Taarifa kwa Vyombo vya Habari
{مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا }
“Miongoni mwa waumini wapo wanaume walio timiza ahadi yao waliyo muahidi Allah. Baadhi wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo” [33:23]
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inaomboleza kifo cha ndugu yetu Kudratullo Sotiboldiev, aliyezaliwa mnamo 1962, baba wa watoto watatu, mwenyeji wa mji wa Margilan, Uzbekistan.
Kuanzia mwanzoni mwa kazi ya Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan, watu waliitikia ulinganizi kwa moyo mkunjufu – watu tofauti tofauti, kutoka matabaka mbali mbali walivutiwa na fikra za Hizb. Ndugu yetu Kudratullo, Allah amrehemu, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuitikia ulinganizi wa Hizb ut Tahrir, alikuwa anatoka katika familia ya wanazuoni wachaji Mungu inayo julikana na wote kwa ucha Mungu wao. Kudratullo alisoma elimu ya lugha ya Kiarabu kutoka kwa Sheikh maarufu Abdul Hokim Vasiev eneo la Asia ya Kati.
Fikra za Hizb ut Tahrir kuhusu kusimamisha tena dola ya Khilafah Rashidah ya pili zilipata nguvu miongoni mwa watu, utawala wa katili Karimov uliwachukia Mashabab wa Hizb ut Tahrir na kuanzisha vita katili dhidi ya Uislamu na Waislamu wa nchi hiyo. Mateso ya halaiki kwa Mashabab yalianza. Hatimaye, mnamo mwaka wa 2000, ndugu Kudratullo alikamatwa na kuhukumiwa miaka 11 gerezani. Baada ya kumaliza kifungo chake, waliendelea kukirefusha kifungo chake, kwa sababu ya msimamo wake usio tingishika dhidi ya adui wa Uislamu na Waislamu usoni mwa utawala wa katili Karimov.
Ndugu yetu, Allah amrehemu, alikuwa katika magereza ya miji ya Navoyi, Zarafshan, Byhara, Tashkent na Almalyk. Hii ilikuwa miaka mirefu ya mitihani katika Imani yake na kukinai kwake, ambayo Kudratullo aliipitia kwa nusra ya Allah (swt). Baada ya kutumikia miaka mingi katika magereza ya katili huyu, mwili wake ulidhoofika na kupata maradhi. Mnamo 2015, Kudratullo aliachiliwa kwa misingi ya kiafya. Miaka ya mwishoni mwa maisha yake, Kudratullo aliugua pakubwa kutokana na maradhi ya maini (cirrhosis).
Mnamo Machi 1, 2018, Kudratullo aliuaga ulimwengu huu na kwenda katika rehma ya Allah (swt). Jamaa waliouosha mwili uliobarikiwa wa ndugu yetu walisema kuwa waliona majeraha mengi mwilini kutokana na mateso aliyopitia katika magereza ya serikali katili ya Karimov. Damu kamwe haikuganda, na mwili ulibakia laini na hauku kukutaa. Masheikh wa eneo hilo walisema kuwa hizi ni miongoni mwa alama za Shahada – japo hatumtakasi yeyote mbele ya Allah.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inatoa rambi rambi zake za dhati kwa familia ya ndugu yetu Kudratullo. Tunamuomba Allah Ta’al kuipa subra na faraja familia yake. Tunamuomba Allah (swt) kutupa Nusrah kwa haraka, tunayalingania majeshi ya Waislamu kusimama na kuutetea Uislamu na Waislamu na kusimamisha Dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Tunamuomba Allah nguvu na uwezo wa kuwakomboa wafungwa wote Waislamu – ndugu zetu na dada zetu kutoka katika magereza ya makatili. Tunaomba adhabu ya haraka kwa makatili na washirika wao wote. Allah ni muweza wa kila kitu.
﴿إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴾
“Hakika sisi ni wa Allah, na hakika kwake Yeye tutaregea.” [2:156]
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 11 Rajab 1439 | Na: 1439 AH / 019 |
M. Alhamisi, 29 Machi 2018 |