Uamuzi wa Kuwasamehe Watu Wote Nakith (aliye vunja kiapo), Tarik (aliye ondoka chamani), Mu’akab (aliye adhibiwa)
بسم الله الرحمن الرحيم
(Imetafsiriwa)
Alhamdulilah, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Allah na jamaa zake na maswahaba zake na wanaomfuata yeye,
Nimepokea risala nyingi kutoka kwa baadhi ya ndugu zetu wakiniomba kuzingatia upya (uamuzi) juu ya watu wote walio vunja kiapo (Nakith), walio ondoka chamani, au wanao adhibiwa tangu kuasisiwa kwa chama hiki mnamo 1372 H – 1953 M na kuwasamehe watu wanao stahiki kusamehewa; kwa kuwapa fursa mpya ya kubeba ulinganizi huu, huenda wale watakao pewa fursa hiyo wakaitumia vizuri ili wakakutane na Allah hali ya kuwa ni wasafi na wenye ikhlasi, na yeyote atakaye samehe …
[عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ] “lakini yeyote atakaye samehe na akasuluhisha basi malipo yake yako kwa Allah”
[Ash-Shura: 40].
Ndugu na Dada wapendwa, nimeitafakari kadhi hii kwa makini kwa pembe zote: juu, chini, kushoto na kulia… na kisha Allah (swt) kuniongoza kufikia uamuzi huu:
1- Kuwasamehe wale wote walio vunja kiapo (Nakith), yeyote aliye toka (chamani), au wanao adhibiwa, kwa adhabu ya kudumu au ya muda, ima kwa kupitia toleo la adhabu hiyo au pasi kupitia toleo. Kila mtu huyo anapaswa kunitumia ujumbe kupitia mas’oul wa nchi yake, na kwa kupitia kuidhinishwa na Mu’tamad, akithibitisha yafuatayo:
- Kujutia kwa mtu huyo sababu iliyompelekea uvunjaji kiapo (Nakth), kuondoka, au adhabu hiyo.
- Kuweka ahadi kwa Allah, Al-Aziz Al-Hakim, kwamba hatarudia tena kitendo hicho (sababu hiyo ya juu).
- Ikiwa mtu huyo ana tovuti au ukurasa (wa kijamii), aondoe maalumati yote yanayo kidhuru chama, uongozi wake kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja.
- Mtu huyo asimame usiku (qiyam) kwa muda wa siku tatu, afanye istighfar na kuomba toba, na awe mkweli kwa Allah kuhusiana na kujuta kwake na ahadi yake, na anapaswa kulitaja hili katika ujumbe wake atakao utuma kwangu.
Ikiwa atatekeleza hayo ya juu, basi tutachukulia chochote alicho kifanya kana kwamba hakikufanyika. Na chama kutamkumbatia kwa mara nyengine tena baada ya kumpa kiapo (qasam) kipya… ikiwa mtu huyo alikuwa anapewa adhabu ya muda, baada ya kutekeleza hayo ya juu; tutachukulia chochote alicho kifanya kana kwamba hakikufanyika, na chama kitamkumbatia tena bila ya kumpa kiapo (qasam) kipya.
2- Watu aina tatu hamo katika msamaha huu:
- Yeyote aliye kikhini chama na kuwa kinara wa uasi na upinzani.
- Yeyote aliye ukhini uongozi wa chama, kuuzulia urongo, na kudanganya kwa makusudi.
- Yeyote aliye ikhini mali ya mayatima, kuichukua, kuitumia na kudumu katika hili.
3- Ningependa kuwaambia ndugu zetu ambao hawafurahii uamuzi huu wa msamaha kwa watu hao kwamba: mimi ndiye niliye na mamlaka mikononi mwangu, na ni lazima wanipe utiifu na heshima yao, na kutekeleza uamuzi wangu, maadamu umo ndani ya jukumu la mamlaka yangu na haumuasi Allah. Pia nimefanya Ijtihad kuhusiana na kadhia hii, na namuomba Allah (swt) kuwa si mwenye kukosea.
[وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ]
“…Na mwenye kumuamini Allah huuongoza moyo wake” [At-Taghabun: 11]
Na Allah ndiye msaidizi wetu
Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
2 Rajab Al-Muharam 1439 H Ndugu Yenu
20/3/2018 M Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah