BBI-WALA SI MCHEZO WA MWISHO WA KUMALIZA UFISADI

Habari

Mnamo tarehe 27th Novemba, 2019 jopo kazi la BBI pamoja na viongozi wa kisiasa waliitangazia wazi kwa umma repoti ya BBI. Ndani mwa repoti hio ilibainika kuwa ufisadi ni miongoni mwa mambo tisa yaliokuwa na umuhimu kuangaziwa iwapo taifa lingependa kustawi. Katika mlango wa nane wa repoti hio, ufisadi uilijadiliwa na mapendekezo juu yake kutolewa ikitarajiwa kwamba laiti yatatabikishwa basi ufisadi utakuwa ni jambo la kusahauliwa.

 

Maoni:

Kutoka kubuniwa kwa taasisi ya ufisadi hadi kubuniwa kwa nambari za mawasiliano za dharura, kwa kweli mengi yamependekeza na kutekelezwa lakini hayakuweza kuangamiza ufisadi.
Mnamo Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2016 katika juhudi za kupambana na ufisadi, Macharia Gaitho alipendekeza katika makala yake kwenye gazeti la Nation ya kwamba “Pengine twahitaji kuomba suluhu la Uchina dhidi ya ufisadi.” Hata hivyo suluhu hili la Uchina limebainika ya kwamba si la uhakika. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph ni kwamba mapambano juu ya ufisadi Uchina licha ya kuwa na sharia kali dhidi yake hayajapelekea kupungua visa vya ufisadi. Wachambuzi wasema ya kwamba kampeni hio ilikuwa haina uwazi na ilikuwa tuu njia moja wapo ya kuwaondoa mahasimu katika nafasi nyeti.

Katika miaka ya nyuma, serikali iliamua kutekeleza mapendekezo ya kuimarisha  taasisi zake kama njia mmoja wapo ya kupambana na ufisadi.Kwa hivyo, sharia mpya zikatawazwa na taasisi kuwezeshwa na rasilimali pamoja na kuwa huru na mamlaka yakutosha. Mnamo katika masiku ya kongamano la mapambano dhidi ya ufisadi yaliokuwa yameandaliwa ikulu ya Nairobi mnamo tarehe 18 Octoba, 2016, viongozi tofautu wa taasisi za umma walihojiwa juu ya vipi mapambano ya ufisadi  hayaja leta natija licha ya yote? Walijibu kwa kutupiana lawama juu ya taasisi ipi ndio ilikuwa kisiki juu ya kufaulu kwa mapambano ya ufisadi. Kupitia mchezo wa kulaumiana, taasisi mbali mbali ziliashiria kwa namna gani haziwezi kupambana na ufisadi licha ya kuwezeshwa kwa hali ya juu. Katika onyesho la fedhea kwa kushindwa vita dhidi ya ufisadi licha ya kujihami na katiba mpya, raisi aliinuka na kusema,”Nimechukuwa hatua ambazo zilitulazimu kwa mujibu wa katiba,hivyo mnataka nifanye nini tena?” Kwa kweli matokeo ya kongamano hilo la mapambano dhidi ya ufisadi yaliashiria kwamba kuwepo kwa taasisi za umma zilizo kuwa huru na kutoshelezwa kirasli mali si tuu ni suluhu dhidi ya vita vya ufisadi.

Katika muhula wake wa pili wa utawala raisi Uhuru huku akiwa na matumaini ya kufaulu, aliamua kupambana upya na ufisadi kwa kubadilisha viongozi mbali mbali wa taasisi zinazo husika na mapambano dhidi ya ufisadi.

Kwa kuashiria kupendezwa na mbinu hii, raisi alisema,” Baada ya kusafisha afisi ya DPP na DCI,sasa tuna timu inayo ajibika.Mumeanza kuona maovu makubwa yakifichuliwa nah ii ni mwanzo tu, Bado hamujaona chochote.” Lakini kwa mbinu hii kupatikana mapendeleo ndani yake, baadhi ya viongozi wa kisiasa   pamoja na jamii zao walisusia juhudi hii mpya dhidi ya ufisadi. Naibu wa raisi Ruto mwenyewe alisikika akikosoa namna kiongozi wa kuendesha mashtaka wa umma Bw. Haji na yule wa uchunguzi wa uhalifu Bw.George Kinoti walivyokuwa wakifanya kazi zao kwa kuwa na mapendeleo ya kulenga watu fulani pekee. Katika hotuba yake  kwenye kongamano la LSK Huko Mombasa, Naibu wa raisi alisema,” Vita dhidi ya ufisadi ambavyo vimekosa uadilifu hupotea kuwa ni vita dhidi ya ufisadi  bali enyewe huwa ufisaidi kamwe.Vita ambavyo havina uadilifu huwa ni kutokujali.Vita adilifu vinavyopiganwa kwa kuchaguwa, kutumia ukweli nusu, na kuwepo maono tayari ya kisiasa kwenye bongo, ni vita vya kutokujali.”

Kwa ufupi, mapambano dhidi ya ufisadi hayatoweza kushindika kwa kupitia njia zilizobuniwa na mfumo wa kirasilimali kwa kuwa ni urasilimali ndio asili umewafanya watu kuwa wafisadi. Pindi Urasilimali ulipotengamanisha mada na roho, na kufanya uchumaji wa vitu vya kushikika ndio lengo kuu la maisha, na kipimo cha vitendo ni maslahi, basi ilikuwa ni jambo la kimaumbile ya kwamba ufisadi utakuwa ndio mtindo wa maisha wa jamii. Laiti mada haingetenganishwa na roho, basi mtu angelikuwa saa zote ni mwenye kutanabahi fikra ya kutunzwa na kuadhibiwa, kupata pepo au moto, kuwa na vitendo vyema au viovu kabla ya kutekeleza vitendo. Laiti akili haingelifanywa ndio chimbuko la kutunga sharia, mwanadamu angeli hukumu katika maisha yake kwa mujibu wa kile allicho amrisha Maulana na kwa hivyo ufisadi ugelikuwa ni jambo la kale kwani sharia za Maulana zingeleta uadilifu na amani. Licha ya hivyo, laiti mwanadamu angelifanya msingi wa matendo yake ni kupata radhi za Mola wake na wala si vitu vya kushikika basi mwanadamu angelikuwa amelindwa  kwa kutekeleza mazuri na kuepuka maovu yakiwemo ufisadi.

Katika jinamizi hili la kutoelewa ni kwa jinsi gani nzuri twaweza kuangamiza ufisadi hususan baada ya kumaliza kutekeleza mapendekezo  kwa mapendekezo, imefika wakati muafaka kwa watawala kusikiza sauti za ndanii zilizo kamilika za kisiasa za kiisilamu. Kama vile ilikuwa wajibu kwa wao kutabani na kutabikisha sehemu chache ya fikra ya nidhamu ya fedha ya kiisilamu, basi nyakati imefika iwe si tuu kuchukuwa sehemu katika islamu bali imefika wakati kuchukuwa uwongozi kamili wa kifikra ya kiisilamu kwani kwa uhakika ni uisilamu pekee ndio badili ya mfumo wa kirasilimali ambao ndio chanzo cha ufisaadi.
“Na inaposemwa kwao wao,”Musifanye uharibifu katika ardhi, ’’wao husema, “Siwe ni watengenezaji.” TYQ  2:11

ABU LEILA,

March 1, 2020.