya uchaguzi yenyewe walikataa kutambua matokeo haya, na kuibua tuhuma za udanganyifu. Kulikuwa na maandamano kupinga matokeo. Odinga alisema: “Ili kuepusha mashaka, ningependa kusisitiza kwamba tunakataa kata kata na kutoridhika na matokeo ya urais yaliyotangazwa jana na Bw. Chebukati” (Anatolia 8/16/2022) na amekwenda katika Mahakama ya Upeo kwa rufaa rasmi mbele ya Mahakama ya Upeo. Shirika la habari la Amerika la ‘Associated Press’ lilisema kuwa “Odinga aliwasilisha asubuhi ya leo (tarehe 22 Agosti 2022) karatasi za pingamizi kwenye Mahakama ya Upeo, ambayo lazima ijibu ndani ya siku 14 kwa mujibu wa sheria.” Na iwapo mahakama itakubali rufaa hiyo, uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria, na hilo halitatengwa hadi wapinzani wanyamazishwe kwa sababu tofauti ni ndogo sana kati ya pande hizo mbili na kwa sababu Tume ya Uchaguzi imegawanyika, na ili kusiwepo vitendo vya vurugu na misukosuko ya matokeo mabaya, inaufanya upinzani uwe na matumaini ya kushinda duru ya pili iwapo hilo litatangazwa au kuwekwa itifaki juu ya muundo wa maridhiano kati ya pande hizo mbili kama kumpa Odinga uwaziri mkuu baada ya kuundwa mara nyengine tena!

4- Kama ilivyo desturi, upinzani hudai udanganyifu katika uchaguzi unaposhindwa, hasa nchini Kenya wakati upinzani huu ni wa Marekani na mshindi ni kutoka kwa mawakala wa Uingereza, na kinyume chake hutokea katika nchi nyingine zinazodhibitiwa na mawakala wa Wamarekani. Kwa sababu kila timu inataka kushinda kwa namna yoyote ile na hutumia ushawishi wao pale inapoongoza. Katika uchaguzi wa 2007, kila upande ulidai kushinda uchaguzi huo. Mapigano yalianza kati ya pande hizo mbili za mzozo, na damu ikatiririka, takriban watu 1,200 waliuawa, na mamia kwa maelfu walilazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi ya kikabila. Lakini katika suala hili, ujanja wa Kiingereza ulichangia kusitisha upinzani, hivyo uliweka mtego kwa kumpa Odinga nafasi ya uwaziri mkuu na Kibaki alibaki kuwa rais wa nchi, na mamlaka yote mkononi mwake, na kuweka vikwazo katika utekelezaji wa madaraka ya waziri mkuu. Lakini Kenyatta, ambaye alitangazwa ushindi wake katika uchaguzi wa 2013, alifuta wadhifa wa waziri mkuu ili kuchukua mamlaka yeye pekee. Katika uchaguzi wa 2017, upinzani ulidai udanganyifu na kutaka Mahakama ya Upeo kurudia uchaguzi huo. Uchaguzi ulirudiwa Oktoba 2017, na upinzani ukasusia, na Kenyatta na naibu wake, William Ruto, kutangazwa washindi. Pamoja na kujua kuwa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliingilia kati suala hilo kwa vile ana asili ya Kenya! Alitoa wito wa utulivu na kukubalika kwa matokeo ya uchaguzi, kwa sababu alijua kwamba uchaguzi ukifanyika, mawakala wa Uingereza watashinda tena, kwa sababu bado wangali wanaidhibiti dola hiyo, na kwa hili alitaka kupata baraka kwa watawala wa Kenya ili ushawishi wake kwao uwe na nguvu zaidi na hivyo kuimarisha ushawishi wa Amerika nchini Kenya na kutumia shinikizo ili mawakala wao wa baadaye waweze kufikia utawala. Lakini Uingereza ilikwepa mawakala wake kila mara ili kudumisha ushawishi wake wa vitisho nchini Kenya. Iliihadaa kupitia wakala wake Kenyatta kana kwamba inampenda wakala wa Marekani Odinga na kumfanya wakala wake Ruto ashinde.

