Mtazamo wa Haraka kuhusu Kifo cha Jenerali Ogolla

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

(Imetafsiriwa)

Hatimaye Jenerali Francis Ogolla amezikwa. Baada ya kifo na mazishi, kuna haja ya kuzingatia mambo yafuatayo:

Kifo ni janga na somo. Janga kwa maana kwamba watu wenye hadhi ya juu wanapofikwa na kifo cha ghafla hupelekea dukuduku na wasiwasi ambapo wanasiasa hutumia fursa hii katika kufikia malengo yao ya kisiasa hivyo kusababisha hali ya vurugu au maridhiano. Hakika pia ni somo kwa wote, bila kujali wadhifa wako, cheo, hadhi na tabaka kifo ni uhalisia usioepukika.

Kwa kuwa tunaishi katika jamii ya kiliberali-kisekula, kifo huonekana chenyewe kuwa kikomo. Usekula hunamlazimisha mwanadamu kutenganisha maisha ya kidunia na kifo na hivyo kumsukuma kuzama katika ulimwengu wa kimada kama njia pekee ya kutoroka. Kinyume chake, Uislamu unakiona kifo kuwa sio kikomo ndani yake bali kuna maisha baada ya kifo, kwamba tutahesabiwa kwa kila kitendo tulichofanya na tutapelekwa Jannah (Peponi) au Jahannam (Moto wa Jahannam) kulingana na matendo yetu.

Bila kujali maoni tofauti kuhusu kifo cha Jenerali Ogolla, ni muhimu kuweka wazi kuwa kuna ombwe la uaminifu na mpasuko katika uongozi wa kidemokrasia. Demokrasia kimsingi inawanyima tabaka la kisiasa kuaminiwa, haki na uhuru kutokana na ushawishi wa kikoloni na waungaji mkono. Kwa hivyo kifo cha Jenerali Ogolla na kama ilivyo kwa viongozi wengine wa ngazi za juu kitabaki kuwa na dukuduku.

Kwa vile siasa ni sehemu muhimu ya maisha, Uislamu umefasili siasa kuwa ni kitendo cha ibada inayomdhamini yeyote anayeshika nafasi ya kisiasa kubeba jukumu kubwa mbele ya Allah (swt). Kwa hivyo wakati wowote kifo kama hicho kikitokea hakitaanikwa kwa uvumi ambao unaweza kusababisha kukosekana kwa utulivu lakini badala yake kuvipa vyombo vyote vya dola kutoa taarifa wazi juu ya suala hilo.

Uteuzi wa haraka na upesi wa kaimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) umeonyesha wazi umuhimu mkubwa wa uongozi katika jamii yoyote ile. Ni bahati mbaya sana kwa Umma wa Kiislamu kwa miaka mia moja leo bila kiongozi! Haishangazi Waislamu wako hatarini kwa kila aina ya udhalilishwaji, ukandamizwaji, dhulma na mauaji ndani ya nchi za Kiislamu na duniani kote. Mfano hai ukiwa Gaza leo ambapo IDF ya umbile la Kiyahudi inafanya mauaji ya halaiki bila kuadhibiwa. Kwa udharura wake, Umma wa Kiislamu unawajibika kufanya kazi kusimamisha tena chombo cha kisiasa (Khilafah) ambacho kitahakikisha usalama na uadilifu kwa wanadamu wote.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya