بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir Kenya ilizindua msururu wa amali za jumuia katika misikiti baada ya swala ya Ijumaa juu ya Kumbukumbu ya 98 Hijria ya kuvunjwa Khilafah.
Iliwakumbusha Waislamu kumbukumbu chungu ya kuangamizwa Ummah wa Kiislamu mnamo Machi 3, 1924. Umma wa Kiislamu unaendelea kuteseka kutokana na kukosekana kwake na kuwasihi Waislamu kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kuasisi maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.
Mnamo Jumatano, 27 Rajab Muharram 1440 AH / 3 Aprili 2019 – Tuliandaa maandamano baridi katika miji mikuu ya Kenya yaani Mombasa na Nairobi. Wazungumzaji walioongozwa na Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya; waliangazia hali za sasa za Ummah wa Kiislamu kote ulimwenguni kutokana na kuvunjwa kwa Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 H (3 Machi 1924 M). Zaidi ya hayo, waliwasilisha suluhisho la Kiislamu ambalo liko katika kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume.