بسم الله الرحمن الرحيم
Hayakupatikana kwa Maqureshi Masharti ya Kutafuta Nusra kabla ya Ufunguzi (Fathi)
Kwa: Ghaith Ghaith
(Imetafsiriwa)
Swali:
Assalamu alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuhu,
Sheikh wetu, nina swali lau utaniruhusu, yajulikana kuwa Mtume (saw) alitafuta Nusra kwa makabila, lakini je, Maqureish walikuwa miongoni mwa makabila ambayo Mtume (saw) alitafuta Nusra kwao?
Na Mwenyezi Mungu awalipe kheri.
Jibu:
Waalaykum salam Warahmatullahi Wabarakaatuhu
Utafutaji wa Nusra huwa kwa yule ambaye anaitikia mwito wa Uislamu na kuslimu… Akawa katika watu wa nguvu na hifadhi kwa namna ambayo itamuwezesha kuunusuru Uislamu na kusimamisha Hukmu kwa alichokiteremsha Mwenyezi Mungu. Haya masharti mawili ni wajibu yapatikane kwa yule inayotafutwa Nusra kwake. Ikiwa hakuitikia mwito wa Uislamu akaslimu, au hakuwa miongoni mwa watu wa nguvu na himaya inayoweza kuathiri mageuzi, yeye peke yake na kabila lake au pamoja na wengine, basi hawezi kuwa katika watu wa Nusra… na Maqureysh hayakupatikana kwao hayo kabla ya ufunguzi (Fathi), kwani watu wa nguvu na himaya hawakusilimu katika mji wa Makkah ambao walikuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko, hivyo Mtume (saw) hakutafuta Nusra kwao, bali alikuwa akilingania Uislamu ndani ya Makkah na wale waliosilimu walikuwa ni madhaifu, na baadhi ya wenye nguvu lakini kibinafsi pasi na makabila yao, hivyo hawakuweza kuleta mabadiliko kama Umar na Hamzah.
Kwa hiyo hakukuwa na utafutwaji wa Nusra kutoka kwa watu wa Makkah kwa kutopatikana masharti hayo mawili, bali mjini Makkah kulikuwa na Daawah kwa Uislamu, Na hakukuwa na mwitiko kwa Uislamu kutoka kwa watu wa nguvu na himaya ndani ya Makkah wenye uwezo wa kuleta mabadiliko; hivyo basi hakukuwa na Talab An-Nusrah (ufafutwaji wa Nusra) mjini Makkah, bali Makkah ilikombolewa kwa ufunguzi.
Kwa hivyo Mtume (saw) alikuwa akijitambulisha kwa makabila yenye nguvu na himaya na kuwalingania kwa Uislamu kwanza kisha kutafuta Nusra kwao wanaposilimu. Haya hapa ni baadhi ya yaliokuja juu ya hayo katika Seera:
Kwanza: kutoka katika Sira ya Ibnu Hisham:
1- Utafutaji wa Nusra kutoka kwa Thaqif:
[Amesema Ibn Ishaq: Alipokufa Abu Twalib Maqureysh walimfanyia maudhi Mtume (saw) ambayo hawakuwahi kumfanyia katika uhai wa ami yake Abu Twalib, Akatoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwenda Twaif, akitafuta Nusra kutoka kwa Thaqif, na himaya kwao dhidi ya watu wake, Na akitarajia wamkubalie alichokuja nacho kutoka kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla,Akatoka kuwaendea akiwa pake yake.
Asema Ibn Ishaq: Yazid bin Ziyad alinihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Kaa’bi Al Quradhiy, Asema: Mtume (saw) alipofika Twaif, alikusudia kundi la Thaqif, Hao walikuwa wakati huo ni mabwana wa Thaqif na masharifu wao, nao ni ndugu watatu: Abd Yaleel bin Amr bin Aasw, Masu’d bin Amr bin Umair, na Habib bin Amr bin Umair bin Awf bin U’qdata bin Ghayrata bin Awf bin Thaqif. Na mmoja wao alikuwa na mwanamke wa Kiquresh kutoka Banu Jumah, Mtume (saw) akaketi nao na kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, akazungumza nao juu ya yale aliyowajia ya kumnusuru kupitia Uislamu, na kusimama naye dhidi ya watakaomkhalifu katika watu wake. Mmoja wao akamwambia: angeirarua nguo ya Kaa’ba ikiwa Mwenyezi Mungu ametumiliza, akasema mwengine: “Kwani Mwenyezi Mungu hukupata mwengine wakumtumiliza asokuwa wewe?”, Akasema watatu: “Wallahi kamwe sitozungumza na wewe!, kwani ikiwa wewe ni Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama unavyosema, basi wewe ni hatari kukurudishia maneno, na ikiwa wamsingizia Mwenyezi Mungu uongo, basi haifai mimi kuzungumza na wewe”, Mtume (saw) akasimama kutoka kwao akiwa amekata tamaa na kheri ya Thaqif.
2- Mtume kujitambulisha kwa Banu Aamir Ibn Swa’swa’ah
Asema Ibn Ishaaq: Al zuhriy amenihadhia kwamba Mtume (saw) aliwaendea Banu Aamir bin Swa’swa’h, akawalingania kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla, akijtambulisha kwao. Akasema mtu miongoni mwao- anayeitwa: Bayharata bin Firaas, asema Ibn Hishaam: Firaas bin Abdillah bin Salamata (Al khayr) bin Qushair bin Kaa’bi bin Rabii’ata bin Aamir bin Swa’swa’h: “Wallahi lau mie ningemchukua huyu kijana wa Kiquresh, ningewatafuna Waarabu kupitia kwake”, kisha akasema: “Je, waonaje sisi tukikupa Kiapo cha utiifu (Baya’h) juu ya jambo lako kisha Mwenyezi Mungu akakupa ushindi dhidi ya wanaokukhalifu, je, jambo hili litakuwa kwetu baada yako?” Akasema (saw):
«الْأَمْرُ إلَى اللّهِ يَضَعُهُ حَيْثُ يَشَاءُ»
“Jambo hili lipo kwa Mwenyezi Mungu analiweka atakapo.” Akasema: akamwambia: Je, walenga shingo zetu tuzitoe muhanga kukulinda wewe dhidi ya Waarabu, kisha Mwenyezi Mungu akikupa ushindi jambo liwe kwa wasiokuwa sisi? Basi hatuna haja na jambo lako, wakamkatalia…]
Pili: kutoka kwa kitabu cha Al-Bidaya Wa Al-Nihaya cha Ibn Kathir Al Dimishqiy
[Asema: “Kisha tukafika katika mkao wenye utulivu na heshima, mara tukawaona wazee wenye vyeo na mapambo, akatangulia Abubakar akasalimia – Asema Ali: na Abubakar alikuwa akitangulia katika kila kheri – Abubakar akawaambia: Ni kaumu gani nyie? Wakasema: Ni kutoka Shayban bin Thaa’laba, akamgeukia Mtume (saw) akasema: “Bi Abi anta wa ummi” (Neno linaloashiria heshima na kujitolea muhanga kwa ajili ya Mtume (saw) baada ya hawa hakuna izza katika jamii yao.
Na katika riwaya: Watu wao hawana udhuru baada ya hawa, Hawa ndio nyota ya asubuhi katika watu wao, hawa ni nyota ya asubuhi.
Na katika miongoni mwa alikuwemo Mafruq bin Amr, Hani bin Quswaybah, Muthanna bin Haarithah, na Nuu’man bin Sharik, na aliyekuwa karibu na Abubakar katika Jamaa ni Mafruq bin Amr, Na Mafruq bin Amr aliwashinda katika uzungumzaji na ufasaha, na alikuwa na tezi mbili zinazoanguka kifuani mwake, na alikuwa amekaa karibu zaidi na Abubakar katika Jamaa wote.
