Uzinduzi rasmi wa kampeni kubwa ya Hizb ut-Tahrir Kenya chini ya kauli mbiu: BBI: Mchezo uleule Mbinu mpya.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya inafuraha kuanzisha rasmi kampeni kubwa itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu yenye kauli mbiu “BBI mchezo uleule Mbinu Mpya inayoanza Jumamosi tarehe 15th Februari,2020 na kumalizika tarehe 24th Mei 2020.

Ripoti ya mradi wa ujenzi wa madaraja iliosajiliwa katika gazeti rasmi la serikali tarehe 24th Mei 2018 na kuwekwa wazi kwa umma kuisoma mwezi Novemba mwaka jana, inadaiwa kuwa ni mwanzo mpya unaodhaniwa kuleta sera za ushirikishi, mabadiliko ya kiuchumi na kutatua  tatizo la siasa za kibwenyenye na ufisadi – matatizo ambayo yamekuwa ni yenye kuikabili Kenya zaidi ya nusu karne. BBI ambayo tayari imeibua tafrani miongoni mwa tabaka la kisiasa inakuja baada ya mwongo mmoja tu wa uzinduzi wa katiba ilioleta mfumo mpya wa utawala wa kiugatuzi na bado nchi inakumbana na matatizo hayohayo.

Kampeni hii inalenga kuangazia kiini na chanzo halisi cha majanga yote yanayoikabili Kenya na ulimwengu kwa ujumla ambacho si chengine ispokuwa ni Mfumo wa kikoloni wa kibepari na siasa yake ya Kidemokrasia inayotanguliza zaidi maslahi ya tabaka la wanasiasa na kupuuzilia mbali maslahi ya walala hoi wanaondelea kusugua maishani. Kampeni hii aidha inanuia kutoa  taswira halisi ya nguvu ya itikadi ya Kiislamu katika kuunganisha jamii kwa mshikamano wa kudumu na kuwa wote ni umma moja na waja wa Mwenyezi Mungu (swt), pia kutatua matatizo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ambayo hayakabili tu jamii ya Kenya bali jamii zote duniani.

Katika kufanya kampeni hii, Hizb ut-Tahrir Kenya itaandaa misururu ya amali ikiwemo darsa kubwa katika maeneo mbalimbali, mazungumzo ya mitaani, semina za wasomi na mufakirina miongoni mwa amali nyengine.

Mwisho, tunatoa mwito kwa umma jumla na hasa umma wa Kiislamu kushiriki nasi katika kampeni hii tukufu ambayo tutajikita ndani kueleza mengi yenye kuleta manufaa sio ya hapa duniani bali pia Akhera.

Fuatilia Kampeni hii kwa Hashtag :

#BBIMchezoUleuleMbinuMpya

 

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir in Kenya

 

 

REF: 07/ 1441 AH

IJUMAA 20 JUMADA II 1441/

14/02/2020  CE