Tunawapongeza kwa Munasaba wa Siku Kuu ya Eidul Fitr

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kutoa salamu za dhati za Eidul-Fitr kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa ujumla.Tunatoa pongezi zetu kwa wabebaji wa Daa’wa wa Ummah wanyofu wanaofanya kazi bila kuchoka kuelekea kusimamisha tena Khilafah Rashidah (Ukhalifa ulioongoka) kwa njia ya Utume. Pia tungependa kutoa salamu  zetu njema kwa Ameer wa Hizb ut Tahrir mwanachuoni mashuhuri Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah na kwa Waislamu wote katika Idi hii yenye baraka.

Umbo la kimauaji la Kiyahudi linalopata uungwaji mkono na Marekani na Ulaya linatekeleza  mauaji huko Gaza. Kwa hiyo, Eid imerejea huku damu za wanawake wetu, watoto na wazee hazijaacha kutiririka kama mito katika mitaa ya Gaza.Wanawake wetu wanapaza sauti zao ambazo zimejaza anga Oh Mu’tasim!! Bila majibu isipokuwa kejeli kutoka kwa wakoloni pamoja na mawakala wao katika Ardhi za Kiislamu!

Suluhisho la Kiislamu juu ya kadhia ya Palestina kama suala lingine lolote linaloshuhudiwa duniani kamwe halitopatikana kwa kufanya ‘mikutano ya dharura’ ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au kauli tupu za Riyadh, Tehran, Islamabad au Istanbul. Tunahitaji Khilafah (Ukhalifa) ambayo itakusukuma na kupeleka  majeshi ya Kiislamu ili kung’oa umbo la Kiyahudi la mauaji linalokomboa sio tu Palestina inayokaliwa kimabavu bali ardhi zote za Waislamu. Khilafah pia itasuluhisha matatizo yote ya kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani kwa suluhisho la kudumu na la kina Bi’idhnillah.

Kullu Aami Wa antum aqrab ilaa lllah

Kullu aamiy wa antum bikheir

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir

Kenya