Abubakar akamwambia: “Vipi idadi yenu?” Akasema: “Sisi twazidi Alfu na Alfu hawashindwi kwa uchache”. Akamwambia: “Je, vipi nguvu zenu na himaya?” Akasema: “Ni juu yenu juhudi na kila watu wana bidii”. Akasema Abubakar: “Je vita ni namna gani kati yenu na maadui zenu?” Akasema Mafruq: “Hakika sisi ni wakali katika mapambano tunapokasirika, sisi twatanguliza farasi wa kivita kuliko watoto, na silaha kuliko mashamba, na Nusra ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu mara anatupa ushindi mara tunashindwa inaonekana kana kwamba wewe ni ndugu wa Kiqureshi?” Akasema Abubakar: “Ikiwa mumefikiwa na habari kuwa Maqureish wana Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu basi huyu hapa”. Akasema Mafruq: “Hakika tumefikiwa na habari kuwa yanatajwa hayo je walingania nini ewe ndugu Mqureshi?”, kisha akamgeukia Mtume (saw), akaketi Abubakar akasimama akamfunika kwa nguo yake. Mtume (saw) akasema:
«أَدْعُوكُمْ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ، وَأَنْ تؤوونى وَتَنْصُرُونِي حَتَّى أُؤَدِّيَ عَنِ اللَّهِ الَّذِي أَمَرَنِي بِهِ، فَإِنَّ قُرَيْشًا قَدْ تَظَاهَرَتْ عَلَى أَمْرِ اللَّهِ، وَكَذَّبَتْ رَسُولَهُ، وَاسْتَغْنَتْ بِالْبَاطِلِ عَنِ الْحَقِّ، وَاللَّهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ»
“Nawalingania kushuhudia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee hana mshirika, na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na mnipokee na kuninusuru mpaka niweze kutekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu ameniamrisha kwayo, kwani Maquresh wamepinga Amri ya Mwenyezi Mungu, na wakamkadhibisha Mtume wake, na wakatosheka na batili badala ya haki, na Mwenyezi Mungu ametosheka na ni Mwenye kusifiwa”.
Akasema: Na huyu ni Muthanna Mzee wetu na bwana wa vita wetu. Akasema Al Muthanna: “Nimesikia maneno yako na nikaona uzuri wa kauli yako ewe ndugu wa Kiquresh, na yamenifurahisha uliyoyaongea. Na Jibu langu ni Jibu la Hani bin Qubaysah; tukiwacha dini yetu na kukufuata kwa mkao uliokaa nasi basi itakuwa tumeshukia kati ya mistari miwili mmoja ni Yamama, na mwengine ni Al samawa. Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):
«وما هذان الصريان؟»
“Mistari hii miwili ni ipi?”
Akamwambia: Ama mmoja wapo: ardhi yenye nguvu na ardhi ya Waarabu, ama nyengine: Ni ardhi ya Fursi na mito ya Kisraa, tumeingia katika ahadi ambayo aliichukua kwetu Kisra kuwa tusifanye chochote, wala tusimhifadhi mgeni. Huenda hili jambo unalotulingania ni katika linalochukiwa na wafalme, ama kwa upande wa biladi za Kiarabu basi hatia ya mmiliki husamehewa na udhru wake haukubaliki.
Ukitaka tukunusuru na kukulinda upande wa Waarabu basi tutafanya. Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):
«ما أسأتم الرد إذ أفصحتم بالصدق، إنه لا يقوم بدين الله إلا من حاطه من جميع جوانبه»
“Majibu yenu sio mabaya kwa kusema kwenu ukweli, Hakika hasimami na Dini ya Mwenyezi Mungu ila yule ambaye ataizunguka kwa pande zote.”]
4- Kisha ikawa Bay’ah ya Aqabah ya kwanza na ya pili na kufuatiwa na Hijra na kusimamisha kwa Dola. Na tamati ni kuwa Hakika kuwa tayari na kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu hakukupatikana katika watu wenye nguvu na hifadhi mjini Makkah ndani ya Miaka ya mwanzo ya Mtume (saw). Hakukupatikana kwao Uislamu kisha maandalizi ya kumnusuru Mtume (saw) kwa hiyo Mtume (saw) hakutaka Nusra yao ili kusimamisha Dola katika Makkah kupitia njia ya Nusra, akaitafuta kwa wale ambao yapatikana kwao fursa ya kuitikia Uislamu na wawe katika (Ahlil quwwah wal mana’h) watu wenye nguvu na mamlaka wanaoweza kuleta mabadiliko. Wakapata Maanswar Utukufu huu mkubwa Duniani na Akhera na huko ndiko kufuzu kukubwa. Kisha baada ya hapo Dola ya Kiislamu ikaikomboa Makkah kwa ufunguzi.
Nataraji haya yanatosheleza na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi na Mwenye hekima.
Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Rashtah
06 Safar 1443 H
13/09/2021 M
Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook