Mkurupuko wa Virusi vya Corona: Janga jengine linafichua aibu za Urasimali na tawala zake.

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Huku ulimwengu ukiendelea kukumbwa na janga la virusi vya Corona,Kenya kama serikali nyengine duniani inaonekana kujikakamua na majaribio ya kukabiliana na janga hili. Visa saba vya maambukizi ya virusi vya Corona visharipotiwa japo hadi sasa hakuna kisa chochote cha kufariki dunia kwa muathiriwa yoyote.

Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kuangazia yafuatayo:-

1-Mkurupuko wa maradhi ya Covid 19 unapata uangaziaji mkubwa sana katika vyombo vikuu vya habari duniani huku habari zinazoripotiwa za janga hili zikionekena kukuza zaidi hofu na wasiwasi.Hatakama ni kweli kuwa dunia inatikiswa na janga la Virusi vya Corona lakini ni muhimu tusiweze kusahaulishwa na mgogoro wa miaka takriban tisa sasa nchini Syria ambao ndio janga kuu la kibinadamu lililozimisha wakaazi takriban laki saba kuyahama makaazi yao. Utawala wa Syria ukisaidiwa na Marekani na Russia pamoja na mawakala wao wanatekeleza mauaji ambayo kwa sasa yamefanywa sio habari tena kwa vyombo vya habari!

Kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba hivyo tunanasihi jamii kuchukua tahadhari za mapema kama vile kuosha mikono na kujiepusha kuzuru maeneo ambayo kuna maambukizi ya virusi vya Corona. Uislamu umehimiza sana hatua ya kuchukua tahadhari huku ukifahamisha kwamba Maradhi ya kuambukiza ni sehemu ya mitihani ya MwenyeziMungu kuwaonja waja wake ili iwe ni rehma kwa waliowema na adhabu kwa waja wake awatakao Allah (Swt).

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا أَنَّهَا «سَأَلَتْ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الطَّاعُونِ، فَأَخْبَرَهَا أَنَّهُ كَانَ عَذَابًا يَبْعَثُهُ اللهُ تَعَالَى عَلَى مَنْ يشَاءُ، فَجَعَلَهُ اللهُ تَعَالَى رَحْمَةً لِلْمُؤْمِنينَ، فَلَيْسَ مِنْ عَبْدٍ يَقَعُ فِي الطَّاعُونِ، فَيَمْكُثُ فِي بَلَدِهِ صَابرًا مُحْتَسِبًا يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا يُصِيبُهُ إِلَّا مَا كَتَبَ اللهُ لَهُ إِلَّا كَانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ الشَّهِيدِ»

Mama Aisha anasimulia kuwa alimuuliza Mtume SAAW juu ya Tauni, Mtume SAAW akamueleza kuwa ilikuwa ni adhabu anayoipeleka MwenyeziMungu kwa mja amtakaye, na huyafanya Maradhi hayo kuwa ni rehma kwa Waumini. Basi hakuna mja atakayesibiwa na Tauni kisha akakaa ndani ya mji wake akisubiria na kutarajia malipo kwa Mola wake kwa kutambua kwamba hakuna litakalomfika ila lile ambalo MwenyeziMungu amemuandikia ispokuwa ujira wake ni kama wa Shahid. [Bukhari]

 

Ama kuhusu kuchukua  tahadhari Mtume SAAW alisema:

إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلاَ تَدْخُلُوهَا، وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلاَ تَخْرُجُوا مِنْهَا»

Pindi mnaposikia mkurupuko wa maradhi ya tauni (Maradhi ya kuambukiza) msiingie katika mji huo uliokumbwa na maradhi hayo na yanapoingia maradhi hayo katika mji mnaoishi ndani yake basi msitoke

3-Japo inawezekana kusemwa kwamba kwa kuwa virusi hivi vimechipuka kwa mara ya kwanza hivyo shughuli ya kutafuta tiba huenda ikachukua miezi kadhaa, lakini mfumo wa kirasilimali kwa kuwa ni mfumo usojali uhai wa wanadamu huwa si la ajabu janga kama hili kugeuzwa na kuwa mradi wa kujitengezea mapato. Mtazamo wa kina juu ya  viwanda vya  utengezaji madawa vya kirasilimali ni kuwa viwanda hivi vinasukumwa na upande wa kupata faida tu; yaani utengezaji na uuzaji wa chanjo  ni kwa kipimo cha kuzalisha pesa tu. Dawa za wagonjwa walio na maradhi sugu wanazozitumia kila siku huzalisha faida zaidi hata kuliko chanjo ya kuzuia magonjwa hayo.

4- Mporomoko wa uchumi wa mataifa mengi duniani kwa sababu ya maradhi ya Covid 19 hauonyeshi tu hali ya udhaifu wa serikali za kibebari bali pia udhaifu wa mfumo wa kiuchumi ambao wenyewe huzalisha matatizo.Kwa hakina ni sawa sawa na nyumba ya buibui nyumba ilio duni zaidi kuliko zote! Ukweli huu wapaswa ufungue macho wasomi ili wafanye kazi ya kuleta mageuzi ya kimfumo nayo ni kuutupilia mbali mfumo wa kirasilimali na kuuweka mahala pake Uislamu ulio na mfumo imara wa kiuchumi.

 

5-Kwa umma wa Kiislamu pindi unapokabiliana na janga kama hili hakika wao hulikabili kwa kumtegemea zaidi Mwenyezi Mungu sambamba na kuchukua hatua za kujikinga na kutafuta tiba. Kumtegemea MwenyeziMungu (Tawakkul) ni sifa muhimu ya Waislamu inayowafanya wasiogope chochote ila MwenyeziMungu kwani siku zote wanayemtegema ni yule alo hai daima dawamu.

6-Kwa teknolojia za kisasa, serikali ya Khilafah itaweza kubuni mazingira mwafaka ya kuleta ufanisi mkubwa wa utafiti wa madawa. Viwanda vya utengezaji wa madawa vitatengewa pesa viweze kujikita kwenye utafiti wa kina wa kupata chanjo na madawa kutibu magonjwa. Al-Khilafah itaekeza sana katika sekta ya madawa sio kwa kuwa ni fadhila kwa raia wake bali kama jukumu la kiserikali katika kusimamia mahitaji msingi ya umma ambayo hujumuisha usalama na afya. Mtume SAAW amesema katika hadithi iliosimuliwa na Ubaidullah Bin Mihswan Al-Ansaariy:

من أصبح منكم آمنا في سربه، معافى في جسده، عنده قوت يومه، فكأنما حيزت له الدنيا بحذافيرها‏

 Yoyote miongoni mwenu atakayepambaukiwa akiwa na Amani kwa watu wake mwenye afya ya kiwiliwili chake na anacho chakula cha kumtosha siku yake basi kama aliekusanyiwa dunia yote.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya.

REF: 1441/08 AH

ALHAMISI, 24th RAJAB/

19/03/2020CE