Kongamano baina ya Afrika na Urusi: Viongozi wa Kiafrika Wanaiuza Afrika kwa Madalali wa Kirasilimali
Habari:
Viongozi wa Serikali zaidi ya 40 wa nchi za Afrika walihudhuria Kongamano la kwanza baina ya Afrika na Urusi katika mji wa Sochi. Kongamano hilo la siku mbili 24 na 25 Oktoba 2019 liliandaliwa kwa pamoja na Rais Vladmin Putin na mwenzake rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi uliangazia zaidi masuala ya kibiashara baina ya Urusi na Afrika likiwemo pia suala la usalama. Kwenye mahojiano ya awali na shirika la habari la serikali la TASS siku ya Jumatatu, 21 Oktoba 2019, rais Putin alisema: “Mkutano huu wa siku mbili ni hatua ya kufufua tena mahusiano yake ya vita baridi ampapo mataifa ya Kiafrika yalijiunga na utawala wa Moscow kwenye vita vya kimfumo na Marekani hii ni kabla ya kusambaratika kwa muungano wa kisovieti ni tukio la kipekee na hatua msingi”
Maoni:
Mnamo Machi, 2014 Muungano wa Ulaya na mataifa kama Marekani, Canada, Australia, Japani, Uswizi, New Zealand, Iceland na mengine yalianza kuiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi kutokana na hatua yake ya kuiteka Crimea. Vikwazo hivyo viliathiri uchumi wa Urusi; taifa ambalo ni moja wapo ya mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani. Kongamano hili bila shaka ni miongoni mwa juhudi zake za kuokoa uchumi wake ambao umekua kwa mwaka huu kwa asilimia 1 tu pekee kutoka asilimia 2.3 katika mwaka jana 2018. Mataifa makubwa yanapora rasilimali za Afrika kupitia kile kinachoitwa ‘mikao ya maendeleo ya biashara’ kama vile Jukwaa la Biashara baina ya Amerika na Afrika, Jukwaa la Ushirikiano baina ya Uchina na Afrika, Japan, Kongamano la Kimataifa la Tokyo la Maendeleo ya Afrika (TICAD) n.k. Licha ya kwamba Urusi inasafirisha bidhaa za vyakula kwa thamani ya dolari bilioni 25 na silaha za thamani ya dolari bilioni 1 kuingia Afrika, inakuwa ni sawa na one baharini ikilinganishwa na Uchina ambayo katika kubadilishana kwake bidhaa na Afrika imetia faida ya dolari bilioni 204! Kwa upande mwingine, biashara ya Urusi na Afrika iko kwa kiwango cha dolari bilioni 26! Hivyo basi, Moscow inalenga kupatiliza fursa ya kongamano hilo ili kuweka mpango wake wa kushindana na Amerika, Muungano wa Ulaya na Uchina kama washirika wa kimikakati ndani ya bara lililo na utajiri wa rasilimali.
Ni wazi sasa utawala wa Putin unaumezea mate utajiri wa Afrika na una matumaini ya kuongeza maradufu biashara yake. Kwa mujibu wa shirika la Habari la Serikali ni kwamba tayari kwenye mkutano huo Urusi na baadhi ya tawala za Kiafrika zimetia saini mikataba ya miradi kadhaa kama vile teknolojia ya nuklia, uchimbaji madini na viwanda. Kwa ujumla Urusi imetenga kitita cha dolari bilioni 190 za kuwekeza katika miundombinu inayotarajiwa kutoa faida ya dolari bilioni 7.
Moscow inawekeza katika utengezaji wa zana za kivita ikiwemo mradi wa nuklia ambao umekua ukionekana kuwa tishio dhidi ya Marekani. Hatua yake ya kuiuzia silaha Afrika ni jaribio lake la kuathiri siasa za Afrika ili iweze kupata baadhi ya vibaraka wake watakaofanikisha tamaa zake za kuipora Afrika. Hata hivyo kwa kuwa nchi nyingi barani Afrika bali karibu zote zimo katika ushawishi wa Marekani na Ulaya, jaribio lake hilo sio rahisi kufaulu hasa tukizingatia kuwa yuko nyuma kiuweledi wa kisiasa ukilinganisha na Marekani na Ulaya. Urusi ina kambi ya kijeshi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi inayotajwa kuwa na umuhimu mkubwa wa kistratejia na eneo salama baina ya Waislamu wa kaskazini na Wakristo wa kusini. Rwanda nchi ambayo inatajwa kuwa na mahusiano ya karibu na Urusi tayari baraza lake la mawaziri limeidhinisha kuasisiwa kwa kituo cha nuklia kufikia 2024.
Warasilimali kwa upande mmoja wanaupora utajiri wa Afrika kwa kisingizio cha kudumisha usalama, kuhifadhi na kulinda mazingira ya Afrika na kufutilia mbali madeni. Kwa upande mwingine viongozi wa Afrika chini ya bendera ya mipango ya maendeleo; viongozi wa Afrika wamekuwa madalali wakuiuza Afrika kwa madalali warasilimali wakubwa kwa kupewa mabaki kidogo ambayo yanaishilia kusababisha madhara zaidi kuliko mazuri kwa nchi zao na raia wao. Nchini Kenya kwa mfano, mradi wa SGR amabo ulidhaminiwa kwa mkopo wa bilioni Ksh324 umepelekea kufutwa kazi kwa asilimia 60 ya wafanyikazi katika Vituo vya Usafirishaji Makasha (CFS) kufuatia agizo la serikali la kusafirisha makasha yote yaliyowasili Mombasa kwenda Nairobi kupitia SGR badala ya barabara!
Afrika lazima itambue kwamba Urusi, Uchina, Marekani na Ulaya yote ni mataifa ya kibepari yanayong’ang’ania maslahi yake barani. Hivyo mikataba ya kibiashara kwa bara la Afrika si lolote ila ni kinyang’anyiro juu ya rasilimali zake. Mataifa hayo hutayarisha mazingira mwafaka ndani ya Afrika kupitia kuzunguka na kutambua utajri ulioko kwenye nchi kavu na bahari huku wakihonga viongozi wa Kiafrika, kuzidisha matumizi yao ya kijeshi barani kwa kile wakiitacho ‘ujumbe wa kuweka Amani na kufanya ziara kadhaa za kiarais kwa nchi hizo kwa lengo tu la kupata utiifu wa kisiasa utakaowawezesha kuchukua mafuta na gesi. Makampuni makubwa ya kibepari pamoja na serikali za Kiafrika wao wote wanasoma kutoka katika ukurasa mmoja wa Urasilimali na hivyo basi utajiri unaozalikana na mauzo ya nje huzunguka tu miongoni mwao huku wakimuacha mlalahoi kwenye umasikini. Serikali pekee itakayolinda kikweli utajiri wa bara la Afrika lililobarikiwa ni Khilafah kupitia kukata kabisa ushirikiano na mataifa ya kirasilimali hivyo kuweza kuondosha taswira za kutamausha za bara hili za njaa, maradhi na kutojua kusoma na kuzibadilisha kuwa sura za siha, afya na maendeleo.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya