JE BBI ITAWEZA KUWAFUNGAMANISHA WATU WATAIFA LA KENYA ?

Mnamo Jumanne 27th Novemba 2019, wakenya kutoka sehemu mbali mbali walijumuika Bomas ya Kenya na kusherehekea kwa kutangaziwa rasmi repoti ya BBI
kwa wananchi. Repoti hio ya kurasa 156 ilikuwepo na agenda tisa na kauli mbiu yake ikiwa: Kujenga Daraja hadi  kuwa na Kenya ilio moja: kutoka taifa lililo fungamanishwa na damu hadi kuwa taifa la maadili. Katika kurasa zake za mwanzo za repoti hio, Jopo kazi la BBI lilimuandikia raisi kwa kusema,” ilikuwa fursa dhahabu kwetu , na kwa uweza tuliopewa wa kubaini husuba za taifa kamavile ilivyo tambulishwa katika kauli ya pamoja ya Ujezi wa Daraja kwa taifa jipya la Kenya, na baada ya kutekeleza wajibu huo, basi
tume pendekeza mapendekezo ambayo yatajenga umoja wa kudumu.”
Katika mazungumzo yake mnamo siku ya kutangazwa rasmi repoti ya BBI, raisi alisema,” Hebu tu shughulike na lile linalotuunganisha sisi  na kuwa wa moja na hebu tuondoe ukabila,”

Kwa kutizama hayo yalio juu, inabainika ya kwamba mchakato wa BBI unafikiriwa kuwa ni wenye kuita watu kuwa kitu kimoja. Kwa hakika mwita wa, umoja na utafutaji wa juhudi za kuwaungamanisha wakenya si jambo geni. Mnamo jumapili tarehe 6 Septemba 2016 kiongozi wa wabunge wengi, Aden Duale katika mkutano hapo Mlango Kubwa alisikika akisema,” Kura za mwaka wa 2017 zitakuwa ni kati ya Jubilee ambayo inaamini umoja wa makabila 42 na wale ambao wapo tu huko kugawanya watu  kwa siasa za kikabila.” Kwa kutumia jukwaa hilo hilo,Bwana sakaja nae kasema,” Ni wakati sa hii yatulazimu tuseme hapana kwa ukabila kwa jina la chama cha kisiasa. Jubilee imekuja kuwaunganisha wakenya chini ya kivuli kimoja.” Katika masiku ya kuzindua rasmi chama cha Jubilee hapo kasarani, Kiongozi wa chama  Bwana Kenyatta alisema,” Chama tunacho kizudua hapa leo ni kuashiria umoja wetu.”

Hivyo basi yaashiria ya kwamba kuwa hapo nyuma, viongozi wa kisiasa waliamini kuwa umoja ungelipatikana tu kwa kupitia vyama vya kisiasa.

Sawia na hayo, miito hio ya umoja iliwahi kusikika mwakani 2008 wakati taifa llilikuwa limetoka katika majeraha ya vita baada ya uchaguzi mkuu. Kwa kupitia mdahalo wa  maridhiano na matangamano wa Kenya, raisi Kibaki na Raila  Odinga walitia saini makubaliano ya utabikishaji wa mapendekezo ya jopo kazi la uchunguzi wa vita vya baada ya uchaguzi wakitarajia kuwa kufanya hivyo ndio wataleta amani ya kudumu milele.

Umar ibn al Khatatab {r.a}, Khalifah wapili wa waisilamu alisema,’’ Hapana uisilamu bila umoja, na  hapana umoja bila uwongozi na hapana uwongozi ila kuthwii,” Kutokana na kauli hii yaeleweka kwamba kuwepo kwa taifa lelote lile hutegemea umoja wa watu kwa taifa hilo. Zaidi ya hivyo, ili taifa liweza kupata matunda ya mafanikio, halina budi liwe na umoja baina ya umma wake. Kwa hivyo ni jambo lisilo staajabisha kuona ya kwamba mataifa yote yata ngangana kuhakikisha umoja kati ya umma zao umepatikana ndani yao.