5- Ni mara ya tano kwa Raila Odinga kutangaza kuwania kiti cha urais na kugombea na kushindwa katika uchaguzi. Hapo awali aligombea mara nne mnamo 1997, 2007, 2013 na 2017, lakini mawakala wa Uingereza wanaodhibiti ulingo wa kisiasa nchini Kenya hawakumwezesha kushinda. Alikuwa na matumaini ya kumrithi Uhuru Kenyatta, ambaye mihula yake miwili imekamilika na hawezi kuwania muhula wa tatu kwa mujibu wa katiba. Odinga na Kenyatta msuluhishi walisimama baada ya kupeana mikono Machi 9, 2018, baada ya miezi kadhaa ya mapigano ya umwagaji damu kati ya wafuasi wao, kutotambua ushindi wa Kenyatta na kujitangaza kuwa rais wa Kenya, na kwa kupeana mikono huku, kulitangazwa kumalizika kwa migawanyiko kati yao na kutambuliwa kwa urais wa Kenyatta. Odinga alimsifu Kenyatta kwa “hisia yake ya uzalendo katika kuanzisha mazungumzo ambayo yalisababisha kupeana mkono wa heri.” Na wengine wakadhani wamefikia makubaliano ya kumtaka Odinga kumrithi Kenyatta, au Odinga amegeuka kuwa wakala wa Muingereza! Lakini Kenyatta na mawakala wa Uingereza hawakuhadaiwa na upatanisho huu, bali waliutumia kwa manufaa yao. Kenyatta alicheza mchezo wakati wa kampeni za uchaguzi kwa kuonyesha kwamba alimuunga mkono Odinga, akisema “Ruto hastahili na hafai kuchukua wadhifa wa juu zaidi nchini.” Ruto akajibu kwa kusema: “Hakika Kenyatta anataka amrithi ali awe rais kikaragosi”  (BBC 16/8/2022)

6- Inajulikana kuwa Chama cha Ruto kiliungana na Chama cha Kenyatta walipoafikiana mwaka wa 2012. Kisha, chama chao tawala kikapanuka, Chama cha Jubilee kikaundwa kutoka kwa muungano wa vyama 11 mnamo 9/8/2016 ili kushiriki uchaguzi wa 2017 na kiliongozwa na Kenyatta baada ya kuwa muungano wa kisiasa mwaka 2013 kumuunga mkono Kenyatta katika kampeni zake za uchaguzi. Ruto alikuwa mshirika na naibu katika vipindi vyote viwili, na alikuwa mfuasi wa wakala wa zamani wa Kiingereza, Rais wa zamani Daniel arap Moi, na alikuwa akihamasisha vijana kwa msaada wake, hivyo akapata kibali chake na kuanza kumpandisha vyeo serikalini. Ameshika nyadhifa za uwaziri akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kilimo na Waziri wa Elimu ya Juu. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilimshtaki yeye pamoja na Kenyatta kwa kufanya uhalifu mwaka wa 2007 na 2008, na waliondolewa mashtaka na mahakama hiyo inayodhibitiwa na Ulaya. Kenyatta aliondolewa mashtaka mwaka wa 2014 na Ruto akaondolewa mashtaka 2016 ili kushiriki katika uchaguzi wa 2017 na kutangazwa ushindi wao ushindi ndani yake, huku Kenyatta akiwa rais na Ruto akiwa naibu wake. Kwa sababu hii, Ruto ni mmoja wa mawakala walioidhinishwa wa Waingereza, na hafikiriwi kuwa ataachiliwa kirahisi na nafasi yake kuchukuliwa na Odinga, wakala wa Amerika, kwa mujibu wa makubaliano hayo, isipokuwa ni hadaa tu iliyoratibiwa na ujanja wa Waingereza!

7- Kenyatta alizuru Uingereza kati ya 26 na 29/7/2021 na kukutana na Waziri Mkuu Johnson na kutangaza kuwa lengo la ziara hiyo ni “kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Kenya na Uingereza” na pande hizo mbili zilitia saini makubaliano mapya ya ushirikiano wa ulinzi kwa miaka mitano. Alitangaza kuwa makubaliano hayo yanalenga “kuimarisha na kutilia nguvu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kukabiliana na changamoto za pamoja za usalama katika Afrika Mashariki” (BBC ya Uingereza). Uingereza haikufanya kama ilivyofanya Marekani na kuibua suala la Nyaraka za Pandora, masuala ya haki za binadamu na masuala ya ufisadi wakati Kenyatta alipoitembelea, haikufanya hivyo kwa sababu ya uaminifu na utii wake kwake! Kumbuka kuwa Uingereza ina kambi mbili za kijeshi nchini Kenya chini ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili, mojawapo ikiwa karibu na Nairobi, mji mkuu wa Kenya, na dhamira yake ni kusaidia kuleta utulivu wa utawala nchini Kenya kwa manufaa ya ushawishi wa Uingereza na kuondoka kutoka huko hadi maeneo mengine kulinda ushawishi huu, na nyingine iko kaskazini mwa Kenya ambayo dhamira yake ni kutoa mafunzo kwa vikosi vya Uingereza vinavyojiandaa kupigana katika maeneo ya jangwa na nusu jangwa. Vikosi vya Uingereza vinafanya mazoezi katika eneo la nchi kavu sawa na mara nne yale ambayo jeshi la Uingereza hutumia katika nchi yake na silaha za moto na risasi zinazoiga hali halisi ya vita. Ripoti za vyombo vya habari zilisema kuwa wanajeshi wa Uingereza waliopigana nchini Afghanistan walikuwa wamefunzwa katika kambi hii nchini Kenya. Ndio maana Amerika inatilia maanani Kenya umuhimu mwingine kwa sababu ya uwepo wa misingi hii ya Kiingereza, kwani inafanya kazi ya kuiondoa kutoka huko.

