Khilafah: Suluhisho kwa Majanga ya Chakula Ulimwenguni

Mnamo Jumatano, 5 Mei 2021 muungano wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, mashirika ya kiserikali na yasiokuwa ya kiserikali yanayofanyakazi kutatua majanga ya chakula yalitoa Ripoti ya 2021 ya Kiulimwengu kuhusu Majanga ya Chakula (GRFC 2021). Ripoti inasema kwamba nchi/maeneo 55 yanayokadiriwa kuwa na jumla ya watu milioni 155 yameathirika na ukosefu wa usalama wa chakula. Kwa kuongezea, ripoti imetambua kuzidi kwa idadi ya watu milioni 20 kutoka mwaka uliopita (2019 ikiwa na watu milioni 135). (The EasternAfrica)

Ripoti hii mpya ya 2021 inaweka bayana idadi kubwa tangu miaka mitano ya kuwepo kwake. Ripoti inataja mizozo/ukosefu wa usalama (watu milioni 99.1 katika nchi 23), mishtuko ya kiuchumi (watu milioni 40.5 katika nchi 17) na hali mbaya ya hewa (watu milioni 15.7 katika nchi 15) ndio sababu msingi zenye kusababisha ukosefu mkubwa wa chakula mnamo 2020. Kwa kuwa maalum, asilimia 66 ya watu milioni 155 wanaopatikana katika Janga au ubaya zaidi walikuwa ni kutoka nchi/maeneo 10 – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (milioni 21.8), Yemen (milioni 13.5), Afghanistan (milioni 13.2), Jamhuri ya Uarabu ya Syria (milioni 12.4), Sudan (milioni 9.6), Nigeria kaskazini (milioni 9.2), Ethiopia (milioni 8.6), Sudan Kusini (milioni 6.5), Zimbabwe (milioni 4.3) na Haiti (milioni 4.1)! Fauka ya hayo, watoto milioni 75.2 walio chini ya miaka 5 ndani ya nchi/maeneo hayo yaliyo na janga la chakula wamedumaa (ukuaji wao umezorota pakubwa)!

Takwimu hizo zinathibitisha uhalisia wa kutamausha wenye kuwakabili wanadamu wanaotaabika chini ya uongozi uliofeli wa kisekula wa kirasilimali. Haishangazi kuwa waasisi wa ule unaoitwa Muungano wa Kiulimwengu Dhidi ya Majanga ya Chakula ndio ambao wanachochea mizozo na majanga ya kiuchumi duniani kote kutokana na kiu chao kisichoisha cha uporaji wa rasilimali za dunia huku wakiwaacha wengi wakihangaika. Katika jopo lao wanaongozwa na taifa fisadi na katili duniani, Amerika na washirika wake. Mamlaka ya kisekula ya kirasilimali yanayosimamiwa na utawala wa Kiamerika unaendesha mambo ya kiulimwengu wanavyotaka kwa kutumia njama na sera za kikoloni zinazo watia vitanzi na minyororo wanadamu na kuwasababishia maisha ya dhiki.

Ili kutoa mifano michache, kitaifa Amerika imeshindwa waziwazi kusitisha mgawanyiko wa kirangi ambao umepelekea jamii ya watu weusi kupata uharibifu mkubwa wa kudumu kijamii na kiuchumi. Ng’ambo kupitia watawala wake vibaraka imo katika vita vya muda mrefu dhidi ya watawala vibaraka wa Ulaya /Uingereza nchini Yemen, Libya na Somalia ili kupata ubwana wa kieneo. Nchini Syria, Afghanistan na Iraq imo kuzinusuru tawala hizo ‘zilizofeli kupindukia katika majaribio ya kidemokrasia’ na ambazo zimepoteza uhalali kutoka kwa watu. Katika mchakato wao huo wa vita hadaifu watu wanauliwa na hususan Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ‘Ugaidi na Misimamo Mikali.’

Natija yake ni kuwa kuna hamaki kiulimwengu za kutafuta mbadala wa mamlaka ya kisekula ya kirasilimali ambayo yanaendelea kusababisha maangamivu katika kila nyanja ya maisha. Majanga ya chakula ni sehemu tu ya tatizo kuhusiana na uharibifu mkubwa kutoka kwa udhibiti wa sumu unaowalipa wanadamu kwa kujisalimisha kwao katika kujifunga na mfumo wake! Mbadala uliowahi kujaribiwa na wenye kustahiki ni Khilafah. Khilafah ni nidhamu ya Kiislamu ya kiutawala ambayo ipo kwa ajili ya kuwalingania wanadamu katika kheri ya Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Nidhamu ambayo inahakikisha wanadamu wanabakia kama watumwa kwa Muumba wao, Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kujisalimisha kwao katika utabikishaji na utekelezaji wa nidhamu za kiwahyi juu yao. Nidhamu ambazo zinalenga kuwaondolea uzito katika maisha yao.

