Katika Makumbusho ya Miaka Tisini na Tisa ya Kuvunjwa kwa Khilafah, Isimamisheni Kabla ya Kutimia Miaka 100
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Miaka tisini na tisa … Huu hapa mwaka mwingine umepita katika maisha yetu, na kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah imerudi kutuzuru tena, kutukumbusha kuwa Ummah wa Kiislamu umechelewa kutoa ahadi ya utiifu kwa Imamu kwa miaka yote hiyo! Kwa hiyo, je, itasimamishwa leo kabla ya maadhimisho ya mwaka wa 100?!
Miaka tisini na tisa … Na suala la kupoteza “utukufu na hadhi” miongoni mwa mataifa ni suala ambalo damu huchemka katika mishipa ya Ummah wa Kiislamu … ambapo watu wake wametoka katika mapinduzi ya kihistoria yasio ya kawaida, na zile zilizozingatiwa kuwa “tawala zisizo yumbishwa” zilipinduliwa. Kwa hiyo, je, itasimamishwa leo kabla ya maadhimisho ya mwaka wa 100?!
Miaka tisini na tisa … Na kafiri mkoloni Mmagharibi aidhinisha mipango, asimamia njama, na kutafuta kuzibadilisha upya njia zake na namna zake za kuuweka Ummah wa Kiislamu katika hali ya kutawanyika bila ya serikali na dhaifu bila nguvu. Kwa hiyo, je, itasimamishwa leo kabla ya maadhimisho ya mwaka wa 100?!
Bado tunaiona Khilafah ikitajwa wakati wote katika mizunguko, miongoni mwa watu, katika wanaoichukia, kati ya familia, katika vipindi na makala. Khilafah imekuwa maoni ya umma miongoni mwa Waislamu, wote ambao wameshangazwa kwa jinsi itakavyorudi! Kila mmoja anafahamu utukufu wake wakati itakaporudi, na kila mmoja anajua kuwa wakati itakaporudi itazindua nguvu za Ummah na kuregesha kutekeleza jukumu lake katika ulimwengu, kuwa muokozi wa ulimwengu huu kutoka katika hali iliyofikia. Vipi hatuwezi kutambua utukufu wa Khilafah, kwani ni serikali ambayo idadi ya watu wake imezidi bilioni moja na nusu wanaotamani kurudi kwake karibuni. Waislamu bilioni moja na nusu, wanaume na wanawake wanaozingatia kila mmoja wao kama kaka na dada kutoka familia moja inayofunika ulimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ)
“Hakika Waumini ni ndugu” [Al-Hujurat: 10]
Utukufu wa Ummah wa Kiislamu umefungika kwa masharti matatu kwa utukufu wa mataifa, ambayo ni, “Ummah, Itikadi na Dola.” Ama kuhusu Ummah, upo, umejaa nguvu na imara, ambapo unajaza viwanja vya mji kwa vijana wa kiume na wa kike. Ama kuhusu Itikadi, pia ipo. Ambapo ufahamu wa maelezo yake na utafiti wa matumizi yake umefanywa na wale ambao wanaujali sana Uislamu, wakiongozwa na Hizb ut Tahrir, ambao wameandaa kurudi kwa Khilafah kama “dola ya Khilafah iliyoendelea” na wameandaa sheria halali ya nidhamu ya kisiasa iliyopitishwa na vyanzo vya sheria za Kiislamu.
Ama kuhusu Dola, inajumuisha nguvu. Kwani dola huchukua nguvu zilizotawanyika za watu na kuwakusanya wao katika kiganja kimoja, hupanga uwezo wao uliotawanyika, kuwafanya wao kuwa nguvu yenye natija. Kwa Ummah wa Kiislamu, dola ni kama kinywaji cha kushangaza na dawa ya ajabu. Kwa kuwepo kwa dola ya Kiislamu, nguvu za Ummah zitapangiliwa, na italipua nguvu zake, na kwa kukosekana kwake huanguka na rasIlimali zake kuporwa. Ndio maana lazima tutambue kuwa kuungana kwa Ummah wa Kiislamu na dola yake itakuwa ni tukio sawia na dhoruba ya nyuklia katika historia ya binadamu. Itayafundisha mataifa jinsi ya kushughulikia mlipuko wa magonjwa na maradhi, na itawakomesha wanaoabudu ng’ombe wa India kutokana kufikiria kuhusu minong’ono ya shetani, na itawafanya wao kuonja matokeo ya vitendo vyao.
Na kwa hili, kwa jina la Mwenyezi Mungu na juu ya baraka za Mwenyezi Mungu, katika ukumbusho wa 99 wa kuvunjwa kwa Khilafah, tunazindua kampeni pana ya kiulimwengu ambayo tunawalingania Ummah wa Kiislamu na watu wake, wanachuoni, majeshi, na watu wenye nguvu kuharakisha kusimamishwa kwa Khilafah kabla hatujafika mwaka wa mia moja! Ili tupate radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na ili historia iweze kurekodi kuwa sisi ni Ummah muhimu ambao uliweza kurudi ulimwenguni chini ya miaka mia moja.
Katika tukio hili, kutakuwa na hotuba yenye maana kubwa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, katika tukio la ukumbusho wa 99 wa kuvunjwa kwa dola ya Khilafah katika tangazo maalumu kwenye kituo cha Runinga ya Al-Waqiyah baada ya Maghrib, Jumapili, ambayo itakuwa ni usiku wa Jumatatu, 28 mwezi mtukufu wa Rajab 1441 H sawia na 23/3/2020 M.
Imepokewa kutoka kwa Ubay ibn Ka’b, radhi za Mwenyezi mungu ziwe naye, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na familia yake, alisema
«بَشِّرْ أُمَّتِي بِالسَّنَاءِ وَالرِّفْعَةِ وَالتَّمْكِينِ فِي الْبِلَادِ…»
“Wabashirie Ummah wangu ushindi, umaarufu na umakinifu katika ardhi…”
Mha. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
#TurudisheniKhilafah
أقيموا_الخلافة#
#YenidenHilafet