Tokea kuvunjwa kwa Khilafah, kubomolewa kwa majumba ya Ibada yemekua ni maafa kwa Waislamu wote.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Kwa hoja ya ukarabati wa Reli ya Nairobi hadi Kisumu,Shirika la  Reli la Kenya lilibomoa msikiti wa Jami’a  na majumba ya wakaazi wa  eneo la Kibos kwenye Jimbo la Kisumu hali iliowaacha familia nyingi bila makao .Msikiti uliojengwa yapata miaka 83 iliopitia, ni moja wapo ya misikiti mikongwe na kituo muhimu cha ibada mjini Kisumu.

Sisi, Hizb ut-Tahrir /Kenya tunakashifu vikali kitendo hiki cha kidhulma na cha kihuni kilichofanywa kinyume na amri ya mahkama iliotaka kutobomelewa msikiti huo na maeneo ya makazi. Ni dhahiri shahiri kwamba serikali imefeli kujenga mahusiano mema na umma hususan Waislamu. Serikali imeshindwa kudhaminia utunzi wa mali na majumba ya Ibada.

Kitendo hiki dhidi ya Uislamu kwa hakika kinachukiza Waislamu na hupelekea hasira za MwenyeziMungu.

 ((وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهاَ

Na ninani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia Misikiti ya MwenyeziMungu kwamba humo lisitajwe jina lake na akajitahidi kuiharibu.

[TMQ 2:114]

Kubomolewa kwa misikiti ni miongoni mwa maafa makubwa kwa umma mzima wa Kiislamu wala sio kwa jamii tu ya Kiislamu ya Kinubi. Hii ni kwakuwa sisi ni umma mmoja na kwamba nafasi ya misikiti kwetu ni kubwa mno kwani ni majumba ya MwenyeziMungu Swt. Kitendo hiki cha kuchukiza kwa hakika kinaonesha wazi uadui dhidi ya Waislamu unaotokamana na uadui wa kimataifa ikizingatiwa kuwa vitendo kama hivi vimekithiri huko china ambao utawala wake unaochukia Uislamu umekua ukivunja misikiti. Tusije tukasahau pia kwamba msikiti mtukufu wa Alqudus bado unakaliwa na mayahudi ambao usiku na mchana huchimba mahandaki ndani yake.

Miaka mia moja ya ukumbusho wa kuvunjwa kwa Khilafah, Waislamu wamekosa mlinzi halisi wa matukufu yao yakiwemo misikiti. Ni miaka mia moja ya vurugu, mashambulizi na ubomoaji. Tukio hili lazima lichachawize waislamu kuzidisha juhudi zao katika kuungana na wale wanaofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah Raashidah chini ya mfumo wa utume katika moja wapo ya nchi za Kiislamu. Ni serikali ya Khilafah ndio ambayo itahifadhi mali ya watu, maisha na nyumba za ibada kwa Waislamu na Wasokuwa Waislamu ulimwengu mzima.

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut Tahrir Kenya