Adhabu ya mzinifu aliyeoa olewa [Muhsan Zani] katika Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

{Imetafsiriwa}

Swali

Assalamualaikum War.Wab. Naam,Sheikh wetu na Amir wetu ningeomba kuuliza swali na nataraji utalijibu.

Kuhusiana na haddi ya kuuwawa kwa muhswan limeainishwa katika hukm gani kulingana na fiqhi ya kiislamu? Kuna baadhi ya wasomi kama Sheikh Abu Zahrah ambaye anasema kuwa hukmu hii si katika kipengele cha huduud.Na imetiliwa nguvu na Sheikh Mustafa Zarqa ambae amesema hii ni katika hukmu za Takzir.Je rai yako ni ipi juu ya hili?

Allah Awajazi khair na naomba kujibiwa swali langu. (Mwisho)

Jibu

Wa Alaikum Salaam Wa Rahamtullahi Wa Barakatuh.

Wauliza Kuhusu adhabu ya mzinifu aliyeoa/olewa kwamba, Je hukmu hii ni ya kukatikiwa katika fiqhi Ya kiislamu? Na Je Ni katika Hududi, Ama ni Katika Ta’zeer kama wasemavyo baadhi ya wanazuoni wa zama hizi?.

Jawabu kwa swali lako ni kama ifuatavyo:

1-Adhabu ya mzinifu alieoa/olewa Kupigwa mawe hadi kufa, yaingia katika mlango wa hukmu za kisheria, wala sio katika mlango wa itikadi(Iman). Kwa hiyo, adhabu hii ni kama hukm nyenginezo za kisheria, sio sharti Dadili yake kuwa ni ya kukatikiwa ndipo itumiwe. Bali, yatosha tu kupatikana dhana yenye nguvu (ghalabat Al-Dhann)  , Kama inavyojulikana katika ilmu ya usulul fiqhi (Misingi ya Sheria)….. Kwa hiyo, haitoangaliwa dalili ya hii adhabu kuwa ni ya kukatikiwa au la, ili iweze kutumiwa. Bali  la muhimu ni dalili yake kuthubutu ktk sheria. Na zimekuja dalili sahihi, ambazo haziachi shaka yeyote kwamba, adhabu ya mzinifu aliyeoa/olewa ni kupigwa mawe hadi kufa, kama inavyoelezwa hapa chini.

2-Yaonekana baadhi ya wanazuoni wa sasa, hawafuati utaratibu sahihi katika kuvua hukmu za kisheria kutoka kwenye dalili zake, na hilo ni kwa sababu, wao hufanya bidii wakati wanapotafuta hukmu za kisheria, ili waende  sambamba na zama na kufikia rai ambazo zinaafikiana na maoni yaliyoenea ulimwenguni, ambayo yamelazimishwa na hadhara ya kimagharibi juu ya watu kwa jina la kanuni za kimataifa” na “makubaliano ya haki za kibinaadamu” na nyenginezo…. na hili jambo sio sawa, kwa sababu, kinachotakiwa kutafutwa ni hukmu ya Allah pekee, wala sio tu hukmu yoyote, wala hukmu inayoendana na rai, sheria, na maafikiano yanayoongoza dunia….Na la wajibu,  ni kuichkua hukmu ya kisheria kama ilivyo kwenye dalili zake, na kuifanyia kazi, na kuilingania ulimwenguni kote. Kwani ndio hukmu pekee inayowafaa wanadamu wote kwa Kua yatoka kwa ALLAH Mtukufu, Muumba wa watu, Mjuzi wa hali zao…
                      أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ
“Hivi asijue aliyeumba, naye ndie mjua siri, mwenye khabari?” {Almulk:14}.
أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ تَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ) 

“…Fahamuni,kuumba na amri ni zake.Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu,Mola mlezi wa viume vyote.”                   

Na kwahiyo, haitakiwi kuzigeukia kauli za wale wanaong΄ang΄ania kuenda na wakati, na kutaka kuafikiana na hadhara ya kimagharibi katika kuvua kwao hukmu. haijalishi wanafanya hivyo kwa kubanwa na hali ilivyo, ama kwa kutaka kuwaridhisha Makafiri wa Kimagharibi!.

3-Adhabu ya zinaa kwa mzinifu aliyeoa/olewa ni kupigwa mawe mpaka kufa, na kwa ambao hawajaoa/olewa ni kupigwa viboko mia (100). Nazo ni adhabu katika uislamu zinaingia kwenye mlango wa Huduud. Na tumefafanua vya kutosha hukmu za Adhabu ya Zinaa kwenye kitabu cha Nidhamu ya Adhabu. Na Nitakunukulia Kutoka Katika Hicho Kitabu Baadhi Yaliyoelezwa Katika Mlango Wa “Adhabu ya Zinaa”:

[Baadhi wanasema: adhabu ya mzinifu mwanaume/mwanamke ni viboko mia (100) sawa wawe wameoa/olewa, wala hakuna tofauti kati yao eti kwa sababu Allah amesema,

(الزانية والزاني فاجلدوا كل واحد منهما مائة جلدة ولا تأخذكم بهما رأفة في دين الله)
“Mzinifu Mwanamke, Na Mzinifu Mwanamume, Mtandikeni Kila Mmoja Wao Bakora Mia Moja, Wala Iisikushikeni Huruma Kwa Ajili Yao Katika Hukumu Ya Mwenyezi Mungu” [An Nur:2].

Wakasema:  Haifai kuacha kitabu cha Allah kilicho yakini, kwa sababu ya mapokezi ya mtu mmoja[akhbar al-ahad] ambayo yaweza kua ya uongo na pia kwakuwa kutapelekea kufuta hukmu ya qur΄an kwa sunnah, na hilo halifai.

Na wanasema wanazuoni wote wa kiswahaba na waliowafuata baada yao, kutoka miji yote, zama zote, kwamba mzinifu ambaye hajaoa/olewa ndie hupigwa bakora 100, na aliyeoa/olewa hupigwa mawe hadi kufa.Hii ni kwa sababu, Mtume S.w.a aliamrisha Maaiz R.a Kupigwa mawe hadi kufa na pia ni kwa Sababu, imepokewa kutoka kwa Jaabir Ibn Abdillah kwamba,” mtu mmoja alizini na mwanamke, Mtume S.w.a akaamuru apigwe bakora 100, akapigwa kisha Mtume  S.a.w  akaambiwa kua ameoa, basi Mtume S.w.a akaamuru apigwe mawe hadi afe”.

Na anayeangalia (kiundani) dalili, ataona kwamba kauli yake Allah:

(الزانية والزاني فاجلدوا كل واحد منهما مائة جلدة ولا تأخذكم بهما رأفة في دين الله)

 “(Mzinifu mwanamke, na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja wao bakora mia moja..” [An Nur:2]ni pana .

Hii ni kwasababu  neno “Azzaaniyah” na neno “Azzaaniy” Yote ni katika matamshi ya kuenea jumla. Kwa hiyo, yanawakusanya wazinifu walioa/olewa na pia ambao hawajaoa/olewa. Na kwa kua, imekuja Hadith Mtume S.w.a Akisema:
 “واغد يا أُنيْس إلى امرأة هذا فإن اعترفت فارجمها”…”

nenda ewe unais kwa mke wa huyu, akikubali (kua amezini) basi mpige mawe hadi afe”.

Pia imethubutu kwamba, Mjumbe wa Allah S.w.a aliamrisha Maaiz R.a Kupigwa Mawe, baada ya kuulizia ikiwa ameoa. kadhalika, Aliamuru S.w.a mwanamke wa kighamidi kupigwa mawe. na dalili sahihi nyenginezo mbali na hizo. Kwahiyo, itakua Hadith imeifanyia Aya Takhsis, na kumvua mzinifu ambaye hajaoa/olewa. Hivyo basi, hizi hadith hazikufuta hukmu ya aya. Ama Kuikhusisha Aya Kwa Hadith Yafaa, na hilo limetokea katikak aya nyingi ambapo, aya zimekuja zikiwa kijumla, halafu hadith zikaja kuifanyia takhswis.

Na hukmu  ya kisheria ambayo imeelezwa na dalili za kisheria -Qur΄an na Sunnah- ni kwamba, adhabu ya mzinifu ambaye hajaoa/olewa apigwe bakora 100 kwa kufanyia kazi qur΄an, na kutolewa mjini (kufungwa) mwaka mmoja kwa mujibu wa sunnah za Mtume S.w.a.

Ila, Kutolewa mjini inaruhusiwa, wala sio lazima, na ameachiwa Khalifah kuamua, akitaka atampiga viboko na kumtoa mjini kwa mwaka mmoja, na akitaka atampiga tu viboko bila ya kumtoa mjini. Lakini, haifai kumtoa mjini tu bila ya kumpiga viboko. kwa sababu, adhabu yake mzinifu huyu ni viboko hasa. Ama adhabu ya mzinifu aliyeoa/olewa ni apigwe mawe mpaka afe, kwa mujibu wa sunnah za Mtume S.w.a ambazo zimekuja kuifanyia Takhswis Qur΄an. Na yaruhusiwa mzinifu aliyeoa/olewa kupigwa bakora mia, kisha apigwe mawe mpaka afe. Na pia yaruhusiwa kupewa adhabu moja tu ya kupigwa mawe. lakini haifai huyu mzinifu kupigwa viboko peke yake. kwa sababu, adhabu yake ya lazima ni kupigwa mawe.

Ama dalili ya adhabu  ya mzinifu aliyeoa/olewa, ni nyingi: Kutoka kwa Abuhuraira R.a na Zaid Bin Khalid R.a asema, kwamba mtu mmoja katika wabeduwi alikuja kwa Mtume S.w.a akasema: “Nakuomba kwa ajili Allah, nihukumu kwa kitabu cha Allah”. Na akasema hasimu wake- naye ndie mjuzi kumliko-: “Ndio, hukumu kati yetu kwa kitabu cha Allah,”. Akasema Mtume S.w.a: “Sema. Akasema:Hakika mwanangu alikua muajiriwa wa huyu, akazini na mke wake. na mimi nikaambiwa kwamba, mwanangu adhabu yake ni kupigwa mawe, nami nikamfidia kwa mbuzi mia moja na kumuacha huru mtumwa, nikawauliza wenye elimu, wakaniambia kua, adhabu ya mwanangu ni kupigwa bakora 100, na kutolewa mjini mwaka mmoja, na kwamba, adhabu ya mke wa huyu ni kupigwa mawe.” Akasema Mjumbe Wa Allah S.a.w:

“والذي نفسي بيده لأقضين بينكما بكتاب الله، الوليدة والغنم ردّ، وعلى ابنك جلد مائة، وتغريب عام، واغدُ يا أنيس – لرجل من أسلم – إلى امرأة هذا فإن اعترفت فارجمها، قال: فغدا عليها فاعترفت فأمر بها رسول الله صلى الله عليه وسلم فرجمت”

“Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake!nitahukumu kati yenu kwa kitabu cha Allah mtumwa na mbuzi utarudishiwa. na mwanao apigwe viboko 100, na kutolewa mjini mwaka mmoja. Na Ewe Unais- Ni mwaanume kutoka ukoo wa Aslam-  Nenda kwa mke wa huyu, akikubali (kua amezini) basi mpige mawe mpaka afe” Akasema: “Akaenda Unais, na mwanamke akakiri. Basi Mtume S.w.a Akaamuru Apigwe Mawe. Mtume S.w.a aliamrisha aliyeolwa kupigwa mawe wala hakuamrisha kupigwa viboko.

Na Kutoka Kwa Shaabi Kwamba :”Ali r.a (alipotaka) kumpiga mawe mwanamke, (kwanza) alimpiga viboko siku ya Alhamisi, halafu akampiga mawe siku ya Ijumaa na akasema:”nimempiga viboko kwa (mujibu wa) kitabu cha Allah, na nimempiga mawe kwa (mujibu wa) Sunnah ya Mtume S.a.w”.

Na kutoka kwa Ubaadah Bin Swaamit amesema: Amesema Mtume S.w.a:

“خذوا عني، خذوا عني، قد جعل الله لهن سبيلاً البكر بالبكر جلد مائة ونفي سنة، والثيب بالثيب جلد مائة والرجم”

“Chukueni  Kutoka Kwangu! Chukueni Kutoka Kwangu! Hakika Allah amewapa njia (wananwake):mtu ambaye hajaoa/olewa akizini, basi ni viboko mia moja, na kutolewa mjini mwaka mmoja. na aliyeoa/olewa akizini, ni kupigwa viboko, na (kupigwa mawe) hadi kifo”.

Kwahiyo, Mtume asema adhabu ya aliyeoa/olewa ni viboko na kupigwa mawe. na ali amempiga viboko na (kisha) mawe.

Na kutoka kwa Jaabir Bin Samura, kwamba Mtume S.a.w aliamuru Maaiz Bin Malik Kupigwa Mawe na hakutaja kupigwa viboko. Na kwenye swahih Bukhari, kutoka kwa Sulaiman Bin Buraida kwamba Mtume S.a.w aliamuru wanamke wa Kighamidiyah na hakutaja kupigwa viboko. Na kwenye Swahih Muslim, kwamba Mtume S.a.w aliamrisha mwanamke wa Kijuhaina akafungwa nguo zake vizuri, kisha akaamrisha apigwe mawe na hakutaja kupigwa viboko. Kwa Hiyo, yaonyesha ya kwamba Mtume S.a.w aliamuru kupigwa mawe hadi kufa kwa aliyeoa/olewa na wala hakuamuru kupigwa viboko na akasema,

“الثيب بالثيب جلد مائة والرجم”

”Mzinifu alieoa kwa alieolewa,viboko mia na kupigwa  mawe hadi kufa”

Ikajulisha kwamba, kupigwa mawe ni lazima, ama kupigwa viboko yaruhusiwa, na ameachiwa Khalifah kuamua. Na imewekwa katika adhabu ya mzinifu aliyeoa/olewa kupigwa viboko na kisha mawe, kwa ajili ya kuzitumia hadith zote.

Na haipaswi kwa yeyote kusema  juu ya hadithi ya Ibnu Samurah kwamba eti Mtume S.w.a hakumpiga Viboko Maaiz, bali alitosheka tu na kumpiga mawe kwa hiyo, imefuta Hadith ya Ubaadah Bin Swaamit isemayo:

“الثيب بالثيب جلد مائة والرجم”

“na aliyeoa/olewa akizini, ni kupigwa viboko 100, na (kupigwa mawe) hadi kifo”.

Haifai kamwe kusemwa hivyo kwa sababu, haikuthubutu dalili inayoonyesha kua Hadith ya Maaiz ilikua baada ya Hadith Ya Ubaadah. Na pamoja na kutothubutu hilo, kutotajwa kupigwa viboko hakubatilishi na kufuta hiyo hukmu. Hivyo basi, kwa kutothubutu ushahidi juu ya ni gani iliyotangulia na gani imechelewa katika hizo Hadith mbili, kunazuia kufutwa hiyo hukmu, na pia hakuna kinachotilia nguvu Hadith mojawapo juu ya nyengine. Na iliyokuja katika Hadith Kuzidishwa mbali na kupigwa mawe, inazingatiwa kua ni jambo la kufaa wala sio lazima, kwa sababu lililowajibu ni kupigwa mawe tu, na zaidi ya hilo ni hiyari ya Khalifa kuamua, kwa kuzitumia hadith zote]. Mwisho wa nukuu kutoka Katika kitabu cha Nidhamul Uqubaat.

Kwa ufupi: Adhabu ya mzinifu aliyeoa/olewa ni kupigwa mawe mpaka kufa kama ilivyo kwenye Dalili Sahihi zilizothubutu kutoka kwa Sunnah za Mtume S.w.a kwenye Sahihi mbili (Bukhari na Muslim) na zenginezo katika vitabu vya Hadith.Kwa hiyvo inaingia katika adhabu za Hudud na wala sio katika adhabu za Taazir.
Na Mwenyezi Mungu ndie ajuaye zaidi.

Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

12 Muharam 1441 H/         

11/09/2019 M