Tangu nchi za Afrika zipate uhuru, zimekuwa zikitambua ya kwamba umoja kati ya makabila yao wapatikana ima kwa kupitia vyama vya kisiasa au midahalo ya amani. Kwa kweli mtazamo huu umepelekea kuona baadhi ya nchi zingine zikibuni chama kimoja cha kisiasa, au kuunganisha vyama vyingi vya kisiasa na au kubuni midahalo ya umoja na amani ambayo huishia kwa kusainia mikataba ya amani na pia kuleta marekebisho ya katiba. Kutokana na msingi huu muovu wa kuleta watu pamoja, imekuwa ni jambo la kimaumbile kuona mara kwa mara nchi kuwa na mfazaiko na kutishiwa kuangamia. Mito ya kujitenga, vita baada ya kura za uchaguzi, chuki za kikabila, zote hizi ni mifano moja wapo inayoonyesha jinsi gani watu wa Afrika hawana umoja. Kwa kweli ni kwa ihsani ya wakoloni wa magharibi ndio twapata kuona nchi za Afrika zina umoja ndani mwao.

Ni jambo la hakika ya kwamba vyama vya kisiasa si vyombo vya kufungamanisha watu katika nchi. Lazima itabulike kuwa kazi ya vyama vya kisiasa ni ku kampeni na kusajili wagombezi ili waweze kushikilia afisi za usimamizi na pia wawe ni wenye kuhisabu serikali kuu.

Vile vile, michakato na midahalo kama vile BBI haijakuwa ni vyombo halisi vya kuleta utangamano wa kudumu. Hi ni kwasababu msingi iliyo simamo kwayo huwa ni maslahi ya mtu binafsi hivyo basi pindi maslahi hayo ni yenye kukosekana nao umoja pia ni wenye kukosekana. Kwa kuwa BBI ilibuniwa kwa ihsani ya viongozi wawili, basi litakuwa ni jambo la kimaumbile kuona ya kwamba BBI itapingwa vikali na kugawanya watu zaidi maadamu maslahi ya watu wengine mbali na ya wawili hao waasis hayakutiliwa maanani. Na hili lilikuwa wazi pindi siku ilipokuwa yazinduliwa rasmi repoti ya BBI. Bwana Senator Murkomen alisikika akisema  siku hio, “ Kwa njia Bwana Mohamed anavyoendesha shughuli hii ina shinda malengo halisi ya mjumuiko huu. Ni wazi kuwa wale ambao waoyesha wana maono tofauti hawaja alikwa kuja kuzungumza.”

Hili basi la tibitisha ya kwamba BBI itagawanya watu zaidi badala ya kuwaugamanisha. Alipokuwa ni mwenye kuzuru huduma ya kanisa hapo Full Gospel Gatunduri Church Embu, William Ruto alisema kuwa BBI itasimamishwa iwapo itaendelea kuwagawa waKenya.” Hii stori twasikia eti hakuna mtu anaweza simamisha rege, ikiwa rege ni ile tunaona ukabila unao pigiwa debe katika mikutano ya BBI, Kukagua makabila, chuki na kugonganisha jamii moja kwa nyengine, ikiwa hio ndio rege wanaiongelea, rafiki zangu, rege itasima,”

Kwa kutamatisha, mchakato wa BBI kamwe hautaweza kuleta umoja wa kudumu ila uhasama. Jambo ambalo hakika litawezesha umoja upatikane ni kuwepo kwa mfumo ambao ndani yake kunapatikana nidhamu. Pindi watu watakapo amini nakutabikisha mfumo inatarajiwa kwao wao kuwa na fikra, hisia na nidhamu mmoja. Ule uwepo wa watu kuwa na hisia, fikra na nidhamu mmoja hujaalia watu wakawa ni wa moja nyakati zozote maishani

Ili ndoto hii iweze kupatikana, ndoto ya kuwezesha taifa liwe taifa la kimfumo haina budi kufanyiwa kazi. Kwa minajili ya kuwepo kwa umoja katika taifa, viongozi wa kisiasa lazima wazidishe kutilia nguvu miito ya kubandua nchi zao kuwa nchi za kiutumwa zinazo zunguka madola makuu ya kimfumo. Sauti za kikweli hizi ndio hatimae zitapelekea taifa kuwa la kimfumo na wananchi kuwa na umoja daima.

ABU LEILA,

March 1, 2020.