Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kinazindua Kampeni ya Kimataifa: “Khilafah: Yenye Kuhakikisha Hadhi, Usalama na Haki za Kisheria za Wanawake”

بسم الله الرحمن الرحيم

Kufuatia kuanguka kwa Khilafah, maisha ya wanawake wa Kiislamu kote duniani yalijawa na aina zote za unyanyasaji na dhulma, mateso na ufukara chini ya mifumo na tawala zilizotungwa na mwanadamu ambazo zilivunja heshima zao, zimeshindwa kuwapatia usalama wa kimwili na kifedha, na hazikujali chochote katika haki zao za Kisheria walizopewa na Mwenyezi Mungu (swt). Kuna njia ya kutoka katika jinamizi hili hai ambalo mamilioni ya wanawake wa Kiislamu wanakabiliana nalo kote duniani, nayo ni kusimamishwa tena kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo Mtume (saw) aliitaja kuwa ni mchungaji na ngao ya Waislamu. Hata hivyo, leo kuna hofu nyingi, mashaka na maswali kuhusu dola kama hiyo inamaanisha nini kwa wanawake na hali na haki zao. Hofu na mashaka hayo yanatokana na uwongo wa karne nyingi, upotoshaji na mashambulizi ya serikali za kikoloni za Magharibi, waandishi, vyombo vya habari na watetezi wa haki za wanawake kuhusiana na muamala wa  wanawake chini ya utawala wa Kiislamu unaoendelea kuenezwa hadi leo.

Kwa hivyo Rajab hii, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kimeanzisha kampeni ya kimataifa ya kushughulikia hofu, mashaka, na maswali haya kuhusu hali ya wanawake chini ya utawala wa Kiislamu. Kampeni hii inalenga kuwasilisha uelewa wa wazi na dira ya jinsi maisha yatakavyokuwa kihakika kwa wanawake chini ya kivuli cha dola ya Khilafah kuhusiana na haki zao, dori na miamala yao kama inavyothibitishwa na kuonyeshwa na utawala wa Kiislamu zama za nyuma, mbali na uwongo na upotoshaji wa wasomi wa mashariki na wakoloni.

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumatano, 01 Rajab 1443 H sawia na 02 Februari 2022 M

– Ili Kufuatilia kwa Lugha Nyenginezo –

Ar

En

Tr

Ur

Gr

Kalima ya Dkt Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya 101 ya Kuvunjwa Khilafah

Jumatano, 01 Rajab 1443 H sawia na 02 Februari 2022 M

00:00
08:46

– Alama Ishara za Kampeni –

#أقيموا_الخلافة Af Facebook Afg Twetter Afg Inst
#الخلافة_101 Af Facebook Afg Twetter Afg Inst
#ReturnTheKhilafah Af Facebook Afg Twetter Afg Inst

YenidenHilafet#

Af Facebook Afg Twetter Afg Inst

TurudisheniKhilafah#

Af Facebook Afg Twetter Afg Inst
#خلافت_كو_قائم_كرو  Af Facebook  Afg Twetter  Afg Inst

Ili Kusoma Taarifa ya Kitengo cha Wanawake

Ambayo ndani ya ulitangazwa uzinduzi wa kampeni yake ya kimataifa

Katika Kumbukumbu ya 101 ya kuvunjwa Khilafah

Kwa Kichwa: “Khilafah… Dhamana ya Utukufu wa Mwanamke, Usalama Wake na Haki zake za Kisheria”

Jumatano, 01 Rajab 1443 H sawia na 02 Februari 2022 M

Bonyeza Hapa

 

Click to enlarge image IntroFlyer.jpg

Click to open image!

  • Click to enlarge image IntroFlyer.jpg