Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ijumaa tarehe 13 April 2018, Hizb ut-Tahrir Kenya iliongoza Ummah kwenye ukumbusho wa tukio kubwa lililoacha Ummah wa Kiislamu kuwa yatima asokuwa na mlezi nalo ni kuvunjwa kwa Khilafah yapata miaka 97 sasa. Ukumbusho huu ulifanywa katika maandamano baridi baada ya swala ya Ijumaa katika Miji ya Nairobi, Mombasa, Kwale na Kilifi. Kauli mbiu kwenye maandamano hayo ilikuwa: MuokoeniJanat_OkoeniGhouta_SimamisheniKhilafah
Katika maandamano hayo, Hizb imewakumbusha Waislamu kuwa uadui wa serikali ya Urusi dhidi ya walinganizi wa Khilafah sio mgeni kwani ilishirikiana pamoja na Uingereza katika kuiangusha Khilafah mwaka 1924. Kuangushwa kwake ndio chanzo cha madhila na masaibu yanayowakumba Waislamu kote duniani kwani Ummah ilipoteza ngao yake halisi; Khalifah aliyesifiwa na Mtume Muhammad (saw):
(إنما الإمام جنة يقاتل من ورائه ويتقى به)
Hakika ya Kiongozi ni ngao watu hupigana nyuma yake na kwake hupata hifadhi.
[Muslim]
Maandamano haya yalikuwa sehemu tu katika ya kampeni ya kiulimwengu iliyoanzishwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir ndani ya mwezi huu mtukufu wa Rajab. Kampeni hii imelenga kukumbusha na kuwataka Waislamu wachangamke katika kutekeleza faradhi miongoni mwa faradhi kubwa bali mama wa faradhi zote nayo kuisimamisha tena Khilafah. Ukumbusho huu unakuja ikiwa bado Waislamu wapo kwenye minyororo ya wakoloni makafiri ambao wanaeneza ufisadi katika ardhi na kuuwa mimea na wanyama .Basi huu ni ukumbusho utakao wafaa wenye kukumbushwa nao wataelewa kuwa kusimamisha Khilafah ndio suluhisho la kweli litakalo tatua matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Na bila shaka siku ya kusimama kwake ndio Waumini watafurahi kwa nusra ya Mwenyezi Mungu (swt).
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
KUMB: 08 / 1439 H
Ijumaa, 26 Rajab 1439 H/
13/04/2018 M
Simu: +254 707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke