Chinja Chinja Nchini Mali Yaua Watu 160

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Duru za kijeshi nchini Mali zimetangaza kukamatwa kwa watu watano juu ya tuhuma za kuhusika katika chinja chinja iliyouwa zaidi ya watu 160 kutoka katika kabila la Fulani katikati mwa nchi hiyo, mnamo Jumamosi, 23 Machi. Wawindaji miongoni mwa kabila la Dogon, ambalo lina historia ndefu ya uhasama pamoja na Fulani juu ya umiliki wa ardhi, wanashukiwa kutekeleza mauwaji katika kijiji cha Ogassogou, nyumbani kwa Fulani jamii ya wafugaji karibu na mji wa Mopti, katikati mwa Mali. Diwani mmoja wa eneo hilo, Oumar Diallo, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa “idadi ya vifo ilifikia hadi 160”, na “pengine huenda ikaongezeka zaidi” na kukataa kuwa shambulizi hilo ni “utakaso wa kikabila”.

Ripota mmoja wa AFP mnamo Jumatatu alisema nyumba nyingi katika kijiji hicho ziliteketezwa na maiti kutapakaa chini. Shahidi mwengine, aliyesaidia kuhesabu miili hiyo Jumamosi iliyopita baada ya mauwaji hayo na kusifia kukamatwa kwa watoto na wanawake katika majumba kabla ya kuchomwa moto, alisema: “Hawakumsaza yeyote. Waliteketeza kila kitu kwa gesi na kuuwa kila kitu ambacho kilikuwa kingali kinatembea kwa silaha za kijeshi”. Manusura mwenye umri wa miaka 75, Ali Diallo alisema: “Sijawahi kuona kitu kama hiki. Walikuja, wakawapiga risasi watu, wakateketeza majumba, wakauwa watoto.” Walitekeleza shambulizi la kuhofisha, ambalo kwalo waathiriwa waliuwawa kwa kupigwa risasi au kukatwa vichwa kwa mapanga, bila ya kuzuiwa. Shambulizi hili la kinyama lilitokea licha ya kuwepo kwa majeshi ya Mali na majeshi ya kuweka amani ya Umoja wa Mataifa yanayojulikana kama MINUSMA, yanayojumuisha vikosi 15,000, vilivyokuja Mali kwa lengo la kumakinisha usalama na ustawi.

Raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keita alijitokeza kutoa ahadi zake za kuimarisha usalama na kusema: “Tunahitaji usalama hapa – hii ndiyo misheni yetu”, akiapa “kupatikana haki”. Badala ya kutoa usalama huu kwa watu wake, alitafuta hifadhi kwa wakoloni Wamagharibi na kuwaonya juu ya matokeo ya kuanguka kwa utawala wake hafifu, ambao unalinda maslahi ya Magharibi eneo hilo. Wakati huo huo, Waziri Mkuu wake aliyasihi majeshi ya Umoja wa Mataifa kutojiondoa kutoka Mali baada ya kufeli kwao kumakinisha usalama wowote, akionya kuwa upunguzaji wowote wa majeshi ya MINUSMA utapelekea kuhatarisha “maendeleo finyo” yaliyopatikana ili kumaliza mzozo nchini Mali. Maiga katika hotuba yake katika Baraza la Usalama alisema, “Nchi yetu ni mithili ya bwawa dhidi ya hatari ya magaidi, na hatupaswi kudharau vipimo au uwezo wa harakati hii kutoka nje ya mipaka yetu au hata nje ya bara hili.” Ni usalama upi utakaopatikana na serikali hii iliyopoteza udhibiti juu ya maeneo makubwa ya nchi hii na kutangaza kufeli kwa usalama wake?

Ni muhimu kuzingatia kuwa ghasia si jambo geni nchini Mali; zimekuwa zikijirudia tangu 2012 kwa kuanza kwa mzozo wa kisilaha kaskazini na udhibiti wa makundi dhidi ya serikali katika miji mikubwa. Lakini uingiliaji kati wa Ufaransa, ukisaidiwa na majeshi ya kimataifa, umeongeza kiwango cha uhasama eneo hilo. Hali hivi karibuni imegeuka kutoka hali ya kawaida ya uhasama hadi unyama wa kikabila katikati mwa nchi hii. Inapaswa kuzingatiwa kuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati wa kujirudia kwa mawimbi ya utakaso wa kikabila tangu 2012, Waislamu wa Fulani walidhuriwa vibaya katika namna hii hii, ambapo makundi ya kisilaha yaliwauwa raia wasiokuwa na silaha na kisha kuteketeza na kuangamiza vijiji na miji. Hii ni licha ya uingiliaji kati wa Ufaransa na usaidizi wa kijeshi wa zaidi ya wawekaji amani 14,000.

Majanga haya haya hujirudia katika kila nchi ambako wakoloni makafiri wamepewa mamlaka juu ya Waislamu, kuanzia Bosnia na Herzegovina, kupitia Indonesia, Burma na biladi nyenginezo za Waislamu ambako giza limetawala. Na juhudi za viongozi wanaotafuta msaada wa makafiri na kuwaachia mkoloni nchi yao ili kukithiri ufisadi na ghasia na kueneza majanga ya ubaguzi wa rangi na mzozo wa kimadhehebu, juhudi zao hazitafaulu.

Kumakinisha fikra za Kiislamu katika mujtamaa na kuzileta katika uwepo na kisha kuzifanya zidhibiti mahusiano ya watu kutamaliza chuki ya kimadhehebu na ya kimajimbo na kuregesha usalama kwa biladi za Waislamu. Hili laweza kufanywa pekee kupitia kuinua mikono ya madhalimu kutokana na kupangilia mambo yetu, na kupitia kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu katika ardhi yake, ili tumridhishe Mola wetu na kufurahi duniani na Akhera. Ewe Mwenyezi Mungu, ziondoe hasira na ghadhabu zako kutoka kwetu, Ewe Mwenyezi Mungu tulinde na zilinde biladi zetu.

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  26  Rajab 1440 Na: 1440 AH / 028
M.  Jumatano, 03 Aprili 2019