Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halaqa 4: Nukta ya Maingiliano

Tutazungumzia leo marhala ya pili miongoni mwa marhala za Daa’wah ya Mtume (saw) nayo ni Nukta ya Maingiliano na jamii ili kupatikane: Rai Aam/Rai ya Ummah inayotokana na Waa’ yi Aam/Muamko wa Ummah.

Nukta hii ya Pili ilikuwa situ ya maingiliano na jamii bali yalikuwa mapambano yaliyojumuisha mvutano wa kifikra na vitendo vya kisiasa. Mtume (saw) aliifanya Ummul Quraa (Mji Mtukufu wa Makkah) ndio kitovu cha Daa’wah yake na kufika sehemu zilizouzunguka mji wa makkah, baada ya mfumo wa Uislamu kua ndio mwili wa maswahaba wake watukufu, Na zikawa fikra za Uislamu na fahamu zake kwao ndio Njia ya maisha yao.

Maqureysh wakasimama dhidi ya Mtume (saw) msimamo wa Uadui na kutumia mbinu Nne (4) dhidi yake na wafuasi wake.

Tutazitaja katika hii Halaqahna tutazizungumzia kwa ufafanuzi kiasi katika Halaqa Toleo zijazo In Shaa Allah.

  1. Ni kumbembeleza/kumrai Mtume (saw) ili awache Da’wah
  2. Propaganda/Uvumi dhidi ya Mtume (saw) na  Da’wah.
  3. Kuwakata/Kuwatenga Mtume (saw) na Wabebaji Da’wah.
  4. Kumuudhi na kumuadhibu Mtume (saw) na Wabebaji Da’wah.

Itaendelea katika UQAB Toleo 9…In Shaa Allah.