بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir Kenya ilizindua msururu wa amali za jumuia katika misikiti baada ya swala ya Ijumaa juu ya Kumbukumbu ya 98 Hijria ya kuvunjwa Khilafah.
Iliwakumbusha Waislamu kumbukumbu chungu ya kuangamizwa Ummah wa Kiislamu mnamo Machi 3, 1924. Umma wa Kiislamu unaendelea kuteseka kutokana na kukosekana kwake na kuwasihi Waislamu kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kuasisi maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.
Mnamo Jumanne, 26 Muharram 1440 H ikiafikiana na 2 Aprili 2019 M – Tuliandaa ugawanyaji mkubwa wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kwa anwani, Hizb ut Tahrir / Kenya Ilikamilisha kwa Mafanikio Kampeni Maalumu chini ya mwito – Ongezeko la Gharama ya Maisha: Uislamu Ndio Suluhisho mabarabarani, masokoni nk. Zaidi ya hayo, tulituma ujumbe hadi Ubalozi wa China nchini Kenya. Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Kenya, Arkanuddin Yassin akiandamana na Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya. Waliwasili katika ubalozi huo jijini Nairobi saa 8:56 asubuhi kwa Saa za Afrika ya Mashariki. Ubalozi huo wa China ulikataa kupokea au kutambua upokezi wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa anwani Khilafah itaikomboa Turkistan Mashariki na Kuwaokoa Uyghur kutokana na ugandamizi wa kihalifu wa China. Fauka ya hayo, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Kenya ilitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kwa anwani Dola na Utawala wa China Inaogopa Mwito wa La Ilaha illah Allah.