Chaguzi za Kidemokrasia: Hadaa inayorudiwarudiwa kwa Umma

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imemtangaza naibu wa Rais William Samoei Ruto kuwa Rais mteule katika uchaguzi uliomalizika hivi punde. Muda mfupi kabla ya tangazo hilo, makamishna wane wa IEBC walikanusha matokeo ya Urais kwa kusema; “yalifikishwa kwa njia isiyo wazi”.  Raila Odinda, mshindani mkuu wa Ruto katika uchaguzi huo, alikataa matokeo na kuapa kwenda Mahakama ya Juu kuhusu kushindwa kwa uchaguzi. Ukisifiwa na waangalizi wa kimataifa kuwa ni kiwango kikubwa na wa amani na “juu ya wastani”, uchaguzi huo ulikuwa na idadi ndogo ya wapigakura waliojitokeza katika kipindi cha miaka 15 huku wengi ya vijana wakisusia upigaji kura.

Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kusema yafuatayo:

Chaguzi za Kidemokrasia huwa ni mbinu tu za kimpito kuondoa utawala mmoja na kwa kuuleta mwengine kwa maana huhalalisha utawala ufuatao. Mchakato huu kwa hakika hauakisi wala kuonesha uhakika wa zoezi la upigaji kura kama kigezo msingi bali huwa ni kupeana uhalalishaji tu wa uongozi mpya. Kwa hivyo, zoezi zima la uchaguzi  ni sura ya kidanganyifu ya  kidemokrasia na ukweli kuwa uteuzi badala ya uchaguzi. Zaidi ya hayo, ‘uchaguzi huru, wa haki huku ukweli unabakia kuwa ni uteuzi tu wala sio uchaguzi. Fauka ya haya misemo ya ‘Uchaguzi huru, haki na uwazi’ ni turufu tu ya Wakoloni Magharibi ili kutunga udanganyifu unaoweka kikomo mabadiliko ya uchaguzi na ratiba inayoitwa ukomo wa muda.

Kuhusiana na suala la ususiaji wa kupiga kura,hii inaonesha bayana kwamba raia wengi na hasa vijana wamekosa imani kwa uongozi ambao kwa muda mrefu wameshindwa kutatua matatizo yao sugu. Raia wametambua kwamba viongozi wa kisiasa wana ubinafsi wa kisiasa ambao ndio kipaumbele kwao na nambari moja kuliko maslahi ya raia. Kiasili na kimaumbile mfumo wa Kibepari husababisha unyama wa kisiasa na uchu wa kupapia mali hivyo kunyima raia mahitaji msingi ya raia wa kawaida.

Tunaeleza bayana kwamba mfumo batili wa Kirasilimali ndio kiini kikubwa cha matatizo yote Kenya inayokumbana nayo miongoni mwake ni ubabe wa kutojali kwa wanasiasa, ufisadi uliozagaa, mfumuko wa bei na utovu wa usalama. Matatizo haya sio kwa Kenya tu bali ni kwa ulimwengu kwa ujumla. Ubepari umejikita katika kuwatajirisha matajiri na kuwanyonya maskini hatimaye kusababisha pengo kubwa kati ya matajiri na maskini. Tuna hakika kwamba katika uchaguzi wowote wa kidemokrasia katika kipindi na wakati wowote hautawahi kutoa uongozi unaodhihirisha uimarikaji wa kweli badala ya uongozi unaofanya kazi kwenye mduara wa  ushawishi wa madola ya kibepari ya kikoloni.

Kenya na dunia nzima inauhitaji mkubwa Uislamu na mfumo wake wa utawala (Khilafah) ulio na suluhisho ya wazi ya matatizo yanayowakabili wanadamu wote. Uislamu unaifafanua siasa kuwa ni kujali kwa dhati mahitaji ya watu na wala sio  kuwania madaraka miongoni mwa wanasiasa wanaopigania manufaa yao binafsi. Mfumo ambapo jukumu la vyama vya siasa halitakuwa kama vyombo dhidi ya maslahi ya Ummah. Badala yake watapewa jukumu la uangalizi ili kuhakikisha uongozi unatimiza wajibu wake na kuwafikishia raia wake wote.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya