Kila Mmoja Anabeba Da’awa Kwa Kadri Ya Uwezo Wake

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu La Swali

Kwa aamir al-Haj jaab

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam alaykum amiri wetu nataka kuuliza ni ipi Dori yangu katika kufanya kazi ya kusimamisba Dola na sina uwezo wa hilo.

Nasubiria Jibu kwani nataka muongozo kutoka kwenu nimetahayari na sijui niwe pamoja na nani nakuuliza wallahi nifanye nini

Jibu:

Waalaykum salam warahmatullahi wabarakatub, ewe ndugu yangu hakika Allah haikalifishi nafsi ila kwa uwezo wake, na watu wanatofautiana katika uwezo wao na katika ujuzi wao wa amali za Daawa na ufikishaji wao mzuri, na kadhalika wanatofautiana katika Elimu, Fikra na Hikma katika ufikishaji wa Mambo, na kadhalika wanatofautiana katika Kuwa na maalumati mapana katika kitabu cha Allah s.w.t na sunna za mtume wake s.a.w … Na haya yanapatikana kati ya wanadamu, na Taklif (kukalifishwa na majukumu) ni kwa kadri ya uweza.. Na hili liko bayana katika aya za quraan na hadith za mtume s.a.w :

Allah anasema:

 «لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا»

Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo

 «لا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلا مَا آتَاهَا»

Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa.

Na anasema mtume s.a.w:

 «لا تحقرن من المعروف شيئاً، ولو أن تلقى أخاك بوجه طلق‏»

(‏‏(‏رواه مسلم‏)‏‏)‏‏.

(Usidharau katika wema chochote hata kama utakutana na nduguyo kwa uso wa bashasha)

Na anasema mtume s.a w:

 «بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً»

( Fikisheni kutoka kwangu japo aya moja) ameitoa Bukhari

Kutoka kwa zaidi bin thabit: kutoka kwa mtume s.a.w asema:

((نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا حَدِيثًا فَحَفِظَهُ حَتَّى يُبَلِّغَهُ فَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ إِلَى مَنْ هُوَ أَفْقَهُ مِنْهُ وَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ لَيْسَ بِفَقِيهٍ))

( Allah amg’rishe Mtu aliyesikia kutoka kwetu maneno (Hadith) akayahifadhi na kuyafikisha kwani huenda mwenye kubeba Fiqhi Sio Faqihi) ameitoa twabrani katika al-kabir.

Basi ewe ndugu yangu unaweza kuamrisha mema na kukataza mabaya kwa kadri uwezavyo na yamkinika kwako ukafikisha aya au aya mbili na Sio Sharti uwe umehifadhi quraan tukufu au sunnah tukufu, ndipo uamrishe mema au kukataza maovu Bali ni kwa kadri ya uwezo wako, na umtake msaada Allah na kumtegemea, na Allah ndie anayewasimamia watu wema.

 

Ndugu yenu atwaa bin Khalil Abu rashta 

 

24 Ramadhani 1441H

Sawa na 17/05/2020M