Watoto wa Ghouta, Takwimu za Kimataifa Zazidi Kuongezeka

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Tangu Februari 18, majeshi katili ya serikali ya Syria yakisaidiwa na jeshi la anga la Urusi yameendelea na mashambulizi yao makali dhidi ya eneo la Mashariki mwa Ghouta, baada ya kuligawanya kuwa sehemu tatu za kivita. Natija yake, yaliweza kudhibiti zaidi ya asilimia 80 ya eneo hili lililo karibu na mji mkuu wa Damascus, ambalo tangu mwaka wa 2012 limekuwa ngome kubwa zaidi na muhimu zaidi kwa makundi ya upinzani.

Shirika la kuangalia haki za kibinadamu la Syria liliripoti mashambulizi makali ya angani na makombora kwa mji wa Arbin ulio mashariki mwa Ghouta kupitia ndege za kivita usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita, yaliyo uwa zaidi ya raia 20, wakiwemo watoto 16 na wanawake 4, ikiongezewa na mamia ya raia kujeruhiwa; wote walikuwa ni watoto na wanawake. Hali mbaya ya wale waliofanya makao chini ya mvungu wa shule iligeuka pia kuwa makao kwa mamia wanaokimbia kutokana na kumiminiwa mabomu.

Afisi ya Haki za Kibinadamu ya mjini Arbin pia ilinakili mauaji ya raia 98 mnamo Machi katika kampeni kubwa zaidi ya kijeshi katika miji na vitongoji vilivyoko mashariki mwa Ghouta tangu mwezi uliopita. Mashabulizi kumi ya milipuko ya makombora yalinakiliwa ndani ya muda wa nusu saa!

Tangu kuanza kwa mashambulizi haya ya kijeshi, zaidi ya raia 1450 wameuwawa, wakiwemo takriban watoto 300, kwa mujibu wa shirika la kuangalia haki za kibinadamu la Syria. Shirika la UM linalo shughulikia watoto (UNICEF) lilisema idadi ya vifo vya watoto iliongezeka maradufu mwaka wa 2017 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Kila mwaka tangu kuanza kwa mapinduzi nchini Syria, idadi ya vifo vya watoto imekuwa ikiongezeka, na mashirika haya ya kimataifa yameweka nguvu zao zote katika kusajili vifo hivi kama vifo vya kinyama katika meza za takwimu. Je, idadi itafikia ngapi mwishoni mwa mwaka wa 2018?!

Mji wa Arbin, kama ilivyo miji mengine Mashariki mwa Ghouta, unakabiliwa na hali mbaya huku tukiwaona watawala wa nyumba ya Saud wakifanya mikataba ya kijeshi na kununua silaha kwa mamilioni ya dolari chini ya kisingizio cha kupigana na Mahouthi na kusimama dhidi ya shambulizi la Iran katika eneo hilo. Na tunamuona mtawala wa Uturuki akiapa kupanua operesheni ya “Olive Branch” nchini Syria kufikia maeneo mengine yanayo dhibitiwa na Wakurdi hata katika mpaka wa Iraq.

Tunaomba radhi kwa watu wetu eneo la Ghouta, kwa mateso ya mji wenu ambao haumo ndani ya mipaka ya ramani ambayo Erdogan ameangazia macho yake juu yake ili kuhami usalama wa taifa lake, na tunaomba radhi kwenu enyi watoto wa Ghouta, kwa mtawala wa familia ya Saud kupeleka majeshi yake na kuyapa silaha zenye nguvu zaidi kuongoza vita vya kiwakala kwa ajili ya bwana wake Amerika nchini Yemen.

Enyi Waislamu jueni kwamba hatua za kwanza za ukombozi na kuondoa dhulma zinaanza kwa ukombozi wa ardhi zetu kutokana na watawala hawa. Hapo ndipo biladi zilizo kaliwa zitakapo kombolewa na biladi nyenginezo pia zitakapo kombolewa, kuongezea ukombozi huu nguvu yenu inayo wakilishwa na majeshi yenu ndipo itakapo wahami na kutekeleza dori yao ya kuhami heshima yenu na uhai wa watoto wenu.

Tunayahutubia majeshi hayo na kuyalingania kwa kile kitakacho leta fahari, ushindi na ukombozi kwa Umma wao: wang’oeni watawala hawa kwa kuunga mkono mradi wa dini yenu [kusimamisha Khilafah].

Jueni kwamba utiifu wenu kwa watawala hawa vibaraka katika miradi yao na kunyamazia kwenu kimya kwa yale yanayo tendeka kwa Waislamu nchini Palestina, Syria, Afghanistan, Burma, nk ni dhambi kubwa. Allah (swt) asema:

وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴿

“Na wakiwaomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].

 Kitengo cha Wanawake katika

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  8 Rajab 1439 Na: 1439 AH / 017
M.  Jumatatu, 26 Machi 2018