Maandamano:Haki ambayo Haitofikisha kwenye uadilifu chini ya Mfumo wa Kibepari na Siasa yake ya Kidemokrasia.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

                             Maandamano yanayoendelea kushuhudiwa humu nchini ambayo kufikia sasa yamesababisha mauaji ya wakenya waso na hatia na kujeruhi wengi yameibua hisia katika jamii. Kwa munusaba huu, sisi katika Hizb ut Tahrir tunawajibika kubainisha yafuatayo:-
                             Malumbano ya kisiasa kati ya serikali na upinzani juu ya maandamano haya yako mbali mno na kutatua hali halisi ya watu. Kiukweli masaibu ya kiuchumi kwa jamii siku zote hutumiwa na kupatilizwa na wanasiasa kwa ajili ya kufikia kwenye malengo ya kisiasa. Sio Chama tawala na nadharia yake ya kiuchumi uangalizi wa maslahi ya watu wa chini (Bottom up Approach) na upinzani na msimamo wao wa kupinga utozwaji mkubwa wa kodi, yote haya katu hayawezi kukomboa watu kutokamana na majanga ya kiuchumi ya mfumo wa kiuchumi wa Kiliberali wa kirasilimali.                          

Tunakariri kwamba matatizo ya kiuchumi sambamba na suluhisho zinazowekwa katika kujaribu kutatua matatizo hayo, hayajafanywa nchini Kenya tu bali yamekuwa yakijaribiwa kote duniani. Utozaji ushuru, ruzuku kwa sekta ya uzalishaji na matumizi,ukopaji na kuongeza viwango vya riba kwenye mikopo na mifano yake yote hayo yameongoze msambao wa saratani ya Kiuchumi duniani. Suluhisho hizi za Kirasilimali kwa hakika zimeongeza mfumuko wa bei,ukosefu wa ajira, kuhujumu mitaji katika soko na kufisha kasi ya uzalishaji.
                          Mwisho twasema,Uislamu ambao ni rehema kutoka kwa Muumba wa Mwanadamu, Uhai na Ulimwengu, kihistoria unabeba ushuhuda jinsi wanadamu walivyonyanyuka kutoka minyororo ya utumwa wa kiuchumi wa riba na kutokuwa mateka wa wanasiasa wa zama zao hadi wakawa ni jamii yenye utendaji wa hali ya juu ulioweza kuondosha umasikini na kufanya maisha kuwa mazuri. Hivyohivyo,Uislamu ndani ya serikali ya Khilafah, itakayosimamishwa kwa mfumo wa Mtume SAAW hivi karibuni katika moja wapo wa nchi za Kiislamu, ndio utakao komboa walimwengu na kumwekea maisha yenye heshima.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir, Kenya