Hakutakuwepo na Hadhi, Usalama na Ustawi kwa Wanawake Waislamu Bila ya Kusimamisha Khilafah Rashidah

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Rajab hii inatukumbusha tukio baya mno, miaka 98 iliyopita pale Ummah wa Waislamu ulipopoteza dola yake adhimu, uongozi wake wa Kiislamu, mlinzi na ngao yake –Khilafah. Tokea wakati huo, wanawake Waislamu na familia zao wamejipata katika maangamizi ya mauaji, njaa, uvunjwaji, adhabu, kukosewa heshimu, umasikini wa kupindukia, upweke, ukandamizaji na madhila yasiyovumilika. Tumetoka kutoka kuwa chini ya dola iliyokuwa ina tawaliwa na viongozi wachamungu wakiwahudumia Ummah kwa huruma na kujali mahitaji yao kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt)… kiasi kwamba Ummah upo chini ya viongozi wasiojali lolote kuwahusu, wanaoiba mali zetu kwa kujitajirisha, na kuwaadhibu Waislamu wanaoshikamana kikamilifu na Dini yao. Kutoka kuwa dola kubwa yenye kubeba Jihad kueneza Uislamu ili ikomboe miji, na iliyowafanya maadui zake kutetemeka kwa uoga kila wanapofikiria kumdhuru mwanamke Muislamu…tumekuwa wahanga wa mauaji na uvamizi.

Kutoka katika dola ambayo mwanamke Muislamu alikuwa ni kadhia muhimu katika kujali na usalama na ambapo hadhi yake ilitazamwa kuwa kitu kikubwa kuliko hazina zote za dunia na viongozi wake waliwaunganisha majeshi ili kuhifadhi hadhi yake… tunaishi katika ulimwengu leo ambapo dada zetu Waislamu wanapitia mahangaiko na kufedheheshwa na kubakwa na maadui wa Uislamu pasi na uoga wala kujaIi kuhesabiwa kwa kuwa hakuna jeshi la kuwanusuru; hakuna mlinzi wa hadhi yao. Kutoka katika dola ambayo mwanamke Muislamu alikuwa anapewa ulinzi na kivuli kiasi kwamba hata wasiokuwa Waislamu walitafuta usalama huo kutokana na uadilifu wa utawala wa Kiislamu… tumefikia hali ambayo wanawake Waislamu wanafungwa na kuteswa na maadui wa Uislamu na wametelekezwa na watawala Waislamu au wameachwa wafilie mbali ima baharini au katika kambi chafu mno ambazo hazifai hata wanyama. Tulitoka katika dola iliyokuwa imenawiri kwa utajiri na mahitaji ya watu yakikidhiwa kwa ukamilifu na Khalifah aliweza kubeba chakula kwa mgongo wake ili kumlisha mwanamke Muislamu na watoto wake ambao walikuwa masikini… tumekuwa Ummah unaohangaika kutokana na umasikini wa kupindukia ambapo wanawake Waislamu wanaombaomba mabarabarani na kuwatizama watoto wao wakichakura majaani ili kutafuta chakula ili kukidhi njaa yao au wakifa kutokana na njaa kwa kukosa wakuwapa chakula.

Yote haya ni matokeo ya kukosekana kwa dola ya Khilafah, mlinzi wetu, ngao yetu na mtetezi wa wanawake Waislamu. Hakika miongo tisa mirefu ya ukandamizaji, kukosewa heshima na majanga inatosha kwa kina dada wa Ummah huu wa Waislamu! Hakika ni wakati wa kuweka wazi kwa dunia hii kuhusiana na uadilifu, usalama na ustawi wa Nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah kwa njia ya Utume.

Miongo yote chini ya serikali za kisekula, vyombo vya habari na taasisi zimekuwa zikiionyesha Khilafah kama mkandamizaji na adui wa wanawake. Bali ni muwakilishi wetu, mtetetezi wetu na anayetuma mahitaji yetu. Mtume (saw) alisema, «الإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»“Imamu (Khalifah) ni msimamizi na ana majukumu juu ya anao wasimamia” na pia akasema (saw) 

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»“Hakika Imamu (Khalifah) ni ngao ambayo nyuma yake mnapigana na kujilinda” Kwa hiyo Rajab hii, Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir itaendesha kampeni kwa kichwa, “Khilafah: Mlinzi Wangu! Ngao Yangu!” ambayo tutawasilisha ruwaza ya namna gani Khilafah Rashidah iliyosimama kwa njia ya Utume, iliyo na misingi, sheria na nidhamu za kusuluhisha kivitendo matatizo yetu kama wanawake Waislamu na kuhakikisha ulinzi kwa maisha, mali, heshima na imani yetu –kama ilivyo kwa upana ndani ya vitabu na kielelezo cha katiba vilivyoandaliwa na Hizb ut Tahrir. Tunawalingania mufuatilie na munusuru kampeni hii muhimu na muwe katika nafasi muhimu wakati huu adhimu wa kusimamisha tena serikali ya Khilafah.

 

Kampeni hii inaweza kufuatiliwa hapa:: http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/

Ukurasa wa Facebook: www.facebook.com/WomenandShariah

Link ya Video ya Uzinduzi wa Kampeni: https://youtu.be/lgV1wrLyrY4

 

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

H.  1  Rajab 1440 Na: 1440 H / 022
M.  Ijumaa, 08 Machi 2019