(Imetafsiriwa)
Hazina inayoshughulikia maswala ya watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema katika ripoti iliyotolewa mnamo Ijumaa 19/1/2018 kuwa watoto 270 waliuwawa nchini Iraq mwaka jana kwa sababu ya vita vilivyo anzishwa na serikali ya Iraq dhidi ya ISIS. Vita hivi pia vilisababisha watoto 1.3 milioni kukosa makao miongoni mwa 2.6 milioni waliokosa makao kutokana na vita hivi vya miaka mitatu. Kulingana na taarifa hiyo, watoto milioni nne katika mikoa ya Nineveh na Anbar waliathirika na ghasia hizo na watoto wengi walilazimika kushiriki katika vita safu za mbele. Taarifa hiyo ilifichua kwamba umasikini na mizozo ilisababisha kusita kwa mchakato wa elimu kwa watoto milioni tatu kote nchini Iraq, baadhi yao wakikosa kabisa fursa ya kukaa ndani ya darasa katika maisha yao yote, huku zaidi ya robo ya watoto wa Iraq wakiishi ndani ya umasikini.
Habari na takwimu hizi zilizo fichuliwa na taarifa hii – licha ya kuogofya kwake – sio mpya wala zakustaajabisha, kwani kwa miongo mingi, raia wa Iraq – hususan watoto na wanawake – wamekuwa wahanga wa mzozo wa kindani na vita vya kinyama, vilivyo anzishwa moja kwa moja na wakoloni, kama vile uvamizi wa Amerika nchini Iraq mnamo 2003, vita vya wakala kupitia vibaraka wao kama vile kuyaondoa majeshi ya Maliki kabla ya ISIS mjini Mosul iliyofuatiwa na Al-Abadi kuipiga vita ISIS na kuirudisha tena Mosul mikononi! Iraq haishi migogoro au vita, kila ukimalizika mmoja unafuatiwa na mwingine, na lengo kuu baina ya vita hivi na migogoro hii ni kuiangamiza nchi hii na kuyageuza maisha ya watu wake kuwa ya taabu ili kuyatumikia maslahi ya wakoloni hawa.
Ni dhahiri kutokana na ripoti hii na kupitia ripoti na habari nyinginezo zilizo chapishwa kwamba “ushindi mkuu” uliotangazwa na Haider Al-Abadi katika vita vyake dhidi ya ISIS ulikuwa ni ushindi dhidi ya watoto na wanawake, ushindi ambao mamia yao wameuwawa na kujeruhiwa na mamilioni yao kukosa makao. Ni ushindi ambao raia mjini Mosul na maeneo mengine wamenaswa ndani ya vinywa vya ISIS na majeshi ya Iraq, na hivyo basi kuteseka kutokana na njaa, ongezeko la hatari ya kuzuka kwa maradhi miongoni mwa watoto, hususan wachanga kutokana na ukosefu wa lishe bora na madawa, na watoto kutumiwa kama ngao za kibinadamu, na katika baadhi hali kulazimishwa kushiriki katika vita.
Kwa takwimu hizi zinazo fichua hali mbaya ya watoto wa Iraq na kuonya kutokea kwa mustakbali mbaya zaidi kutokana na viwango vikubwa vya umasikini na kutojua kusoma wala kuandika miongoni mwao, tunauliza: Je, huu ndio ugaidi ambao vita hivi vimewashwa kwa ajili ya kuumaliza?! Je, waanzilishi wa vita hivi na vifaa vyao sio magaidi halisi?!
Enyi Waislamu:
Mpaka lini vita vitaendelea kuwashwa katika biladi yetu na damu za vijana wetu na binti zetu kumwagwa? Mpaka lini wataendelea kuishi katika maisha ya mateso na katika hali ngumu, huku wakoloni wakivuna matunda ya vita hivi?! Je, wakati haujawadia kwa Umma wa Kiislamu kutoa tangazo la kurudia upya hadhi yake miongoni mwa mataifa?! Je, wakati haujawadia wa kung’oa wale watawala, vibaraka, na kuteua mahali pao mtawala mukhlis kututawala kwa Kitabu cha Mola wetu na kurudisha hadhi na izza yetu?! Je, nafsi hazitamani siku zile za izza ambazo kwazo Harun ar-Rashid aliyahutubia mawingu kunyesha mvua wakati wowote yapendapo kwani mavuno yake yatarudi katika hazina ya mali ya Waislamu (Bait ul-Maal al-Muslimeen)?! Je, nafsi hazitamani zile siku za fahari ambapo heshima na damu ya Waislamu zilihifadhiwa na kujibishwa shambulizi lolote dhidi yao, “Je, jibu hili ndilo munaloliona au ni lile munalolisikia?!” ndio, Wallahi, nafsi zinatamani. Kwa hivyo, je wapo miongoni mwa majeshi ya Waislamu wale watakaoitikia mwito huu na kunali kheri ya dunia hii na kesho Akhera kwa kuzirudisha siku hizo?!
(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيم)
“Na siku hiyo watafurahi Waumini. Kwa nusra ya Allah humnusuru amtakaye, Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].
Kitengo cha Wanawake
Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 7 Jumada I 1439 | Na: 007/1439 AH |
M. Jumatano, 24 Januari 2018 |