Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Majeshi vamizi ya umbile la Kiyahudi yalimwita mtoto Malak Sidr (umri wa miaka 8, kutoka katika mji wa Hebron (Al-Khalil) baada ya kuvamia nyumba ya familia yake katikati mwa mji huo na kumpa babake ilani ya kutaka kumhoji mtoto huyo kwa mashtaka ya kuleta usumbufu kwa walowezi hao. Kabla ya tukio hili, mtoto Qays Firas Obaid (umri wa miaka 6) kutoka Al-Aysawiyah [Isawiyah] pia aliitwa kuhojiwa, kwa kisingizio cha kurusha jiwe kuelekea upande wa gari la majeshi hayo vamizi walipokuwa wakivamia mji huo. Hili lilifanyika saa chache kabla ya kuwasili kwa mtoto Mohammed Rabie Alayna ambaye ana umri wa miaka minne na nusu katika kituo cha polisi hao wavamizi jijini Jerusalem baada ya kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa kwa kisingizio hicho hicho.
Mvamizi huyu anaendeleza sera yake ya kikatili juu ya watu wa Ardhi Tukufu – Palestina kupitia mbinu zote, na kuwaita watoto hawa ili kuwahoji kwa kisingizio chochote kile, ni sura nyengine ya msururu wa sera hii ya kihalifu, inayo kiuka ubinadamu na yale yote wanayo dai ya haki za kibinadamu na za watoto. Badala ya kuwazuia walowezi hao wavamizi kutokana na kuwatesa watu wa Ardhi Tukufu – Palestina, wanamuhoji mtoto wa kike kutokana na kuwasumbua wahalifu hawa!!
Kwa mujibu wa takwimu kuna watoto karibu 230 ndani ya magereza ya umbile hilo la Kiyahudi miongoni mwa wafungwa 5700 wa Kipalestina, na mahakama za Kiyahudi ndani ya miaka mitatu iliyopita zimetoa hukmu juu ya watoto ambao wengi wao wanatoka Jerusalem, huku wengi wao wakituhumiwa kurusha mawe. Mnamo Juni 2015, Knesset ili halalisha sheria inayo ongeza muda wa kifungo kwa warushaji mawe wa kipalestina hadi miaka 20. Vilevile, baraza la mawaziri linalo husika na mambo ya kisiasa na usalama limeruhusu upanuzi wa mamlaka yaliyo pewa jeshi la polisi ya kuwapiga risasi warushaji mawe.
Umbile hilo la Kiyahudi linakadiriwa kuwa la pekee ulimwenguni kushtaki watoto katika mahakama za kijeshi licha ya kuwepo kanuni za kisheria zinazo kataza hili. Kwa mfano, makubaliano ya kimataifa ya haki za kibinadamu hususan Makubaliano juu ya Haki za Mtoto (UNCRC) yanasisitiza juu ya umuhimu wa kuwalinda watoto na maisha yao na kupewa fursa ya kukua na kuimarika. Makubaliano haya yamekataza kuwanyima watoto uhuru wao. Lakini, mvamizi huyu amefanya kuwaua na kuwafunga watoto wa Kipalestina kuwa ndio mbinu yake ya kwanza ya hifadhi yake. Hivyo basi ikiwa watoto kama hao, ambao umri wao hauzidi idadi ya vidole vya mkono wa mtu, wanawatia hofu na kutaka kuwakandamiza na kuwatisha ili wasikulie kuwa vijana mashujaa wanaokirimiwa na dini yao na kufanya kazi ya kuwafurusha na kukata mizizi yao, hali itakuwa vipi basi endapo kutakuwepo na jeshi kubwa lililo na Imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu na kujitolea kidete?!!
Enyi Waislamu: Hawa ndio Mayahudi na hili ndilo jeshi lao ambalo watawala watepetevu (Ruwaibidhwaat) daima wanawahadaeni kuamini kuwa hawashindiki… wanaovamia mji ili kuwakamata watoto!! Wanamlenga mtoto kumhoji, ambaye umri wake hauzidi miaka 4, huku watawala wenu ambao mumeridhika nao wakikimbilia kusawazisha uhusiano nao na kufunga mikataba na makongamano tiifu yenye kudhalilisha na kufedhehesha.
Wakati huo huo, hawa ndio watoto wa Palestina ambao wanatenda mithili ya simba kuanzia utotoni mwao. Wanahitaji chombo tu cha kuwaongoza na sio kuwapotosha dira yao kutoka katika mwelekeo wa kuundoa uvamizi na kuirudisha Palestina, na chombo hicho ni jeshi kubwa linalo ongozwa na kiongozi mlinzi litakalo komboa biladi hiyo na watu wake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) na hilo haliko mbali kwa Mwenyezi Mungu (swt).
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 6 Dhu al-Hijjah 1440 | Na: 1440 H / 040 |
M. Jumatano, 07 Agosti 2019 |