Demokrasia: Chombo cha Matumaini Hewa

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Huku siku zikisonga kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 9 Agosti,2022, ushindani mkali ni kati ya Naibu rais William Samoe Ruto anayeongoza muungano wa Kenya Kwanza na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Wagombea hawa wawili and wafuasi wao wanafanya kampeni kila pembe ya nchi wakiahidi wapiga kura kuleta mabadiliko na kuimarisha maisha ya watu.

Kutaja majina mapya ya miungano;Azimio la Umoja na Kenya Kwanza, wanasiasa wameibua matarajio yao ya kisiasa kwa kuahidi wapiga kura matumaini hewa,jambo linalothibitisha wazi sura danganyifu ya Demokrasia. Miungano hii mipya ya kisiasa imejengwa juu ya msukumo wa maslahi ya kibinafsi yanayoooneshwa kwa raia kuwa mazuri kwa watu.

Katika taifa ambalo limegawanyika mno katika misingi ya kikabila na kimaeneo hali ambayo imekuwa ni dharura kutumika kwenye chaguzi yoyote ile ya Kidemokrasia kwa sababu idadi ya namba ndio kiambajengo msingi cha kufikia kwenye hatamu za uongozi.Kwa bahati mbaya,maamuzi msingi ya kuimarisha hasa maisha ya raia wa kawaida hupuziliwa mbali huku kipaumbele ikiwa ni maslahi ya kibinafsi ya kisiasa.Kwa namna yoyote ya matokeo ya uchaguzi bado raia wa kawaida atabakia akisota kwenye msoto wa kimaisha.

Tunasema, chaguzi hizi zinafichua wazi sura halisi ya urongo wa siasa ya Kidemokrasia;raia kuhadaiwa na kupewa ahadi za urongo kwa kuambiwa kwamba sanduko la kura ndio njia pekee ya kufikia kwenye maendeleo, mabadiliko na mustakbali mwema. Kwa hakika kufeli kwa mfumo huu kumekuwa kweupe pepepe kwa watu kuuona. Demokrasia ni siasa rahisi mno katika soko la kisiasa kununuliwa na mabwenye wakubwa.

Kinyume chake, Uislamu haukuacha maisha ya watu kuchezewa na kutapeliwa na wanasiasa wenye uchu wa mali wanaohubiria raia Demokrasia kama njiya ya kuwafanya waende sambamba na maslahi yao ya kibinafsi. MwenyeziMungu SWT alituma Mtume wake wa mwisho na njia sahihi ya kimaisha isiyodanganya watu wala kuwaonyesha uwajibikaji wa kirongo na kushiriki kwenye siasa za pesa nane.Uislamu kwa hakika umewajibisha upangiliaji wa maisha ya watu kuwa ni jukumu kubwa lililoamrishwa na MwenyeziMungu kwa lengo la kufikia radhi za MwenyeziMungu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut Tahrir Kenya