8- Inaonekana Uingereza, wakati wa ziara ya Kenyatta kwao, ilimtaka aandae ziara ya Amerika ili kuwaonea huruma na kuthibitisha maridhiano na Odinga ili Marekani isifanye “matendo ya kuvuruga” uchaguzi unaokuja. Kwa hiyo, mipango ilikuwa ni kuzuru Amerika, na ndivyo ilivyokuwa baada ya takriban miezi miwili kutoka katika ziara yake nchini Uingereza, Rais Biden wa Marekani alimpokea Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mnamo 14/10/2021, na ndiye rais wa kwanza wa Afrika kupokewa na rais wa Marekani. Msemaji wa Ikulu ya White House Jen Psaki alisema marais hao wawili watajadili “uhusiano thabiti wa nchi mbili pamoja na haja ya uwazi na uwajibikaji katika mifumo ya fedha ya ndani na kimataifa.” Jina la Kenyatta lilitajwa katika uchunguzi wa “Nyaraka za Pandora” uliofanywa na Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi juu ya kupambana na ufisadi, yeye pamoja na watu sita wa familia yake wanamiliki kwa siri mtandao wa makampuni 11, ambayo moja inamiliki hisa zenye thamani ya dolari milioni thelathini. Akijibu taarifa hiyo Psaki aliongeza kusema “Rais siku zote amekuwa akikemea mambo yasiyolingana (matumizi mabaya) katika mfumo wa fedha wa kimataifa, hii haimaanishi kuwa hatutakutana na watu tunaotofautiana nao, kuna masuala kadhaa ambayo tunayo nia ya kufanya kazi na Kenya na hilo ndilo litakalokuwa lengo kuu [la mkutano kati ya marais hao wawili.) Marais hao wawili watajadili juhudi za kutetea demokrasia na haki za binadamu, kuendeleza amani na usalama, kuharakisha ukuaji wa uchumi na makubaliano na mabadiliko ya tabianchi” (AFP 14/10/2021).

Amerika ilijaribu kutumia nyaraka hizo kutia shinikizo kwa Kenyatta kutangaza kuunga mkono ugombezi wa Odinga, ilifanya hivyo na akaonekana ni mfuasi wa Odinga, lakini uungwaji mkono huu haukuwa wa dhati, bali ni wa kinafiki ili kuficha kashfa zake ili Marekani isiwachokoze na kumchafua, hivyo ilikuwa vigumu kwake kugombea kwa muhula wa tatu na Amerika ilitikisa upinzani wake kwa mfano huo… Mnamo Novemba 17, 2021 Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika alizuru Kenya kama sehemu ya ziara yake ya Afrika iliyojumuisha pia Nigeria na Senegal, ambayo ilidumu kwa wiki moja. Alisema alipokuwa katika mji mkuu wa Nigeria: “Serikali zimekuwa na uwazi mchache,”. Hili linafanyika kote barani Afrika. Viongozi wanapuuza mipaka ya utawala, wizi au kuahirisha uchaguzi, kutumia malalamiko ya kijamii ili kupata na kudumisha mamlaka, kukamata viongozi wa upinzani, kukandamiza vyombo vya habari na kuruhusu huduma za usalama kuweka vikwazo vya kikatili kwa janga la maambukizi (Korona)” (Asharq Al-Awsat 21/11/2021).

Vile vile, misingi ya chama cha Kenyatta ilikuwa ikifanya kazi ya kutafuta uungwaji mkono kwa Ruto, huku makubaliano ya ndani ya chama yakiwa miongoni mwa mawakala walioujua mchezo huo na kumchagua Ruto licha ya kujifanya kumpinga.

9- Nchi nyingi za Afrika chini ya ushawishi wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Kenya na Senegal, zinafanya kazi ya kuimarisha China dhidi ya Amerika, ambayo inajitahidi kupanua ushawishi wake ndani yake. Senegal, chini ya ushawishi wa Ufaransa, inaimarisha uhusiano wake na China. Ilikuwa mwenyeji wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika katika mji mkuu wake, Dakar, kati ya Novemba 29 na 30/11/2021, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Isata Tal Sal alisema, “Tuna diplomasia huru, ambayo hatuzuii mtu yeyote.” Wakati ushawishi wa Amerika barani Afrika, bado ni mdogo tofauti na ushawishi wa Uingereza na Ufaransa, inafanya kazi ya kuimarisha kwa njia na kazi mbalimbali Ili kushindana na ushawishi wa kiuchumi wa China ambao Uingereza na Ufaransa zinaimarisha ili kuimarisha mawakala wao barani Afrika. Hivi majuzi, Diwani wa Jimbo la China na Waziri wa Mambo ya Nje, Wang Yi alizuru Kenya mnamo 6/1/2022, na kukutana na Rais Kenyatta, ambaye alisema: “China sio tu rafiki wa dhati wa Kenya, bali pia ni mshirika wa maendeleo wa ushirikiano wa karibu… mafanikio ya maendeleo hayataweza kupatikana bila uungaji mkono mkubwa wa China… Kenya inapenda kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana na China ili kufikia maendeleo ya pamoja,” huku Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akisema, “China inapenda kuimarisha ushirikiano wa pande mbili pamoja na Kenya kuisaidia kuimarisha uwezo wake wa kujiendeleza, kuharakisha ukuaji wa viwanda na kukuza Mshikamano na uratibu nayo katika masuala ya kimataifa na pande nyingi.” Wang aliwasilisha “Mpango wa Maendeleo Salama katika Pembe ya Afrika.” Kenyatta alisema, “Mpango huu unakidhi mahitaji ya dharura ya nchi za Pembe ya Afrika, na Kenya inakubali kucheza dori katika suala hili” (Xinhua 6/1/2022). Haya yote yanaikasirisha Amerika, ambayo inajitahidi kudhoofisha ushawishi wa Ulaya barani Afrika na pia kufanya kazi kupunguza nguvu inayokua ya China.

10- Mukhtasari ni kwamba ushawishi wa Uingereza bado una nguvu nchini Kenya na wengi wa wahusika wa kisiasa ni miongoni mwa mawakala wake, huwaunganisha haja inapotokea na pia huwagawanya inapobidi. Iwapo hapana budi kuwepo na makubaliano kati ya mawakala wake na mawakala wa Marekani, na kisha kugawanya mamlaka pamoja nao huku ikishikilia udhibiti, inafanya hivyo na kuwaagiza wateja wake kupatanisha na kuhitimisha makubaliano katika suala hili. Na ikiwa itafaulu kumweka wakala wake Ruto madarakani na akafanikiwa kunyamazisha upinzani, basi hatamwagiza wakala wake kufanya hivyo, kwa kuwa wako mikononi mwake na wanatafuta tu mamlaka, kwa namna ya mawakala wa Marekani. Hii ndio desturi ya mawakala katika kila nchi. Kwa upande wa Amerika, haitaondoka uwanjani na itafanya kazi ya

kuimarisha ushawishi wake nchini Kenya, na haipendezwi na umwagaji damu, machafuko na ghasia ndani yake na katika nchi zingine za Kiafrika. Inafanya kazi kwa mitindo na mbinu mbalimbali, iwe ni za kiuchumi, kisiasa, au katika ngazi ya usalama na kijeshi. Inafanya kazi ya kuvuna mawakala katika sekta hizi mbili kwa jina la uwekezaji wa usalama na kusaidia kutoa mafunzo kwa jeshi na vikosi vya usalama, na kisha inafanya kazi ya kuandaa mapinduzi kama ilivyofanya nchini Mali au kuchochea uasi kama ilivyokuwa nchini Chad, uasi huo ulisababisha kuuawa kwa wakala wa Ufaransa, Idriss Deby.

Kwa hivyo, nchi hizi, nyingi zao zikiwa ni nchi za Kiislamu, zimesalia kuwa uwanja wa mvutano wa kimataifa, haswa kati ya Amerika, Uingereza na Ufaransa. Hakuna matumaini kwa nchi hii kuondokana na mvutano huu wa kikoloni unaoifanya kuwa nyuma na ilhali ni miongoni mwa nchi tajiri zaidi kwa rasilimali, isipokuwa kwa kurudi Khilafah kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ametoa bishara njema ya kusimama kwake kwa kusema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Imepokewa na Ahmad.

1 Safar 1444 H

28/8/2022 M