Mgogoro wa Madeni ya Kenya: Wanasiasa wanatupiana lawama huku wakidanganya watu kwa kutofichua hasa tatizo msingi lilioko (Ubepari)

Habari na Maoni

Habari:

Kenya inagubikwa na wasiwasi wa kiwango chake cha madeni kufikia shilingi trilioni la Sh9.1 trilioni. Sajili ya hivi punde ya deni la Hazina ya Kitaifa inaonyesha deni la taifa lilifikia Sh8.2 trilioni kufikia Desemba mwaka jana. Jumla ya mkopo wa nje ulikuwa Sh4.174 trilioni huku mikopo ya kimataifa ikiwa Sh1.782 trilioni, kibiashara Sh1.208 trilioni na baina ya Sh1.17 trilioni. Kenya huenda ikalazimika kukagua kikomo chake cha deni angalau mara mbili katika muda wa miezi 24 ili kuunda nafasi ya kukopa kwa serikali itakayokuja baada ya ile ya Uhuru Kenyatta. (Duru: Gazeti la The Star)

 

Maoni:

Huku Kenya ikukurubia uchaguzi mkuu, kampeini za kisiasa zinarindima ahadi chungu nzima zikaahidiwa wapiga kura kwamba watanasuliwa kutokamana na janga hili la madeni na umasikini. Huku haya ya kijiri kwenye fukuto hili la madeni wanasiasa wamo katika kutupiana lawama na kuficha hasa kiini cha tatizo hili nalo ni mfumo wa Kibepari.

Katika kipindi cha tandavu la Covid -19 uchumi duniani ulikua taabani na sasa baada ya janga hilo shauku na uchu wa kuomba mikopo umezidi. Kwa sasa Kwa sasa uwiano wa deni la taifa la Kenya kwa Pato la Taifa ni 70% zaidi ya kiwango kilichopendekezwa na IMF cha 40% ya Pato la Taifa. Hii ikimaanisha kwamba usimamizi wa masuala ya ndani ya nchi unaenda kwa kiwango kisichozidi asilimia 30 ya jumla ya mapato.

Kwan nchi ikikumbwa na matatizo ya kifedha ambao bila shaka utaendelea kizazi kwa kizazi jambo litakalohujumu raia na kuwasukuma kwenye shimo la utumwa. Kwa kuwa Kenya huomba pesa kwa kwa sarafu ya dollar hatua inayofanya sarafu ya nchi kuanguka thamani yake kwani malipo ya mikopo hupelekea kuwa na hitajio la sarafu ya kigeni.

.

Mduara huu mbaya utaendelea kuongezeka siku hadi siku na hakuna njia kabisa ya ukombozi wa kiuchumi na ufufuo katika mfumo wa sasa wa uchumi wa kibepari. Ili kukabiliana na janga hili la kukopa, ulimwengu unahitaji mabadiliko makubwa ya mfumo wa kiuchumi ambao utaangamiza kabisa aina zote za uchumi unaoidhinishwa na kodi. Mabadiliko hayo yanatokana na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unaotekelezwa chini ya Khilafah- dola huru ambayo sera zake za ndani na nje hazina ushawishi wa kigeni.

Athari za kuwa na mikopo mikubwa iliosheheni  riba huathiri bei za bidhaa na huduma zenye kodi ya juu hivyo kusababisha mfumuko wa bei unaoweka maisha ya raia kati ya mahali pagumu na mwamba. Katika Ubepari, madai ya mikopo ni utaratibu wa kifedha uliowekwa tangu kupitishwa kwa mfumo wa Fedha wa Fiat kama ilivyoainishwa katika mkutano wa Bretton Woods wa 1944. Mkutano huo uliweka misingi ya kikoloni na taasisi za fedha kama vile Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) udhibiti wa uchumi wa dunia. Kupitia Sera maarufu za Marekebisho ya Miundo (SAP) yenye masharti magumu.

 

Hali hii mbovu itaendelea kuongezeka siku hadi siku na hakuna njia kabisa ya ukombozi na mageuzii ya  kiuchum katika mfumo wa sasa wa kiuchumi wa kibepari. Ili kukabiliana na janga hili la kukopa, ulimwengu unahitaji mabadiliko makubwa ya mfumo wa kiuchumi utakaongamiza kabisa aina zote za chumi zinazojikita kwa msingi wa riba na ushuru.Mabadiliko hayo yanatokana na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unaotekelezwa chini ya Khilafah- dola huru ambayo sera zake za ndani na nje hazina ushawishi wa kigeni.

Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi kuu ya Hizb ut-Tahrir na:

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya  Kenya