Mwanamume Muislamu aliyezama katika kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt) kama Khalifah atajizatiti kuweka sera ambazo zitaleta amani, utulivu na ustawi. Kama ilivyokuwa katika Khilafah ya pili ya Umar (ra) ambapo alihakikisha kwamba wanaume, wanawake na watoto wako salama dhidi ya njama bali hata alihofia asije punda akapata jeraha kutokana na barabara kutoshughulikiwa chini ya uongozi wake! Khilafah itakuwa makini kuwapa raia wake mahitaji msingi kama unavyotaka Uislamu. Mtume (saw) alisema:  «لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ فِي سِوَى هَذِهِ الْخِصَالِ بَيْتٌ يَسْكُنُهُ وَثَوْبٌ يُوَارِي عَوْرَتَهُ وَجِلْفُ الْخُبْزِ وَالْمَاءِ» “Mwana wa Adamu hana haki bora zaidi ya kuwa na nyumba ambamo ataishi, kipande cha nguo ambacho ataweza kuhifadhi uchi wake na kipande cha mkate na maji.” [Tirmidhi]

Kwa kuongezea, Rasulullah (saw) alisema: «مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافًى فِي جَسَدِهِ آمِنًا فِي سِرْبِهِ عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»Yeyote atakayeamka akiwa salama miongoni mwa watu wake, akiwa na afya (kimwili) na akiwa na chakula cha siku hiyo, ni sawa na kama ambaye dunia yote imekusanywa mbele yake.” [Tirmidhi na Ibn Majah]. Kwa hiyo sio fadhila kwa dola ya Khilafah kutoa mahitaji msingi (chakula, mavazi na makaazi) na mahitaji ya kijamii (usalama, elimu na matibabu) kwa raia wake. Badala yake ni moja katika faradhi zake ambazo lazima itimize kwa njia iliyo bora iwezekanavyo. Na kunapotokea utelekezaji aina yoyote basi Imam / Khalifah atahesabiwa hapa Duniani na Akhira.

Nabii (saw) alisema: «أَلاَ كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ عَلَيْهِمْ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ» “Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja wenu atahesabiwa kwa kundi lake (analolichunga).  Amir (mtawala/khalifah) ambaye yuko juu ya watu ni mchungaji na atahesabiwa kwa kundi lake…” [Abu Dawud] Imesimuliwa kutoka kwa Abu Dharr (ra) aliyesema: عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلاَ تَسْتَعْمِلُنِي؟ قَالَ: فَضَرَبَ بِيَدِهِ عَلَى مَنْكِبِي ثُمَّ قَالَ:‏ «يَا أَبَا ذَرٍّ إِنَّكَ ضَعِيفٌ وَإِنَّهَا أَمَانَةٌ وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْىٌ وَنَدَامَةٌ إِلاَّ مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا» “Nilimwambia Mtume (saw): Nabii wa Mwenyezi Mungu, kwani hunichagui kufanyakazi katika afisi za umma? Akanipiga mabega yangu kwa mkono wake na kusema: Abu Dharr, wewe ni dhaifu na mamlaka ni amana. Na Siku ya Kiyama itakuwa ni sababu ya kufedheheka na kutubia isipokuwa kwa yule anayetekeleza wajibu wake na (kwa uzuri) akatenda majukumu yake.” [Muslim]

Kwa mujibu wa dalili hizo ni wazi kabisa kwamba nidhamu ya Khilafah haitojishughulisha na sera duni zinazojumuisha na sio tu za chakula. Kama inavyoshuhudiwa hivi sasa katika nidhamu ya kimakosa ya kisekula ya kirasilimali; ambapo asasi za dola zinachochea mizozo na mishtuko ya kiuchumi miongoni mwa maovu mengine. Na kuwasababishia watu kutoweza kushiriki shughuli makini za kilimo ili kuboresha maisha yao kupitia uzalishaji chakula cha kutosheleza. Kwa kuwa wapo mbioni kukimbia mizozo ya kudumu na sera mbovu za kifedha na ardhi ambazo zinawatoa thamani na kuwapatiliza wengi katika sekta ya kilimo ambayo imesalimishwa kwa makampuni machache yanayo weka sheria na masharti!

InshaAllah, hivi karibuni Khilafah itakayosimamishwa tena kwa njia ya Utume itatabikisha na kutekeleza sera nyingi ikijumuisha ile ya kilimo ili kuifanya kuwa dola salama na yenye kujiendeleza yenyewe kichakula duniani kote. Ni matumaini yetu kwamba wanadamu watajifunga na mradi wa Khilafah unaoongozwa na Hizb ut Tahrir ili kuwakomboa kutoka katika makucha yenye sumu ya udhibiti wa kikoloni wa Kimagharibi. Hatimaye, kuchukua hatua za kidharura zinazohusisha kufanyakazi na kuwa na msimamo ndani ya Hizb ut Tahrir kwa kutafuta Nussrah kutoka kwa watu wa nguvu (majeshi ya Waislamu) ili kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. ﴿وَيَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ “Na siku hiyo waumini watafurahi.” [30. Ar-Rum: 4]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

                                  Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir