Barua ya Wazi kwa Mufti na Maulama ndani ya Sultani ya Oman

 (Imetafsiriwa)

Kwa Maulama Waislamu ndani ya Sultani ya Oman hususan Mufti Mkuu Ahmad bin Hamad al-Khalil,

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Muslim aliripoti katika Sahihi yake katika mlango wa: “Ukarimu wa watu wa Oman” kutoka kwa Abu al-Wa’dh Jabir ibn Amr al-Rasibi: Nilimsikia Abu Barzah akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma mtu kwa kabila miongoni mwa makabila ya Waarabu. Walimchukia na kumpiga. Akarudi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kumsimulia (mateso aliyofanyiwa na watu wa kabila hilo). Hapo hapo Mtume akasema: «لَوْ أَنَّ أَهْلَ عُمَانَ أَتَيْتَ مَا سَبُّوكَ وَلَا ضَرَبُوكَ»“Lau ungelikwenda kwa watu wa Oman, wasingeli kuchukia wala kukupiga.”

Kwa hiyo tizama na huku rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako, namna Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyo elezea wema wa watu wa Oman kutokana na elimu yake juu ya uzuri na ukarimu uliomo ndani yao…Leo hii hususan sisi Hizb ut Tahrir pamoja na Ummah wa Kiislamu kwa ujumla tukijumuisha watu wa Oman tunawalingania muwe ndiyo sehemu ya amana ya Ummah kama mlivyokuwa hapo awali na mutekeleze jukumu lenu ambalo Mwenyezi Mungu amelifanya ni amana katika shingo za maulama nayo ni kuwahesabu watawala na kusitisha dhuluma wanapo kandamiza na kusitisha makosa yao wanapo kosea.

Ripoti za hivi karibuni kuhusu kauli iliyotolewa na waziri wa kigeni wa Oman kwamba Israel ina wasiwasi juu ya hatima yake na kwamba Waarabu wawahakikishie na kuondosha hofu yao; kauli hizi na mapokezi ya awali yaliyo fanywa na Sultan wa Oman kwa muhalifu Netanyahu inaonyesha kuwa watawala hawa hawaoni tena aibu kwa Mwenyezi Mungu au wanao muabudu  Mwenyezi Mungu. Wanaonyesha wazi ushirikiano wao na maadui wa Waislamu na umbile la Kiyahudi ili kumakinisha miguu yao katika uvamizi wa kidhalimu ndani ya Palestina na kumtizama mvamizi huyo adui kama ndiye muhanga na anayestahiki kuhurumiwa na kuhifadhiwa!

Maulama na masheikh ndani ya Oman, hususan wewe, mheshimiwa Mufti, munaheshimiwa na kukubalika kwa watu wa Oman na muna mahusiano mazuri miongoni mwa Ummah, kwa hiyo musiwavunje moyo wale waliowapa amana na kuwa ni kiigizo chema katika kusema ukweli pasina kuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Jukumu lako la kiShari’ah ni kwa uwazi na uaminifu kutangaza kuwa huna makosa kutokana na vitendo vya watawala wa Oman vya; kumakinisha mahusiano na mvamizi umbile la Kiyahudi, kutelekeza ardhi ya Palestina na msikiti mtukufu Al-Aqsa, kuwakaribisha watawala wa Kiyahudi na kuwaweka karibu na kuwawasilisha kama ndio muhanga walio kandamizwa, licha ya kuwa wao ni wavamizi, wakandamizaji na wauaji, na tekeleza Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«أَفْضَلُ الْجِهَادِ مَنْ قَالَ كَلِمَةَ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»“Jihadi Kubwa, ni kwa yule anaye zungumza neno la haki mbele ya kiongozi dhalimu” [Tirmidhi, Abu Dawood na Ibn Majah]. Kimya cha maulama juu ya udikteta na usaliti wa watawala kinatumiwa na watawala hawa kuhalalisha usaliti wao na kumakinisha nidhamu zao zilizo tungwa na wanadamu ambazo hazitokamani na itikadi ya Waislamu bali zinagongana nayo.  Hawajali hisia za watu bali wanahudumikia maslahi ya Wamagharibi na kumakinisha udhibiti wao juu ya nchi na watu na kuupiga vita Uislamu na kuweka vikwazo usirudi katika maisha ya Ummah kupitia utekelezwaji wake kama nidhamu kamilifu ya kutatua matatizo ya Waislamu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunawalingania watu wa Oman na maulama wa Oman walioko safu za mbele; tunawakaribisha ili wasonge mbele pamoja na Ummah katika njia ya kusimamisha tena utawala wa Mwenyezi Mungu. Watu wa Oman wanaupenda Uislamu na mioyo yao inatamani kutekelezwa kwa Uislamu na kupeana Bay’ah kwa Imamu anaye tawala watu kwa Kitabu na Sunnah na kuubeba Uislamu kwa ulimwengu kupitia Da’wah na Jihadi.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua (hatima yake).” [Al-Anfal: 27].

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  15  Sha’aban 1440 Na: 1440 H / 030
M.  Jumapili, 21 Aprili 2019