Utozaji Ushuru Ni sura halisi ya kikatili ya Ubepari

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Wakenya wanatarajiwa kuendelea kuwa na hali ngumu zaidi ya kimaisha kufuatia mapendekezo yaliyoko kwenye mswada wa fedha mwaka 2023. Mswada huo uliowasilishwa na wizara ya fedha unarejesha asilimia 16 ya ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) katika petrol,diseli na mafuta ya taa pia ukipendekeza kodi ya nyumba ya asilimia 3. Takriban bei za bidhaa na huduma zote zimepanda katika miezi ya hivi karibuni ikijumuisha gharama kubwa ya umeme, mafuta na unga wa mahindi.

Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya, tungependa kuangazia yafuatayo:

Mswada huu umefichua hulka mbovu ya wanasiasa ya kuwa na kauli kinzani wasopambika na ukweli, ikizingatiwa kwamba viongozi wakuu wa serikali ya sasa wamekuwa kwenye utawala uliopita waliukataa mswada wa merekebisho wa Ushuru na Kodi 2021Taxes and Levies (Amendment) Bill 2021. Baada ya serikali ya Jubilee kumaliza muhula wake wa kuhudumu, wanasiasa hawahawa waliokuwa wapingaji wakubwa wa mswada ulio na sura kama huu wa sasa wamegeuka na kuwa waungaji mkono wakubwa.

Kwa mtazamo wa harakaharaka,wakenya wakawaida wamekuwa wakitozwa ushuru tokea kipindi cha kabla na baada ya uhuru,licha ya hayo utakuta kwamba sera hii haijatatua kabisa matatizo ya kifedha wala kiuchumi bali yameitumbukiza nchi kwenye lindi lile la majanga ya kiuchumi na kifedha. Ni bayana kwamba utozwaji wa ushuru kama pato kubwa zaidi mfumo wa kiuchumi wa kibepari hauwezi katu kuwa suluhu ya uchumi ambao tayari ni wenye kusuasua.

Ni dhahiri shahiri kwamba tawala za kirasilimali haziwajibiki katika kusimamia mambo na maslahi ya raia wa kawaida. Badili yake wakisema kuinua maisha ya watu, kwao humaaninsha kuwaongezea ushuru ambao hatimaye husababisha bei za bidhaa na huduma kupanda maradufu hivyo kuwaacha raia wao kwenye uchochole. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, serikali za kibepari huegemea zaidi kukopa fedha. Kuchukua mikopo mikubwa ya kifedha hulimbikiziwa raia kwa kutozwa ushuru kama njia ya kufadhili miradi hewa huku pesa zilizokopwa zikifujwa na viongozi mafisi serikalini.

Tunakariri kwamba suluhisho la kiuchumi hupatikana ndani ya mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu ukitekelezwa na serikali yake ya Khilafah ambayo iko mbali kabisa na utozaji ushuru wa kikatili kama vile VAT na ule wala mapato. Mtume Muhammad SAAW alisema:


لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ صَاحِبُ مَكْسٍ

Haingii peponi mtozaji ushuru

Uislamu una mfumo wake wa kipekee wa ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na mapato yatokanayo na mali za umma (kama vile gesi) na uzalishaji wa kilimo (kama vile kharaj), ambayo huingiza mapato bila kukaba koo shughuli za kiuchumi. na maji kama mali ya umma. Si serikali au watu binafsi peke yao wanaoweza kujinyakulia manufaa yake, bali manufaa yake ni kwa ajili ya watu wote. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:


الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّار

Waislamu ni shirika katika kunufaika na mali tatu: Maji, Ardhi za Malisho na Moto

Ibn Majah

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir